Watumishi wa sekta ya afya katika halmashauri ya wilaya ya Nkasi Mkoani
RUKWA wameandaa mpango maalumu wa kushirikiana na wakunga wa jadi katika
wilaya hiyo ili kukabilina na changamoto za vifo vya mama na mtoto
wakati wa kujifungua.
Akizungumzia mpango huo mganga mkuu wa hamlashauri ya wilaya ya
Nkasi DKT GWAMAKA MWABULAMBO amesema hatua hiyo itasaidia kujenga uelewa
kwa wakunga wa jadi namna ya kutumia njia sahihi za kuzuia vifo wakati
wa kijifungua na kuwahamasisha mama wajawazito kujifungulia katika vituo
vya afya.
DOKTA GWAMAKA amesema wamefikia maamuzi hayo kutokana na ukweli kuwa
bado wakunga wa jadi wanaendelea kutumiwa kuwazalisha mama wajawazito
na hasa katika baadhi ya maeneo yaliyo mbali na huduma za afya kikao cha
pamoja kitasaidia kuwaelimisha wakunga hao wao kuwa msaada wa
kuwapeleka akina mama hao maeneo mahususi kwa ajili ya kujifungua
salama.



0 comments:
Post a Comment