Monday, 10 November 2014

LOWASA awaasa viongozi kuwa na moyo wakujitolea


Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa MUNDULI EDWARD LOWASA ametoa wito kwa viongozi mbalimbali nchini kujenga moyo wa kujitolea katika kutatua changamoto mbalimbali zinatokea katika jamii.

LOWASSA ametoa wito huo jijini DSM wakati akizindua helkopta iliyonunuliwa na mchungaji JOSEPHAT GWAJIMA wa kanisa la saa ya ufufuo na uzima itakayotumika kusaidia jamii pindi yanapotekea majanga mbalimbali kama vile mafuriko na kuhudumia jamii katika maeneo yasiyofikika kwa urahisi.


HELKOPTA hiyo yenye namba 5H OLY SAA YA UFUFUO imezinduliwa na helkopta zingine tatu zinatarajiwa kuzinduliwa mwakani kwa lengo la kuhudumia jamii

0 comments:

Post a Comment