Friday, 7 November 2014

Idadi ya wanawake wanaojifungua yaongezeka MBEYA

















Idadi ya wanawake wanaokwenda hospitali kujifungua imeongezeka Mkoani MBEYA ikilinganishwa na miaka MITATU iliyopita baada ya kuanza kutekelezwa kwa mradi wa matibabu bure kwa wajawazito mkoani huo.

Mganga Msaidizi katika Hospitali ya Rufaa ya MBEYA Kitengo cha Wazazi cha META Dakta GODLOVE MBWANJI amesema hayo mbele ya maafisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya waliofanya ziara ya kushitukiza katika hospitali hiyo kuangalia namna mradi wa matibabu bure kwa wajawazito unavyotekelezwa.

Mradi wa matibabu bure kwa akinamama wajawazito ulianzishwa mwaka 2012 kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Watu wa UJERUMANI na tayari wanawake zaidi ya LAKI MOJA NA ELFU 70 wa Mikoa ya TANGA na MBEYA wamenufaika na huduma hiyo ambapo pia umepunguza vifo vya akinamama wajawazito.

0 comments:

Post a Comment