This is default featured post 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Friday, 14 November 2014

Mwanamke mzazi abakwa hospitalini.

Mwanamke nchini Pakistan

Polisi nchini Pakistan wanawashikilia wanaume watatu kwa kosa la utumizi dawa za kulevya na ubakaji kwa mgonjwa aliyefuata matibabu katika hospitali ya serikali.

Mwanamke huyo, ambaye alijifungua hivi karibuni,alikwenda katika eneo la Burewala Mashariki ya jimbo la Punjab,iliko hospitali hiyo na alikwenda hapo akiwa na mumewe pamoja na mtoto wao mchanga kwa uchunguzi wa kitabibu.

Mume wa mwanamke huyo alimwacha mkewe kitambo kifupi tu na aliporejea eneo alipokuwa ,hakumkuta ila mtoto na begi la mwanamke huyo vimetelekezwa.

Saa kadhaa baadaye,alimpata mkewe akiwa amelala katika chumba chenye kiza ,kilichomo katika hospitali hiyo na kuthibitika kuwa amebakwa .

baada ya fahamu kumrejea mwanamke huyo alisema kwanza alichomwa sindano na wanaume hao watatu kisha wakaanza kumbaka kwa zamu.Wanaume wote hao ni wanafanya hospitalini hapo.

Putin alalama kuwekewa vikwazo

Rais wa Urusi,Vladmir Putin
Rais wa Urusi Vladmir Putin amesema Marekani na Umoja wa Ulaya, EU hautaathiri Urusi tu pekee isipokua uchumi wa dunia.

Putin amesema vikwazo hivyo vinakwenda kinyume na makubaliano ya kibiashara na kusema kuwa Umoja wa mataifa ndio ina haki kuweka vikwazo hivyo.

Vikwazo viliwekwa dhidi ya Urusi baada ya kuunga mkono kujitenga kwa jimbo la crimea lililokua sehemu ya Ukraine na kutuhumiwa kusaidia waaasi mashariki mwa nchi hiyo.

Putin ametoa kauli yake mjini Brisbane, Australia wakati huu wanapoelekea kwenye mkutano wa G20.
Viongozi wa dunia wakiwemo Putin, Rais wa Marekani,Barack Obama na Rais wa China,Xi Jinping wanakutana kwa siku mbili nchini Australia.

Watoto wazungumza lugha isiofahamika

Watoto wamekaa na mamayao wakila chakula.nchini Uganda watoto watatu waliofungiwa na baba yao kwa miaka saba wameanza kuzungumza lugha isiofahamika.

Watoto watatu kutoka kijiji cha Barca katika kaunti ndogo ya Aber Wilayani Oyam nchini Uganda wameanza kuzungumza lugha tofauti isiojulikana baada ya kufungiwa katika nyumba kwa miaka saba.
Lugha hiyo mpya imetajwa kuwa Leb -adam ikimaanisha lugha ya ubongo na jamii ya eneo hilo.

Inadaiwa kuwa baba ya watoto hao aliwafungia ili kuwalinda kutokana na hatari yoyote.

Kulingana ma gazeti la the monitor nchini Uganda,watoto hao hawajaathirika kiakili lakini hawawezi kuzungumza na watu wengine.Wanaamini tu kile baba yao anachowaambia.

Kulingana na mama yao watoto hao waliweza kuishi kwa kula mayai ya chura yaliochemshwa na majani,ambayo hula kila asubuhi na jioni na hutumia maji kutoka shimo lililochimbwa na baba yao.

Mama yao anasema kuwa baba ya watoto hao alimzuia kutozungumza nao hatua iliowafanya kutojifunza lugha ya kiluo wakati walipokuwa wadogo.

Mwanamke huyo amesema kuwa alionywa na baba huyo kutosema chochote kuhusu watoto hao.

Ndege ya kijeshi yaanguka Nigeria

Ndege ya kijeshi yaanguka nchini Nigeria.Ndege hiyo ni ya pili kuanguka.

Helikopta ya kijeshi ya Nigeria imeanguka katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo , ikiwa ni helikopta ya pili kupata ajali kwa muda wa chini ya wiki mbili 
.
Ajali ya hivi karibuni imetokea viungani mwa mji wa Yola, mji mkuu wa jimbo la Adamawa ambako kwa sasa jeshi linahangaika kukabiliana na uasi wa wanamgambo wa Jihad.

Kuna taarifa kutoka jimbo hilo kuwa wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa wakiwasukuma wanajeshi nje ya mji muhimu uliopo karibu na mpaka wa Cameroon . Wanafunzi katika chuo kikuu cha Modibbo Adama kilichopo katika mji wa Yola wanasema walisikia Helikopta ikianguka karibu na chuo chao .

Baada ya kuanguka ikafuatiwa na mfulurizo wa milipuko , kwani inaaminiwa kuwa ilikuwa inasafirisha silaha na zana nyingine za kijeshi kwa wanajeshi wanaopigana Boko Haram. Haijawa wazi ikiwa mtu yeyote aliekuwa ndani ya ndege hiyo amenusurika na kifo .
Ndege ya kijeshi yaanguka nchini Nigeria


Baada ya kusikia kelele , baadhi ya wanafunzi walianza kukimbia wakihofia kuwa wapiganaji wa jihad walikuwa wakiwashambulia Hii ni helikopta ya pili ya kijeshi kuanguka katika mji wa Yola wiki hii.

Wakati huo huo katika eneo la kaskazini kuna taarifa kuwa mji wa Mubi hauko tena mikononi mwa Boko Haram baada ya askari na vikosi vya usalama vya eneo hilo, wakiwemo wawindaji kuurejesha tena.

Lakini katika sehemu hii ya kaskazini ya jimbo la Adamawa bado hali ni mbaya na watu wamekuwa wakiukimbia mji huo ambao makundi ya Jihad yamekuwa yakijaribu kuuteka

Wednesday, 12 November 2014

Wanafunzi 70 wanusurika kifo

WANAFUNZI 70 katika Shule ya Msingi ya Filbertbay iliyopo Kwamatiasi wilayani Kibaha, Pwani, wamenusurika kifo baada ya moto mkubwa kuzuka ghafla katika bweni pamoja na majengo mengine ya shule hiyo.

Tukio hilo lilitokea saa nane usiku wa kuamkia Novemba 11, ambapo uliteketeza kabisa mabweni ya wanafunzi, chumba cha kulia chakula, maktaba na miundombinu nyingine ya shule hiyo.

Wanafunzi hao wamenusurika baada ya jitihada za uongozi wa shule hiyo kufanikiwa kuwanusuru licha ya kutokuwepo gari la zima moto.

Akithibitisha kutokea kwa moto huo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Ulrich Matei alisema, moto huo umezuka ghafla katika bweni namba nne la wasichana.

Matei alisema, moto huo ulianza na kusambaa kwa kasi ambapo pia uliteketeza bweni lingine la wavulana, madarasa 14 ya kawaida, ofisi moja, maktaba, ukumbi wa chakula na darasa moja la Compyuta na maeneo mengine ya mazingira ya shule hiyo.

Taarifa za awali kutoka kwa kamanda huyo zinabainisha kuwa, chanzo cha moto huo ni hitirafu ya umeme na kwamba uchunguzi unaendelea.

Mkurugenzi wa shule hiyo, Filbet Bay alikiri moto kuteketeza majengo hayo na kuongeza kuwa kwa sasa ni mapema mno kueleza thamani halisi ya madhara yaliyopatikana.

