![]() |
| BERNAD MEMBE |
Taarifa hizo zinafuatia ripoti iliyotolewa na taasisi ya kimataifa ya MAREKANI inayojihusisha na uchunguzi wa masuala ya mazingira inayodai kuwa maofisa hao walinunua kiasi kikubwa cha pembe za ndovu.
Akitoa tamko la serikali bungeni mjini DODOMA ,waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa , BERNAD MEMBE amesema taarifa zinazosambazwa katika vyombo vya habari duniani zina lengo la kuichafua TANZANIA na kufifisha harakati zake za kupambana na ujangili na uuzwaji wa pembe hizo duniani.
Biashara ya pembe za tembo ambayo imekuwa ikipigwa vita duniani kote na mataifa mbali mbali kutokana na kutokuwa na tija zaidi ya kuogeza ujangili dhidi ya wanyama hao.




0 comments:
Post a Comment