Tuesday, 11 November 2014

Mabilioni yatengwa kwa umeme Mbinga

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga
Naibu wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga
JUMLA ya Sh bilioni 4.59 zinatarajiwa kutumika kupeleka umeme katika baadhi ya vijiji vilivyopo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbinga Mashariki, Gaudence Kayombo (CCM).

Mbunge huyo alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuweka umeme katika vijiji vyote vya wilayani Mbinga. Pia, alihoji kama Serikali inaweza kutoa programu ya umeme vijijini katika kila kijiji wilayani Mbinga.

Akijibu swali hilo, Kitwanga alisema Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatekeleza mradi wa kupeleka umeme katika wilaya ya Mbinga chini ya Mpango Kabambe wa Umeme Vijiji Awamu ya Pili.

Alitaja maeneo yatakayonufaika na mradi huo kuwa ni Mbagamao, Sekondari ya Dee Paul, Kigonsera Misheni, Kitanda, Lusonga, Mkumbi, Mkumbi Misheni, Utiri, Mkako, Kihaha, Masumuni na Matarawe.

0 comments:

Post a Comment