Tukio hilo la Moto limetokea siku mbili tangu tukio jingine kutokea na kuteketeza maduka katika eneo la Mailimoja mjini Kibaha huku gari la zimamoto likidaiwa kuwa katika matengenezo na hivyo kutegemea gari kutoka jijini Dar es Salaam

Mradi wa maji SBL kunufaisha Temeke

SEKTA ya afya nchini imezidi kupata msukumo baada ya kuzinduliwa kwa mradi wa maji katika zahanati ya Mkamba, Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam.

Mradi huo uliozinduliwa jana ulifanikiwa baada ya uwekezaji wa sh. milioni 50 uliofanywa na kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).

Kutokana na mradi huo, pia zaidi ya wakazi 80,000 wa Mkamba, sasa watafaidika na maji safi na salama uliotekelezwa katika mradi wa kampuni hiyo wa “Maji kwa Uhai”.

Mradi huu unajumuisha kisima cha maji, tenki la maji na pampu inayotumia umeme wa jua na lina uwezo wa kuzalisha hadi lita 4,000 za maji kwa siku.

Pia utasaidia katika kuwezesha utoaji huduma endelevu na shughuli nyingine katika zanahati ya Mkamba ambayo hapo awali lilishindikana kuzinduliwa kutokana na tatizo la uhaba wa maji masafi na salama.

"Tunafurahia kuwa kati ya wadau ambao wamechangia kutoa suluhisho la changamoto ya uhaba wa maji,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Steve Gannon.

Kabla ya mradi huo, upatakinaji wa maji safi na salama katika zahanati hiyo ilikuwa changamoto, na hali hiyo ilisababisha kuchelewa kwa ufunguzi wa zanahati.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema, ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema kukamilika kwa mradi huo katika kituo cha afya cha Mkamba ni moja ya hatua muhimu za kuboresha huduma za maji katika hospitali nchini.

CCM yazidi kumeguka

WAKATI joto uchaguzi wa Serikari za Mitaaa unaotarajiwa kufanyika Desemba 14,mwaka huu, likipamba moto, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimezidi kumeguka baada ya Mwenyekiti wa mtaa wa Matela kata ya Nyanguge, Wilaya ya Magu, Joseph Maneno na wenzake wanne kutimukia CHADEMA.

Akiwakabidhi kadi za CHADEMA wakati wa mkutano wa hadhara uliyofanyika kwenye uwanja wa Nyanguge Stendi, Mratibu wa Kanda ya Ziwa Magharibi, Robert Bujiku alisema Serikali ya CCM imeshindwa kuwatatulia wananchi wa Nyanguge kero ya maji tangu uhuru.

Alisema wananchi zaidi ya 5834 wa Nyanguge wamekuwa wakikosa huduma hiyo muhimu licha ya nchi kubarikiwa rasilimali lukuki ambazo CCM imeshindwa kuzitumia kuwaondolea umaskini.

Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Magu, Sylevester Makanyaga alisema kuwa kumekuwepo na kesi mbalimbali mahakamani zinazosababishwa na uhaba wa maji katika wilaya hiyo kutokana na wananchi hao kutafuta huduma hiyo umbali mrefu.

Alisema serikali ilitakiwa kujenga tenki la maji lenye ujazo wa lita laki 200,000 lakini wamejenga la ujazo wa lita 40,000 ambalo sasa halifanyi kazi.

Mbali na Joseph Maneno, wafuasi wengine wa CCM waliotimukia CHADEMA ni Paul Mabuku, Daud Marco, Julius Yayamhola na Samwel Silingi.

Nagu: Tunatambua mchango wa sekta binafsi

  Nagu: Tunatambua mchango wa sekta binafsi
Dr. Mary Nagu
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu amesema Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na sekta binafsi, hususan wawekezaji wa ndani na wafanyabiashara katika kukuza uchumi na kuongeza kasi ya maendeleo nchini. 

Alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa 15 wa mwaka wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), akisema kuwa shughuli mbalimbali zinazofanywa na sekta binafsi katika sekta zote za uchumi pia zimekuwa zikichangia kukua kwa pato la Taifa.

“Mchango wa TPSF katika ukuaji wa uchumi ni muhimu sana, hivyo serikali itafanya kila jitihada kuhakikisha mchango wa sekta binafsi unaongezeka ili tuweze kujenga uchumi imara na wa kisasa kama ilivyoelekezwa kwenye dira yetu ya maendeleo ya mwaka 2025,” alisema.

Aidha, Dk. Nagu alisema kukosekana kwa uwekezaji kwenye sekta zinazogusa maisha ya watanzania walio wengi kumesababisha washindwe kufikia azma ya kujenga uchumi imara na kuondoa umaskini.

“Ili kuondokana na jambo hili la baadhi ya watu kushindwa kuwekeza katika sekta zinazogusa maisha ya jamii, ni muhimu kuweka mikakati ya kuongeza idadi ya watanzania watakaoingia kwenye tabaka la kati katika sekta zote, kusudi tuongeze kiwango cha uwekaji wa akiba na kujenga soko litakalokuwa chachu ya kuongeza shughuli za uzalishaji na uwekezaji,” alisema.

Dk. Nagu pia alitoa wito kwa taasisi zote za serikali kutimiza wajibu wao wa kuhidumia sekta binafsi kwa kasi na viwango vya ubora wa huduma vinavyokubalika kimataifa ili kwa pamoja wafikie malengo ya kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi nchini.

Naye Mwenyekiti wa TPSF, Reginald Mengi alisema bila amani na utulivu katika nchi sekta binafsi haitaweza kufanya kazi yake kwa weledi unaotakiwa.

Mengi alisema suala la rushwa limekuwa likiongeza gharama za kufanyabiashara na kuiomba serikali kuchukua hatua madhubuti zitakazowezesha wafanyabiashara kufanya kazi kwa amani.

Dk. Slaa amvaa JK kashfa ya ujangili

Dk. Slaa amvaa JK kashfa ya ujangili
Dr. Slaa
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, amesema kwamba hakuna namna ambavyo Serikali ya Rais Jakaya Kikwete inaweza kukwepe kuhusishwa na tuhuma za ujangili wa meno na pembe za ndovu, kutokana na hatua yake ya kushindwa kuwachukulia hatua wahusika licha ya kutamba kwamba anawatambua pamoja na vinara wao. 

Kauli ya Dk. Slaa inakuja siku chache baada ya serikali kukanusha tuhuma zilizochapishwa na gazeti la New York Times la Marekeni, likinukuu ripoti ya Wakala wa Uchunguzi wa Mazingira (EIA) yenye makao yake jijini London-Uingereza, ikidai kwamba China ilinunua maelfu ya kilo za pembe za ndovu na kuzitorosha kwa kutumia ndege ya Rais wao, Xi Jinping wakati alipozuru Tanzania Machi 2013.

Katika habari hiyo, mwandishi Dan Levin anasema kuwa EIA imehusisha rushwa na biashara hiyo haramu nchini Tanzania hususani kwa wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa kutoka Chama tawala Cha Mapinduzi (CCM), kwamba Rais Kikwete alipoingia madarakani mwaka 2005, kulikuwa na tembo takribani 142,000 na wakati huu ambapo amebakiza mwaka mmoja kuondoka, idadi hiyo inakadiriwa kupungua na kubakia tembo 55,000.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Rais Kikwete alikabidhiwa orodha ya siri na vyombo vya usalama ikiwataja wahusika wakuu waliyo nyuma na biashara hiyo ya ujangili, wakiwemo wanasiasa mashuhuri na wafanyabiashara waliokaribu na CCM, lakini ni watuhumiwa wachache waliochunguzwa na kuchukuliwa hatua.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano, kuhusu tuhuma hizo, Dk. Slaa alisema kuwa ripoti hiyo inaeleza jinsi maofisa wa China walivyotumia fursa ya kidiplomasia ya kutokukaguliwa kwa mizigo yao, kupitisha bidhaa hizo haramu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA).

