![]() |
| Polisi wa Ki Israel huko West Bank |
Mwanamke mmoja mwenye asili ya
Israel ameshambuliwa kwa kisu na kusababisha kifo chake katika eneo la
ukingo wa magharibi, tukio hilo limedumu kwa saa moja baada ya askari
mwenye asili ya Israel pia kushambuliwa na kuumizwa vibaya mjini Tel
Aviv.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameahidi kutumia kila mbinu ili kukomesha kabisa mashambulizi hayo.
Inasadikika kwamba mashambulio ya namna hii yamesababishwa na suala la kuendelea kuwepo kwa mpango wa makazi mashariki mwa Jerusalem na suala la haki ya kuabudu katika eneo nyeti la msikiti wa Al Aqsa ulioko mjini Jerusalem ambao pia hujulikana kama hekalu la milimani.




0 comments:
Post a Comment