KOCHA wa timu ya Taifa ya Judo, Zaidi Khamis ametaja kikosi cha
wachezaji 25 walioanza kambi ya kujiandaa na mashindano ya Kanda ya Tano
yatakayofanyika Januari mwakani.
Wachezaji hao ni washindi wa mashindano ya taifa yaliyomalizika
mwishoni mwa wiki ambapo yalilenga kuchagua kikosi hicho ili kuanza
maandalizi ya michuano hiyo ya kimataifa.
Waliochaguliwa ni Ahmed Magogo kilo 60, Abuu Mcheteko (60), Salmin
Bunu (60), Philipo Sabini (66), Omar Uledi (66), Emmanuel Mkande (66),
Moses Matulanda (66), Rahimu Ally (66), Andrew Mlugu (73), Mohamed
Kisandu (73), Seif Malulu (73) na Lucas Shirima (73).
Wengine ni Mohamed Korogombe (81), Gervas Chilipweli (81), Jeremia
Makame (81), Rajabu Chuhila (81), Geoffrey Mtawa (90), Mussa Kagoma
(90), Kusekwa Izengo (90), Augustino Simbili (90) na kwa upande wa
wanawake ni Matilda Temba, Pilly Mohamed, Diana Marcus, Paulina Mbezi na
Marry Awedasia.
Katibu Mkuu wa Chama cha Judo, Innocent Mallya alisema jana kuwa
tayari kikosi hicho kimeshaanza kambi kuanzia jana katika mazoezi
wanayofanya kwenye ukumbi wa Kisutu, Dar es Salaam.
Mallya alisema sababu ya kuweka kambi mapema ni kwa sababu
wamedhamiria kutetea ubingwa wanaoushikilia. Timu hiyo ndio mabingwa
mara mbili wa mwaka 2013 na mwaka huu, hivyo katika michuano ya mwakani
itakayoandaliwa na Tanzania, wanategemea kutetea ubingwa huo.
Katika mashindano ya Kanda ya Tano yatakayofanyika nchini mwakani,
yanatarajia kushirikisha Rwanda, Zanzibar, Burundi, Kenya, Ethiopia na
baadhi ya nchi nyingine za Afrika ya Kati ambazo zitapelekewa mialiko.
Mallya alisema washindi watakaofanya vizuri kwa upande wa timu ya
Tanzania na ile ya Zanzibar baadaye wataunda timu moja ya muungano kwa
ajili ya kujiandaa na Michezo ya Afrika maarufu ‘All African Games.



0 comments:
Post a Comment