Alisema kuwa utetezi wa serikali uliyotolewa bungeni na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianao wa Kimataifa, Bernard Membe kwamba tuhuma hizo zinatokana na wivu na husda wa wabaya wa Tanzania ni dhaifu kwa kuwa haikuwahi kukubali hata mara moja juu ya tuhuma mbali mbali zilizoelekezwa kwake hata zile ambazo baadaye ilibainika ni za kweli.

Dk. Slaa alifafanua kuwa utetezi huo unaweza kufananishwa na ule uliotolewa wakati wa tuhuma za ufisadi wa fedha za EPA ambapo viongozi wa serikali ya CCM walisema ni kelele za chura zisizoweza kumzuia ng’ombe kunywa maji na kwamba baada ya wizi huo kudhihirika serikali ikaamua kuwaomba wezi warudishe fedha hizo kisha wasamehewe.

Aliongeza kuwa viongozi wa vyama vya siasa walishawapigia kelele viongozi wa serikali watoe kauli wakati meli inayomilikiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ilipokamatwa na meno ya Tembo nchini Vietnam na kwamba hakukuwa na kauli yoyote.

“Rais hakutoa kauli licha ya kwamba Kinana alikiri meli ni yake ila akasema hamjui aliyesafirisha mzigo huo. Rais alikaa kimya, vyombo vya ulinzi kimya utafikiri meno yale yalisafirishwa pasipo kuwa na vibali wala kupitia katika bandari yetu.

“Rais Kikwete akiwa nchini Uingereza, alisema anayo orodha ya majina 40 ya watu wanaojihusisha na ujangili na kwamba kinara wao yuko jijini Arusha, lakini mpaka leo hawajakamatwa. Ingekuwa kauli hii imetolewa na Dk.Slaa labda wangesema ni maneno yake, lakini Tembo wanaouawa wapo Selou,Serengeti na mbunga zingine nchini, Twiga wanaondoka, michanga ya dhahabu inabebwa ila husikii hatua zimechukuliwa,” alisema Dk. Slaa.

Alihoji kuwa katika hali kama hiyo huwezi kumuondoa Rais katika suala la kuwalinda wanyamapori wetu wasiuawe na majangili na kwamba kama kauli hiyo ingesemwa na watu wengine isingekuwa na tatizo, lakini kwa Rais lazima hatua zingechukuliwa.

“Lakini naawaambieni haya yatakoma pale Watanzania watakapokataa kugeuzwa shamba la bibi kwa kuachana na CCM, maana ndani ya chama hicho kwa misingi ya kifisadi waliyojiwekea hata aje malaika hawezi kukiongoza kwa uadilifu, isipokuwa ataungana nao katika ufisadi,”alisema.

Dk. Slaa alisema ni ajabu kwa Waziri Membe kukanusha kuwa hakukuwa na meno na pembe za ndovu katika mizigo iliyotajwa wakati yeye hakuwa miongoni mwa waliopakia mizigo hiyo, kwamba kiutaratibu mabegi ya kidiplomasia yanafungwa na watumishi wa balozi husika hali inayowafanya hata maafisa usalama wasiweze kujua kilichomo ndani yake kwa kuwa hayakaguliwi.

Kwa mujibu wa Katibu huyo, Membe ni mtu wa ajabu anayetafuta sehemu ya kukimbilia kwa ajili ya kujificha huku akijua hana ushahidi wa hayo anayoyasema. Alitolea mfano akisema kuwa siku za nyuma aliwahi kusema CHADEMA inafadhiliwa fedha na mataifa ya Magharibi kwa ajili ya kuiangamiza nchi bila kutoa uthibitisho hadi leo.

Alisema kuwa katika mataifa yanayoizunguka Tanzania, mambo haya huwezi kuyasikia kwa sababu viongozi wao wako makini na rasilimali za nchi.

“Tulisikia kule Kenya zilipokamatwa pembe za ndovu, zilichomwa. Tanzania ni mara ngapi tumekamata, mlimsikia aliyekuwa Waziri wa Maliasili, Balozi Khamis Kagasheki akiongoza ukamataji maeneo ya Msasani lakini mmesikia wapi zimeenda pembe hizo,”alihoji.

CCM wameshindwa, UKAWA tutawakwamua

CCM wameshindwa, UKAWA tutawakwamua
Mh. Mbowe

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa taifa liko kwenye mkwamo mkubwa wa kukosa uongozi imara kutokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushindwa, hivyo amewaomba Watanzania waunge mkono vyama vinavyounda Umoja wa Kitiba ya Wananchi (UKAWA) ili viwakwamue. 

Alisema kuwa moja ya sekta nyeti ambazo watawala waliyoko madarakani wameshindwa kuziboresha ni elimu, jambo linalosababisha taifa kuzalisha matabaka makubwa katika eneo hilo huku viongozi wakichukulia suala hilo kama jambo la kawaida.

Mbowe aliyasema hayo juzi akiwa katika siku yake ya mwisho mkoani Tabora baada ya kufanya mikutano 36 ndani ya siku nne, ambapo akiwa mjini Sikonge alisema kuwa kupitia ziara yake katika vijiji na miji ya mkoa huo, amezidi kujionea Watanzania wanavyohitaji mabadiliko ya mfumo na utawala.

“Nimepita maeneo ya vijiji na miji mbalimbali ya mkoa wa Tabora, nimejionea kwa macho yangu hali inayowakabili wakulima wa pamba, tumbaku, mpunga na mazao mengine kwa ujumla, nimeona hali inayowakabili wafugaji, jinsi wanavyopitia kwenye mateso ya kunyanyaswa pamoja na mifugo yao.

“Wakulima na wafugaji ni moja ya makundi ambayo kwa sasa yanaweza kuwa mfano mkubwa wa namna ambavyo watawala wa CCM wameshindwa, sera zao zimeshindwa, hawana mikakati tena ya kuwasaidia na kuwainua wananchi wa vijijini ni dalili ya nchi kukwama,” alisema.

Mbowe ambaye juzi aliingia mkoani Katavi kuendelea na ziara itakayokwenda katika mikoa sita, alisema kuwa; “ukitaka kuua taifa lolote duniani ua elimu ya taifa husika; viongozi wetu wameua taifa hili kwa kuharibu elimu yetu”.

“Sasa kama taifa tumekwama kabisa. Tumaini pekee la Watanzania kwa sasa ni kupitia vyama vinavyounda UKAWA na lazima tuanze kupitia kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji,” alisema Mbowe.

Lewis Hamilton atang'ara Abu Dhabi

Lewis Hamilton

Nguli wa zamani wa dunia wa mbio za magari Nigel Mansell amesema Lui Hamilton anayo nafasi moja iliyosalia kufanya vyema na kutinga fainali huko Abu Dhabi November 23.

Katika mahojiano maalumu na BBC Radio 5 Mansell anasema nafasi ya ushindi iko wazi mbele ya Lui na sasa ni uamuzi wake kuamua kushindwa ama kushinda!

Hamilton anaiongoza timu ya Mercedes kwa pointi 17, na nafasi ya kufanya maajabu anayo mikononi mwake.

