![]() |
| Takriban watu 5,000 wamefariki Afrika Magharibi kutokana na Ebola |
Muuguzi kutoka nchi ya Mali amekufa
kutokana na ugonjwa wa Ebola, hiki kikiwa kifo cha pili kutokana na
Ugonjwa huo kudhibitishwa nchini humo.
Kesi hii haihusiani na ya kwanza ambayo msichana mwenye umri wa miaka miwili alikufa kutokana na Ebola mwezi oKtoba.
Shirika la Afya Duniani limetangaza mlipuko huu wa Ebola kama wa dharura duniani.
![]() |
| Mtoto wa miaka miwili ndiy alikuwa wa kwanza kufariki kutokana na Ebola Mali |
Kesi hii ya Mali imeibuka siku moja baada ya shirika la Afya Duniani kuwatoa watu ishirini na tano karantini waliodhaniwa kumkribia msichana wa miaka miwili aliyefariki oktoba .
Walikuwa miongoni mwa watu 100 waliokuwa karantini.
Kisa cha mtoto huyo kuugua na kufariki kutokana na Ebola kimewashangaza sana maafisa wakuu kwani inaarifiwa alisafiri kwa basi kutoka mjini Bamako kuelekea Guinea.





0 comments:
Post a Comment