![]() |
|
Rais wa BURKINA FASO aliyejiuzulu BLAISE COMPAORE
|
COMPAORE aliyejiuzulu hivi karibuni amewatuhumu wapinzani wa serikali na jeshi kwa kufanya njama za kuzusha mgogoro nchini humo.
Kuhusu suala la kufanyika kwa kura ya maoni ili kukomesha mgogoro huko BURKINA FASO, COMPAORE ameongeza kuwa hatua hiyo huwenda haitapelekea kubadilishwa kipengee cha 37 cha katiba ya nchi hiyo.
BLAISSE COMPAORE ambaye alikuwa madarakani nchini BURKINA FASO kwa muda wa miaka 27, alilazimika kujiuzulu baada ya kukumbwa na malalamiko yaliyosababishwa na hatua yake ya kutaka kubadili katiba ya nchi hiyo ili aongeze muda wa kuweko madarakani.




0 comments:
Post a Comment