Awali ni awali ,mwaka 1986 huko Australia kwenye

Mbio za Langa langa zilishuhudia William akiukosa ushindi hivi hivi baada ya kupata pancha . lakini yeye anasema hana tofauti na bata, mzoefu wa kupata,!

Alisahau maumivu ya tairi kukosa upepo na kuukosa ushindi pale alipojiona ana bahati ya mtende kuota jangwani baada ya kupata tuzo ya Sports Personality of the Year zitolewazo na BBC kakosa huku kapata kule!

Kama wewe ni shabiki sugu wa michezo!Tuzo hizo zimewadia tena ingia katika mtandao wa BBCSWAHILI.COM utapata maelekezo ya namna ya kupiga kura kumchagua mchezaji umtakaye, akwae tuzo hiyo ya BBC SPORTS PERSONALITY OF THE YEAR, na Mshindi atatangazwa baadaye mwezi ujao kazi kwako.

Hodgson ammwagia sifa kemkem Rooney

Siku ya jumamosi England itakipiga na Slovenia, ambapo Rooney atatimiza mechi yake ya 100

Kocha wa England Roy Hodgson amemsifu nahodha wa timu hiyo ya taifa Wayne Rooney kabla hajacheza mechi ya 100 katika michuano ya michuano ya ulaya mwaka 2016, ambapo England itakutana na Slovenia.

Rooney (29), alianza kuichezea timu ya England akiwa na miaka 17 mwaka 2003 na ni mfungaji wa nafasi ya nne akiwa ashatia nyavuni magoli 43.

Rooney ana kadi sita nyekundu, mbili akiwa na England, Hodgson ameeleza. Kazi yake hii imekuwa na vikwazo ya kila namna lakini imemkomaza na kumkuza kiakili.

Akizungumza na Radio 5 ya BBC, Hodgson amesema kuwa Rooney ni mkombozi wa soka la uingereza, huhakikisha kuwa kila mmoja yuko sawa na anaridhika na kuhakikisha kuwa hakuna tatizo ndani ya kikosi.

Lilian Kamazima ambaye ni Miss Tanzania 2014 apatwa na kashfa ya uraia na kudaiwa anatoka Rwanda


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjK0mX3Wb0vh1vzCMgNKoN35Tij_EbTYyCuomGkESo79Wg9TGC5PtlUantkjpoqZik8yC9MLymNwPI6mUsbQ2cNWeGv0yZhnzVNPi99M_WB0cr4eVjqc4lYEjtX7Y69zoZRyqfE4gPLRT4/s1600/Miss+Tanzania+Lilian+Kamazima__Follow+us+on+Facebook,+Twitter+and+Instagram+@TubongeTZ.jpg
Miss Tanzania 2014 Lilin Kamazama
 
 Baada ya Sitti  Abbas Mtemvu  kuvua taji kwa tuhuma za kudanganya umri  na  kupewa  taji  hilo aliyeshika nafasi ya pili  kwenye shindano hilo la Miss Tanzania Lilian Kamazima mengine ya ibuka  kuwa siyo raia wa Tanzania na  kwamba  anatokea Rwanda


Muandaaji wa shindano hilo  Hashimu  Lundenga  amesema kuwa tetesi hizo siyo za kweli, “Sisi tunajua Lilian ni Mtanzania,  tunaangalia cheti cha kuzaliwa alichotuletea  kamati yetu ambacho kinaonyesha alizaliwa Tanzania, pia ni Mtanzania, hayo yanayosemwa kwamba Lilian siyo Mtanzania hatuyajui kabisa”, alisema Lundenga


?'

CAF yawaza na kuwazua

Kombe ambalo mwenyeji anasuasua

Shirikisho la kanda kanda barani Africa CAF ,bado labangua bongo pa kupatia hifadhi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015.

Fununu zinaashiria huenda Angola wakafunika kombe na kuwa mwenyeji wa fainali hizo.
Endapo Angola nao wakileta za kuleta, jicho la tatu litaelekezwa kwa Gabon ama Nigeria.

Sintofahamu hii ,imekuja baada ya Morocco kukimbiza ubawa wake wakiuhofia ugonjwa wa Ebola
Naye Mcheza mpira wa zamani wa Nigeria Efan Ekoku ametoa ya moyoni alipoongea na BBC:

Asema Inakatisha tamaa,karibu kabisa na michuano hiyo, hatujapata mwenyeji !?

Lakini nazikubali sababu zilizotolewa na Morocco kuangalia usalama wa jamii yao sasa na baadaye.

Kwa muda mfupi ulosalia CAF wana kazi ya ziada kupata mwenyeji aliye tayari kwa kombe la mataifa ya Africa

Saa ghali zaidi duniani yanunuliwa

 Saa ghali zaidi duniani iko Uswiss  
Saa ghali zaidi duniani imenunuliwa mnadani huko Geneva,Uswiss kwa gharama ya dola za kimarekani milioni 21.3.

Saa hiyo imetengenezwa kwa kutumia karati ishirini na moja za dhahabu na ina uzito wa nusu kilo,saa hiyo iliyoundwa kwa mbwembwe ilitengenezwa mahsusi kwa ajili ya mtoto wa mfanya biashara,Henry Graves mnamo mwaka 1930.

Na ilimchukua miaka nane kwa watengeneza saa maarufu wa Uswis kuikamilisha hiyo saa ghali ambaye ni Patek Philippe.

Saa hiyo ilinunuliwa siku mbili tu baada ya mmiliki wa mwisho kufariki dunia kutoka falme za kiarabu Saud Bin Mohammed Al-Thani.

Mmiliki huyo alikuwa na madeni mengi ambayo yangemgharimu nyumba yake kuuzwa na hivyo akaikabidhi saa hiyo kwenye nyumba ya mnada ya Sothebys.

Watoto wafunzwa fikra za Osama Pakistani

Abdul Aziz Ghazi anamilikia shule nane zinazofundisha msimamo wa Bin Laden

Kiongozi wa kidini nchini Pakistani anatoa mafunzo ya fikra za Osama bin Laden kwenye shule za dini kwa Wanafunzi takriban 5,000.ingawa serikali ya nchi hiyo inapambana na wanamgambo wa Taliban kaskazini magharibi mwa Pakistani, haina mipango ya kuzifungia shule zinazotoa elimu kwa watoto kuunga mkono wanamgambo wa Taliban.

Imamu wa msikiti mmoja mjini Islamabad Abdul Aziz Ghazi amesema wana malengo sawa na Taliban lakini amesema hawatoi mafunzo ya kijeshi.

Kiongozi huyo amesema wanatoa mafunzo kuhusu misingi ya Jihad ila ni juu ya wanafunzi kupata mafunzo ya kijeshi baada ya kutoka shuleni hapo.

Ghazi anamiliki shule nane za kidini yaani Madrasa,moja ya shule yake iliwahi kufanya ziara ya kwenda kukutana na Osama Bin Laden nchini Afghanistan.

Hivi sasa wasichana 3,000 na wavulana 2,000 wanasoma kwenye taasisi zake.

Mitaala ya shule zake inatoa mafunzo ya kusoma Quran, kiarabu na thiolojia,hesabu na sanaa inaonekana kuwa masomo ya kidunia, vitabu vingi vimeandikwa na Ghazi na kuchapishwa katika shule hizo zenye vyumba vya kuchapisha.

Katika moja ya shule, kuna maktaba iliyopewa heshima ya jina la bin Laden

Baba Mtakatifu:G20 kumbukeni maskini

Baba Mtakatifu Francis


Baba Mtakatifu Francis ametaka viongozi duniani wanaoshiriki mkutano wa G20 mjini Brisbane kuwafikiria watu masikini ulimwenguni.

