WAKATI joto uchaguzi wa Serikari za Mitaaa unaotarajiwa kufanyika
Desemba 14,mwaka huu, likipamba moto, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimezidi
kumeguka baada ya Mwenyekiti wa mtaa wa Matela kata ya Nyanguge, Wilaya
ya Magu, Joseph Maneno na wenzake wanne kutimukia CHADEMA.
Akiwakabidhi kadi za CHADEMA wakati wa mkutano wa hadhara uliyofanyika
kwenye uwanja wa Nyanguge Stendi, Mratibu wa Kanda ya Ziwa Magharibi,
Robert Bujiku alisema Serikali ya CCM imeshindwa kuwatatulia wananchi wa
Nyanguge kero ya maji tangu uhuru.
Alisema wananchi zaidi ya 5834 wa Nyanguge wamekuwa wakikosa huduma
hiyo muhimu licha ya nchi kubarikiwa rasilimali lukuki ambazo CCM
imeshindwa kuzitumia kuwaondolea umaskini.
Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Magu, Sylevester Makanyaga alisema
kuwa kumekuwepo na kesi mbalimbali mahakamani zinazosababishwa na uhaba
wa maji katika wilaya hiyo kutokana na wananchi hao kutafuta huduma hiyo
umbali mrefu.
Alisema serikali ilitakiwa kujenga tenki la maji lenye ujazo wa lita
laki 200,000 lakini wamejenga la ujazo wa lita 40,000 ambalo sasa
halifanyi kazi.
Mbali na Joseph Maneno, wafuasi wengine wa CCM waliotimukia CHADEMA ni
Paul Mabuku, Daud Marco, Julius Yayamhola na Samwel Silingi.



0 comments:
Post a Comment