Friday, 7 November 2014

Serikali kutunga sheria kali ya kudhibiti dawa za kulevya

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge WILLIAM LUKUVI
Serikali imeliambia Bunge kuwa imetunga Sheria mpya kali zaidi itakayoondoa changamoto zilizokuwa zikijitokeza wakati wa matumizi ya Sheria inayotumika sasa namba 9 ya mwaka 1995 ya Kuzuia biashara haramu ya Dawa za Kulevya.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge WILLIAM LUKUVI amesema kuwa Muswada wa Sheria hiyo mpya inayoitwa Sheria mpya ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, 2014 utawasilishwa Bungeni katika Mkutano unaoendelea Bungeni.

LUKUVI, hata hivyo amekiri kuwa Sheria zinazotumika sasa kudhibiti matumizi ya Dawa za Kulevya zinalegalega, jambo linalosababisha kuchukua muda mrefu kuamuliwa kwa Kesi za Dawa hizo.

0 comments:

Post a Comment