Amewataka Viongozi hao kupata ufumbuzi wa kuimarisha hali ya maisha ya watu walio masikini.

Viongozi wa nchi 20 zilizo na uchumi mkubwa wanakutana Brisbane nchini Australia mwishoni mwa juma hili kujadili maswala mbalimbali yahusuyo uchumi.

Kiongozi huyo wa juu wa kanisa katoliki amesema pia mkutano huo unatarajiwa kujadili hali ya mambo mashariki ya kati.

Amewataka viongozi kutotupia kisogo maisha ya watu yaliyo hatarini na kuonesha matumaini kuwa mkutano huo utatathimini kuinua maisha ya watu walio masikini na kupiga vita hali ya ukandamizaji ambao haukubaliki.

Mkutano wa G20 utaanza siku ya jumamosi.

Njia ya uzazi wa mpango hatari India

Madaktari wasio na ujuzi huhatarisha maisha ya Wanawake


Chama kikuu cha upinzani cha Congress nchini India kimeitisha mgomo katika jimbo la Chhattisgarh ambako wanawake 13 wamepoteza maisha kutokana njia za uzazi wa mpango zinazotolewa kwa njia ya upasuaji.

Wanawake sitini wako hospitalini kati yao 20 wako kwenye hali mbaya baada ya upasuaji huo.
Jopo la madaktari kutoka mjini Delhi wamefika katika jimbo hilo kusaidia hali hiyo ya dharula.

Serikali ya Chhattisgarh imetoa amri kufanyika uchunguzi kuhusu vifo vilivyojitokeza, huku waziri Kiongozi, Raman Singh akisema kuwa tukio hilo limetokea kutokana na uzembe wa madaktari.

Familia za waathirika, wote kutoka familia masikini zimeahidiwa kulipwa fidia ya takriban dola za marekani 6,600.

Maafisa wa afya wanne wamesimamishwa kazi na madai dhidi ya Daktari aliyefanya upasuaji yameshafikishwa Polisi.

Lakini chama cha Congress kimefanya maandamano kushinikiza Waziri wa afya Amar Agrawal kujiuzulu.


Waathirika kutokana na upasuaji huu wameahidiwa kupatiwa fidia


Namna ambavyo upasuaji huu hufanyika:


upasuaji huu hufanyika kwa kuziba mirija ya uzazi ambayo hubeba mayai kutoka kwenye Ovari kwenda tumboni, hubanwa kwa kutumia vitu mfano wa vibanio au pete ndogondogo au kwa kukata mrija.Hatua hii huzuia mayai na mbegu za kiume kukutana, hivyo mimba haiwezi kutungwa.

Mayai nayo kutoka kwenye ovari kama kawaida, lakini badala yake yatapotelea mwilini.
Waathirika kutokana na upasuaji huu wameahidiwa kupatiwa fidia
Njia hii huwa ya mafanikio ikiwa itafanyika inavyopaswa na mtaalam wa hali ya juu, hata hivyo kuna madhara ambayo huweza kujitokeza.

Madhara

Kuna hatari ya kuharibika kwa ogani nyingine wakati wa operesheni . Damu huweza kutoka kwa wingi pia maambukizi, pia njia hii ya uzazi wa mpango ni ya kudumu , hali haiwezi kurejea tena kama awali kama inavyokua kwa njia nyingine za uzazi wa mpango.

Mamlaka nchini India imekua ikipigia upatu sana swala la uzazi wa mpango kwa miongo kadhaa kwa ajili ya kuwashawishi watu kuwa na familia ndogo.

Ebola:Kifo cha pili charipotiwa Mali

Takriban watu 5,000 wamefariki Afrika Magharibi kutokana na Ebola


Muuguzi kutoka nchi ya Mali amekufa kutokana na ugonjwa wa Ebola, hiki kikiwa kifo cha pili kutokana na Ugonjwa huo kudhibitishwa nchini humo.

Maafisa wanasema kuwa muuguzi huyo alikuwa amemtibu raia aliyewasili nchini humo kutoka Guinea katika kituo cha afya cha Pasteur jijini Bamako, kituo ambacho kwa sasa kimewekwa karantini.

Kesi hii haihusiani na ya kwanza ambayo msichana mwenye umri wa miaka miwili alikufa kutokana na Ebola mwezi oKtoba.

Shirika la Afya Duniani limetangaza mlipuko huu wa Ebola kama wa dharura duniani.

Mtoto wa miaka miwili ndiy alikuwa wa kwanza kufariki kutokana na Ebola Mali


Kesi hii ya Mali imeibuka siku moja baada ya shirika la Afya Duniani kuwatoa watu ishirini na tano karantini waliodhaniwa kumkribia msichana wa miaka miwili aliyefariki oktoba .

Walikuwa miongoni mwa watu 100 waliokuwa karantini.

Kisa cha mtoto huyo kuugua na kufariki kutokana na Ebola kimewashangaza sana maafisa wakuu kwani inaarifiwa alisafiri kwa basi kutoka mjini Bamako kuelekea Guinea.


Tuesday, 11 November 2014

NICK MINAJI, AWAONGOZA WASHINDI WA TUZO ZA MTV EMA 2014 HUKO GLASGOW



Nicki Minaj, Beyonce, Katy Perry Justine Bieber ni miongoni mwa washindi wa tuzo za MTV Europe Music Awards (MTV EMA 2014) zilizofanyika Jumapili Nov. 9 huko Glasgow, Scotland
Nicki Minaj ndiye alikuwa host wa tuzo hizo ambaye pia alitumbuiza.
Orodha kamili ya washindi:
Best Video
Iggy Azalea – “Black Widow ft. Rita Ora”
Katy Perry – “Dark Horse ft. Juicy J” — WINNER
Kiesza – “Hideaway”
Pharrell Williams – “Happy”
Sia – “Chandelier”
Best Alternative
Fall Out Boy
Lana Del Rey
Lorde
Paramore
Thirty Seconds to Mars — WINNER
Best New
5 Seconds of Summer — WINNER
Ariana Grande
Charli XCX
Kiesza
Sam Smith
Best Female
Ariana Grande — WINNER
Beyoncé
Katy Perry
Nicki Minaj
Taylor Swift
Best Look
Iggy Azalea
Katy Perry — WINNER
Nicki Minaj
Rita Ora
Taylor Swift
Worldwide Act
Dulce Maria
Alessandra Amoroso
5 Seconds of Summer
Fifth Harmony
Bibi Zhou — WINNER
Dawid Kwiatkowski
Best Live
Beyoncé
Bruno Mars
Justin Timberlake
Katy Perry
One Direction — WINNER
Best Rock
Arctic Monkeys
The Black Keys
Coldplay
Imagine Dragons
Linkin Park — WINNER
Best Male
Ed Sheeran
Eminem
Justin Bieber — WINNER
Justin Timberlake
Pharrell Williams
Best World Stage
Afrojack
B.O.B
Ellie Goulding
Enrique Iglesias — WINNER
Fall Out Boy
Flo Rida
Hardwell
Imagine Dragons
Kings of Leon
Linkin Park
Nicole Scherzinger
Pharrell Williams
Simple Plan
The Killers
Best Song With a Message
Beyonce – “Pretty Hurts” — WINNER
Meghan Trainor – “All About That Bass”
Alicia Keys – “We Are Here”
Hozier – “Take Me to Church”
Arcade Fire – “We Exist”
Best Hip Hop
Drake
Eminem
Iggy Azalea
Kanye West
Nicki Minaj — WINNER
Best Pop
5 Seconds of Summer
Ariana Grande
Katy Perry
Miley Cyrus
One Direction — WINNER
Best Song
Ariana Grande – “Problem” ft. Iggy Azalea — WINNER
Eminem – “The Monster” ft. Rihanna
Katy Perry – “Dark Horse” ft. Juicy J
Pharrell Williams – “Happy”
Sam Smith – “Stay With Me”
Biggest Fans
5 Seconds of Summer
Ariana Grande
Justin Bieber
Nicki Minaj
One Direction — WINNER
Best Electronic
Afrojack
Avicii
Calvin Harris — WINNER
David Guetta
Hardwell
Best Push
5 Seconds of Summer — WINNER
Ariana Grande
Charli XCX
Cris Cab
John Newman
Jungle
Kid Ink
Kiesza
Lorde
Sam Smith
Zedd
Global Icon
Ozzy Osbourne

