SEKTA ya afya nchini imezidi kupata msukumo baada ya kuzinduliwa kwa
mradi wa maji katika zahanati ya Mkamba, Wilaya ya Temeke, Dar es
Salaam.
Mradi huo uliozinduliwa jana ulifanikiwa baada ya uwekezaji wa sh. milioni 50 uliofanywa na kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).
Kutokana na mradi huo, pia zaidi ya wakazi 80,000 wa Mkamba, sasa
watafaidika na maji safi na salama uliotekelezwa katika mradi wa kampuni
hiyo wa “Maji kwa Uhai”.
Mradi huu unajumuisha kisima cha maji, tenki la maji na pampu
inayotumia umeme wa jua na lina uwezo wa kuzalisha hadi lita 4,000 za
maji kwa siku.
Pia utasaidia katika kuwezesha utoaji huduma endelevu na shughuli
nyingine katika zanahati ya Mkamba ambayo hapo awali lilishindikana
kuzinduliwa kutokana na tatizo la uhaba wa maji masafi na salama.
"Tunafurahia kuwa kati ya wadau ambao wamechangia kutoa suluhisho la
changamoto ya uhaba wa maji,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Steve
Gannon.
Kabla ya mradi huo, upatakinaji wa maji safi na salama katika zahanati
hiyo ilikuwa changamoto, na hali hiyo ilisababisha kuchelewa kwa
ufunguzi wa zanahati.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema, ambaye alikuwa mgeni rasmi
alisema kukamilika kwa mradi huo katika kituo cha afya cha Mkamba ni
moja ya hatua muhimu za kuboresha huduma za maji katika hospitali
nchini.



0 comments:
Post a Comment