Shirika la madaktari wasio na mipaka
Medecins Sans Frontieres limesema kuwa viwango vya Ebola nchini Liberia
humo vimeshuka kidogo.
Hata hivyo shirika hilo limeonya kuwa kuna
ongezeko la visa vya ugonjwa huo nchini Guinea na Sierra Leone likisema
kuwa visa vya maambukizi vilivyokuwa vimepungua nchini Guinea
vimeongezeka tena.
Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa mafanikio nchini Liberia yanatokana na jitihada za kuzika maiti kwa njia iliyo salama.
WHO inasema kuwa karibu watu 5000 wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo.



0 comments:
Post a Comment