Wachezaji 25 kuunda timu ya Taifa ya judo

KOCHA wa timu ya Taifa ya Judo, Zaidi Khamis ametaja kikosi cha wachezaji 25 walioanza kambi ya kujiandaa na mashindano ya Kanda ya Tano yatakayofanyika Januari mwakani.

Wachezaji hao ni washindi wa mashindano ya taifa yaliyomalizika mwishoni mwa wiki ambapo yalilenga kuchagua kikosi hicho ili kuanza maandalizi ya michuano hiyo ya kimataifa.

Waliochaguliwa ni Ahmed Magogo kilo 60, Abuu Mcheteko (60), Salmin Bunu (60), Philipo Sabini (66), Omar Uledi (66), Emmanuel Mkande (66), Moses Matulanda (66), Rahimu Ally (66), Andrew Mlugu (73), Mohamed Kisandu (73), Seif Malulu (73) na Lucas Shirima (73).

Wengine ni Mohamed Korogombe (81), Gervas Chilipweli (81), Jeremia Makame (81), Rajabu Chuhila (81), Geoffrey Mtawa (90), Mussa Kagoma (90), Kusekwa Izengo (90), Augustino Simbili (90) na kwa upande wa wanawake ni Matilda Temba, Pilly Mohamed, Diana Marcus, Paulina Mbezi na Marry Awedasia.

Katibu Mkuu wa Chama cha Judo, Innocent Mallya alisema jana kuwa tayari kikosi hicho kimeshaanza kambi kuanzia jana katika mazoezi wanayofanya kwenye ukumbi wa Kisutu, Dar es Salaam.

Mallya alisema sababu ya kuweka kambi mapema ni kwa sababu wamedhamiria kutetea ubingwa wanaoushikilia. Timu hiyo ndio mabingwa mara mbili wa mwaka 2013 na mwaka huu, hivyo katika michuano ya mwakani itakayoandaliwa na Tanzania, wanategemea kutetea ubingwa huo.

Katika mashindano ya Kanda ya Tano yatakayofanyika nchini mwakani, yanatarajia kushirikisha Rwanda, Zanzibar, Burundi, Kenya, Ethiopia na baadhi ya nchi nyingine za Afrika ya Kati ambazo zitapelekewa mialiko.

Mallya alisema washindi watakaofanya vizuri kwa upande wa timu ya Tanzania na ile ya Zanzibar baadaye wataunda timu moja ya muungano kwa ajili ya kujiandaa na Michezo ya Afrika maarufu ‘All African Games.


Maelfu wamzika Amigolas, JK amlilia

MAELFU ya watu walijitokeza jana kumzika aliyekuwa mwanamuziki mahiri wa muziki wa dansi nchini, Khamis Kayumbu maarufu Amigolas katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.

Walikuwapo wasanii wa muziki, maigizo, wasanii wa zamani, wa sasa pamoja na makundi mbalimbali ya muzi ki. Mwili wa mwanamuziki huyo ambaye hadi mauti yanamkuta alikuwa kiongozi wa bendi ya Ruvu Stars inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), alipumzishwa kwenye nyumba yake ya milele saa tisa alasiri.

Mwanamuziki huyo aliyewahi pia kutamba na bendi ya Twanga Pepeta akiwa mmoja kati ya waanzilishi wake, alifariki juzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa.

Alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo alichangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya muziki wa dansi nchini. Alikuwa mahiri zaidi wa kucheza, kuimba, kutawala jukwaa pamoja na kuchombeza vionjo mbalimbali vya muziki.

Wanamuziki mbalimbali walimzungumzia mwanamuziki huyo kwa kusema kuwa alikuwa ni chachu ya maendeleo ya sanaa kwa kuwa alikuwa hana majivuno na alikuwa akiwasaidia wasanii wengi.

Mwanamuziki Robert Hega maarufu kama Katapila, alisema Amigolas alikuwa na maisha mazuri kwa wasanii wenzake hata nje ya kazi yake ya muziki.

Alisema alikuwa akishiriki katika kutoa mawazo ya kuendeleza muziki hata kwa wasanii wasiokuwa kwenye bendi aliyokuwapo.

“Huyu kwangu binafsi nilifanya naye kazi pale Twanga akiwa kama kaka yangu na alikuwa anajua muziki vyema kuliko hata ambavyo ilikuwa ikifahamika, lakini hakuwa na nyodo kabisa,” alisema Katapila.

Mwanamuziki mwingine, Muumini Mwinjuma alisema Amigolas alimshauri mengi na kumtia moyo kuhusu muziki. Moja kati ya nyimbo alizotunga mwanamuziki huyo ni Aminata alioimba akiwa na Twanga Pepeta.

Katika hatua nyingine, Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara kuomboleza kifo cha Amigolas.

“Nimehuzunishwa na kusikitishwa na taarifa za kifo cha mwanamuziki Khamisi Kayumbu kilichotokea tarehe 9 Novemba, 2014 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya ugonjwa wa moyo,” alisema Rais Kikwete katika salamu zake
.
Rais Kikwete alisema anatambua mchango mkubwa wa Amigolas, katika kuhamasisha maendeleo ya nchi kupitia sanaa ya muziki katika kuwafikishia wananchi ujumbe muhimu wa masuala mbalimbali ya kijamii na kiuchumi.

Amesema Kayumbu alikuwa mfano unaofaa kuigwa na wasanii wengine kote nchini.

“Kutokana na msiba huu, naomba upokee salamu zangu za rambirambi kwa kumpoteza mmoja wa wanamuziki mahiri hapa nchini, na rambirambi hizi ziwafikie pia wanamuziki wengine kote nchini kwa kumpoteza mwenzao,” alisema.

Azam FC yaleta kocha, ‘nduguye’ akina Kipre

George Nsimbe ‘Best’
George Nsimbe "Best"
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC wameimarisha kikosi chao kabla hata ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo kwa kusajili beki wa kati, Serge Wawa wa Ivory Coast.

Aidha, Azam FC imeleta Kocha Msaidizi mpya, George Nsimbe ‘Best’ na kumtupia virago Ismailla Diarra wa Mali ili kufuata kanuni za ligi zinazotaka klabu kusajili wachezaji watano wa kigeni.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Meneja wa Azam FC, Jemedari Said alisema Wawa aliwasili nchini jana na leo anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kusajili.

“Wawa ameshafika leo asubuhi (jana) na kesho (leo) atafanyiwa vipimo vya afya kama yuko safi. Tutamsubiri wakala wake tarehe 12 (kesho) aje tusaini mkataba,” alisema Said akimzungumzia beki huyo ambaye alikuwa akiichezea El Merreikh ya Jamhuri ya Sudan.

