![]() |
| Waziri mkuu MIZENGO PINDA |
Waziri mkuu PINDA ametoa rai hiyo mkoani Arusha alipofungua mkutano wa kujadili mbinu na njia shirikishi za kupambana na vitendo vya kijangiri unaowashirikisha wadau kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Naibu Waziri wan chi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira UMMY MWALIMU,amesema wizara itashiriki katika kutoa hamasa na elimu katika kutunza mazingira kwani mazingira hayawezi kukamilika bila wanyama.
Wadau wa masuala ya utalii toka katika nchi mbali mbali Dunani hapo jana wamehitimisha mkutano wa siku MBILI wakupambana na vitendo vya kijangili pamoja na kukomesha uuzaji wa meno ya tembo ambapo nchi 9 zimesaini makubaliano yenye maazimio 20 yaitwalo azimio la ARUSHA,yakuzuia ujangili pamoja na masuala ya uhifadhi,
nchi hizo ni KENYA,UGANDA,BURUNDI,RWANDA, CONGO DRC,MALAWI na MSUMBIJI, ZAMBIA pamoja na TANZANIA.




0 comments:
Post a Comment