Friday, 7 November 2014

Mabadiliko ya tabia ardhi yajidhihirisha nchini BRAZIL

Mtaalamu wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi nchini BRAZIL amesema kuna uhusiano mkubwa kati ya uharibifu wa mazingira katika msitu wa AMAZON na mfululizo wa ukame nchini humo.
Dr. ANTONIO NOBRE amesema takwimu zinaonyesha kuwa ukame huo umekuwa na madhara makubwa katika mji SAO PAULO nchini BRAZIL.
NOBRE amesema vyanzo vya maji vinaweza kutoweka na kusababisha madhara kwa zaidi ya watu milion 20 iwapo hali hiyo ya uharibifu katika msitu wa AMAZON haitadhibitiwa.

Baada ya ukame kwa zaidi ya miaka MINANE mfululizo kina cha maji katika huo wa SAO PAULO kipo hatarini. Serikali nchini humo iansema imelazimika kuanzisha mgao wa umeme kutokana na uhaba wa maji ikiwa ni moja ya hatua za dharura .

0 comments:

Post a Comment