“Na pia tumevunja mkataba na Diarra ili kuwa na idadi sawa ya wachezaji wa kigeni.”
Alisema Diarra walisaini naye mkataba wa mwaka mmoja unaotarajiwa kumalizika Juni mwakani, hivyo wameshamalizana naye na kwa sasa mchezaji huyo yupo huru.

Hakucheza mechi hata moja ya Ligi Kuu Bara. Wawa anakuwa mchezaji wa tatu wa Ivory Coast kusajiliwa na Azam FC akitanguliwa na pacha wawili, mshambuliaji nyota Kipre Tchetche na kiungo Kipre Balou.

Kuhusu Kocha Msaidizi Nsimbe ‘Best’, Said alisema wameshamalizana naye na jana jioni alitarajiwa kurudi kwao Kampala kabla ya kuja kuanza kazi baada ya wiki moja.

“Tumemalizana na Best, tumesaini naye mkataba wa miaka miwili leo (jana) na jioni atakwenda kuweka sawa mambo yake ya kifamilia atarudi kuanza kazi rasmi wiki ijayo,” alisema meneja huyo.

Best anachukua nafasi ya Kally Ongala anayedaiwa kuwa na mpango wa kwenda nje ya nchi kuongeza elimu zaidi ya taaluma ya ukocha, ingawa taarifa zinadaiwa ametupiwa virago.

Best atasaidiana na Joseph Omog kuinoa Azam FC inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara. Azam FC imefanya mabadiliko baada ya kutetereka na kupoteza mechi mbili kwenye ligi.

Kwa sasa ina pointi 13 sawa na Yanga iliyo kwenye nafasi ya pili. Mtibwa Sugar ndio inaongoza ikiwa na pointi 15.

Ligi Kuu imefika katika raundi ya saba na imesimama kuanzia jana kupisha mechi za kalenda ya Fifa kati ya Taifa Stars dhidi ya Swaziland itakayochezwa Jumapili wiki hii mjini Mbabane na kisha michuano ya Kombe la Uhai na Kombe la Chalenji kwa njia za Afrika Mashariki na Kati ambayo pia iko katika hatihati.

Sare sasa bye bye – Phiri



Add caption








KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Patrick Phiri amesema kwa sasa hataraji kikosi chake kupata matokeo mengine ya sare baada ya ushindi bao 1-0 walioupata juzi dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Phiri alisema vijana wake walicheza kwa juhudi kubwa na kupata ushindi huo wa kwanza msimu huu na kufufua matumaini yao ya kunyakua taji la Ligi Kuu ya Tanzania Bara linaloshikiliwa na Azam FC.

“Naweza kusema matokeo ya sare kwa sasa ‘bye bye’ kwa sababu ushindi utatuongezea hamasa katika mechi zinazofuata na kutufanya tucheze kwa nguvu na kuweza kupata ushindi,” alisema Phiri.

Mzambia huyo alisema lengo lake ni kuhakikisha Simba inarudi katika kiwango chake kilichozoeleka na kumaliza mzunguko wa kwanza wakiwa kwenye nafasi mbili za juu ili iwe moja ya timu ambazo zinawania taji msimu huu.

“Hatupo mbali sana na timu zinazoongoza ligi kwa hiyo Simba bado ni moja ya timu zinazowania ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu kwa sababu ina uwezo wa kufikia pointi ilizonazo Mtibwa kama tutashinda mechi zetu zilizobaki,” alifafanua Phiri.

Akizungumzia mchezo huo wa juzi, alisema ulikuwa mgumu kwa sababu wapinzani wao, Ruvu Shooting ni timu nzuri na iliwapa upinzani mkali hasa katika kipindi cha kwanza na kumfanya aumize kichwa kutafuta mbinu za kupata ushindi.


“Nawapongeza sana mashabiki, viongozi pamoja na wachezaji wangu kwa kuonesha jitihada kubwa na kuhakikisha tunaondoka na pointi zote tatu, lakini mchezo ule hata Ruvu wangeweza kupata ushindi kulingana na upinzani ulivyokuwa uwanjani,” alisema Phiri.

Ushindi huo umeokoa kibarua cha Phiri aliyepewa mechi mbili kubadili matokeo ya sare na pia matokeo hayo yameivusha timu hiyo kutoka nafasi ya 10 iliyokuwa awali hadi ya saba ikiwa na pointi tisa kibindoni.
Tangu kuanza kwa Ligi Kuu, Septemba 20, mwaka huu, Simba imecheza mechi sita na kutoka sare zote, kabla ya ushindi wa juzi, na kuzua sintofahamu kubwa kwa viongozi, wachezaji, wanachama na mashabiki wake.

Inakwenda katika mapumziko ya kupisha michezo ya kimataifa ya kalenda ya Fifa na Kombe la Uhai na Kombe la Chalenji ikiwa na nguvu baada ya ushindi huo wa kwanza msimu huu. Ligi itarejea tena Desemba 26, mwaka huu.

Asilimia 13 ya Wakazi Mkoani Morogoro hawana vyoo

Ofisa Afya wa Halmashauri ya Manispaa Morogoro, Gabriel Malisa amesema halmashauri hiyo ina kata tano zenye wakazi wasio na vyoo, ambayo ni sawa na asilimia 13 ya wakazi wote wa manispaa hiyo.

Akizungumza ofisini kwake jana, Malisa alisema kuna kampeni maalumu inaendelea ili kukomesha tatizo hilo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha elimu inawafikia wakazi hao ili wajenge vyoo bora.

Alitaja kata hizo kuwa ni Kingorwila, Mzinga, Kauzeni, Bigwa na Mindu. Alisema kuwa mkakati uliopo ni kuhakikisha wakazi hao wanajenga vyoo ili kusaidia kuondokana na magonjwa ya kuambukiza.

Malisa alisema kuwa takwimu zinaonesha kuwa hapa nchini ni asilimia 22 tu za kaya za mijini, ndizo zenye vyoo bora. Alisema kuwa katika maeneo ya vijijini ni asilimia 9 tu ya wakazi walio na vyoo bora.

Alisema Manispaa hiyo itakuwa mwenyeji wa siku ya kunawa mikono na usafi wa mazingira kitaifa kuanzia Novemba 14 na kilele chake ni Novemba 19. Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni “Choo bora na mikono safi kwa afya bora, utu na usawa.”

Mabilioni yatengwa kwa umeme Mbinga

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga
Naibu wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga
JUMLA ya Sh bilioni 4.59 zinatarajiwa kutumika kupeleka umeme katika baadhi ya vijiji vilivyopo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbinga Mashariki, Gaudence Kayombo (CCM).

Mbunge huyo alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuweka umeme katika vijiji vyote vya wilayani Mbinga. Pia, alihoji kama Serikali inaweza kutoa programu ya umeme vijijini katika kila kijiji wilayani Mbinga.

Akijibu swali hilo, Kitwanga alisema Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatekeleza mradi wa kupeleka umeme katika wilaya ya Mbinga chini ya Mpango Kabambe wa Umeme Vijiji Awamu ya Pili.

Alitaja maeneo yatakayonufaika na mradi huo kuwa ni Mbagamao, Sekondari ya Dee Paul, Kigonsera Misheni, Kitanda, Lusonga, Mkumbi, Mkumbi Misheni, Utiri, Mkako, Kihaha, Masumuni na Matarawe.

