Sunday, 5 October 2014

Wazee waiomba Serikali kuwachukulia hatua watu wanao wanyanyasa katika kupata huduma za kijamii,Mkoani kagera.

Wazee mkoani kagera wameiomba Serikali kuwachukulia hatua watu wote wanao wanyanyasa katika huduma mbalimbali za kijamii na wale wanao jihusisha na  ukatili wakuwauwa vikongwe. 

Wakiongea katika Maadhimisho ya siku ya wazee Duniani wazee hao wamesema wamekuwa wakinyanyasika katika mambo mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya nakwamba Serikali inatakiwa kuchukua hatua Madhubuti za kuwawajibisha watu wote wanaojihusha na vitendo vya ukatili kwa  wazee ambao  wameshiriki katika kulinda amani na utulivu ulioko hapa Nchini ambapo wameongeza kuwa wazee wanatakiwa kulindwa na kuheshimiwa.
 
Katika taarifa yake kwa Mgeni Rasimi mzee Yolonimo Ijugo amesema wazee wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali ikiwemo kukubwa na magonjwa na kwamba Serikali inatakiwa kuangali upya suala la afya kwa wazee, nahivyo kuongeza kuongeza kuwa serikali inatakiwa kuimarisha ulinzi kwa wazee kwakua wamekuwa wakituhumiwa katika kesi mbalimbali ambazo maranyingi zimekuwa zikisababisha vifo visivyokuwa vya lazima kwa wazee.
 
Kwa upande wake Mgeni Rasimi katika hafla hiyo Nashoni Kabaye  amesema serikali  imejipanga vyema katika kuhakikisha kuwa inawasaidia wazee kuwasaidia katika kutoa huduma mbalimbali muhimu ambazo zinaweza kuwasaidia wazee wote hapa Nchini huku mratibu wa maadhimisho hiyo Lydia Lugazia amesema katika shirika lao wamekuwa na Changamoto mbalimbali katika kuwahudumia wazee nakwamba Shirikala lao linahudumia zazidi ya wazee elfu moja wanao hitaji kupata pesheni.

0 comments:

Post a Comment