Serikali yasikia kilio deni kubwa la MSD

HATIMAYE kilio cha wagonjwa kupoteza maisha na kuteseka, kutokana na uhaba mkubwa wa dawa katika hospitali nyingi nchini, kunakotokana na Bohari ya Taifa ya Dawa (MSD) kuishiwa dawa, kwa kutolipwa zaidi ya Sh bilioni 102 na Serikali, kimesikika.

Jana wabunge kadhaa walisimama na kuibana Serikali wakitaka sasa suala hilo litolewe maelezo, huku baadhi wakipinga hatua ya vikao vya Bunge kuendelea kama fedha hizo hazitalipwa.

Hatua hiyo ilitosha kuifanya Serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi Maalumu ambaye anakaimu pia nafasi ya Kiongozi wa Shughuli za serikali bungeni, Profesa Mark Mwandosya kuahidi kuwa tamko la serikali kuhusu hali ya vifaa tiba na dawa nchini litatolewa wiki hii.

Mbunge wa kwanza kulalamikia hali mbaya ya huduma za matibabu nchini, alikuwa ni Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Bulaya (CCM) ambaye aliomba Mwongozo wa Spika, na kuelezea namna wanawake wenye saratani ya shingo ya kizazi wanavyopata mateso, kutokana na kuharibika kwa mtambo maalumu wa mionzi katika Hospitali ya Saratani ya Ocean Road.

Alisema hali hiyo inatokana na mtambo wa pili katika hospitali hiyo kuwa mbovu kwa muda mrefu sasa bila kutengenezwa, hatua iliyofanya wagonjwa kutegemea mtambo mmoja uliokuwa umesalia, ambao nao sasa umeharibika.

Mbunge wa Viti Maalumu, Rukia Khasim Ahmed (CUF) yeye alipinga vikali hatua ya vikao vya Bunge kuendelea, huku deni la zaidi ya Sh bilioni 102 la MSD likishindwa kulipwa na serikali na kufanya wagonjwa kuendelea kuteseka.

Mbunge huyo ambaye alitoa hoja na kuungwa mkono na wabunge wengine, alisema hakuna sababu kwa Bunge hilo kuendelea na hivyo alitoa hoja ya kuahirishwa kwa Mkutano wa 16 na 17 wa Bunge unaoendelea ili fedha za wabunge, zikalipe deni la MSD.

Hatua hiyo ilitosha kumfanya Mwandosya kusimama na kutoa ahadi ya Serikali ya kuwasilishwa kwa tamko maalumu la Serikali bungeni wiki hii kuhusu hali ya vifaa tiba, ikiwemo pia suala la deni la MSD.

Mbali ya suala la MSD, Waziri Mwandosya akijibu mwongozo wa Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde (Chadema) kuhusu wakulima kukosa masoko na kulemewa na mazao ambayo sasa yanakaribia kuoza, pia alisema Serikali kupitia kwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza itawasilisha tamko wiki hii.

Ahadi hiyo ya Waziri Mwandosya ilipokelewa kwa furaha na wabunge wengi, ambao baadaye wakichangia kwenye muendelezo wa hotuba ya Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa 2015/2016, waliipongeza Serikali kwa ahadi ya kushughulikia suala hilo la MSD.

Tangu kuanza kwa Mkutano unaoendelea wa Bunge, suala la deni la MSD limechukua sehemu kubwa ya mjadala, hatua ambayo bila shaka ndiyo iliyoifanya Serikali kuamua kulitolea tamko kwa lengo la kueleza mikakati ya kuokoa maisha ya Watanzania wanaoteseka hospitalini.

Mbunge mwingine ambaye amewahi kupendekeza Bunge kuahirishwa ili fedha wanazolipwa zikalipe deni la MSD kuiwezesha Bohari hiyo kununua dawa, ni Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM), aliyetoa hoja hiyo wiki iliyopita.

Naibu Spika, Job Ndugai mara zote ambazo suala hilo limetajwa bungeni, amekuwa akisema ni suala zito na kubwa, lakini amekuwa akiwaomba wabunge kuvuta subira wakati Serikali ikiendelea kulifanyia kazi ili kupata ufumbuzi wa kudumu na wa uhakika.

Kampuni ya simu yamwaga ajira 2,000

 

KAMPUNI ya simu ya Viettel ya Vietnam inayokua kwa kasi duniani ambayo sasa inahamishia nguvu zake katika soko la Tanzania, imetangaza ajira kwa wasomi wa Tanzania zaidi ya 2,000.

Viettel ambayo uongozi wake wa juu ulikutana na Rais Jakaya Kikwete akiwa ziarani nchini Vietnam hivi karibuni na kuahidi kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya mawasiliano nchini, imetangaza nafasi hizo kupitia gazeti hili na gazeti lake dada la Daily News matoleo ya jana.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, Viettel inahitaji wataalamu wa karibu fani zote, huku kiwango cha chini kabisa cha elimu kikiwa stashahada, yaani diploma.

Wafanyakazi wanaohitajika ni wenye ujuzi katika masuala ya rasilimaliwatu, sheria, fedha, uhasibu, masoko, uchumi, mipango, takwimu, uwekezaji, ugavi, usafirishaji, utunzaji wa vifaa, umeme, simu, teknolojia ya habari na mawasiliano, biashara, utawala na uhusiano wa umma.

Tangazo hilo limeendelea kuonesha kuwa, waombaji wanatakiwa kutuma maombi yao kuanzia leo kwa njia ya baruapepe, mwombaji akitakiwa kutuma ujumbe unaoomba fomu kupitia anuani za makao makuu na pia mameneja wa kampuni hiyo walioko katika mikoa yote, Tanzania Bara na Zanzibar.

Moja ya anuani ya makao makuu inasomeka; viettelrecruiter@ gmail.com, ambapo mtumaji baada ya kuwasilisha ombi lake, atatumiwa fomu maalumu.

Mwenyekiti wa Viettel inayomilikiwa na Jeshi la Vietnam, Nguyen Manh Hung katika mazungumzo yake na Rais Kikwete, alisema kampuni yake inakusudia kuja na huduma bora zitakazomwezesha kila Mtanzania kumiliki simu ya kisasa (Smart phone), kutokana na punguzo kubwa la bei, licha ya ubora wa huduma zake.

Aidha, aliahidi Viettel itafunga huduma ya mawasiliano ya intaneti katika kila kijiji nchini, huku taasisi za umma kama vile shule, hospitali, vituo vya Polisi vikinufaika kwa kupatiwa huduma hiyo bila malipo yoyote.

Kwa mujibu wa Hung, kampuni yake inapanga kupunguza bei ya simu za kawaida hadi kufikia dola za Marekani 15, sawa na Sh 25,000 na kupunguza bei ya smart phone hadi kufikia dola za Marekani 40, sawa na Sh 65,000.

Sasa hivi, bei ya simu hizo ni kubwa zaidi ya kiasi hicho kinachokusudiwa.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa, kampuni yake itawekeza kiasi cha dola za Marekani bilioni moja (Sh trilioni 1.7) katika huduma za simu na huduma nyingine nchini Tanzania, hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi ya pili nyuma ya Peru kupata mfumo wa simu wa kisasa zaidi miongoni mwa nchi ambako kampuni hiyo ina shughuli zake.

Alisema ndani ya miaka mitatu tangu kampuni hiyo kuanza shughuli zake nchini, kiasi cha vijiji 4,000 ambavyo kwa sasa havina mawasiliano, vitapatiwa huduma hiyo katika awamu ya kwanza.