Mtoto mwenye umri wa miaka (7) Mkazi wa nane nane mjini Morogoro amebakwa na mtu mzima mwenye umri wa miaka (53) na kumsababishia maumivu makali na kulazimika kupelekwa hospitali ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu
.
Akizungumza kwa uchungu mtoto huyo akiwa katika kituo cha polisi mkoani Morogoro amemtaja aliembaka kuwa ni Joseph Paula(53) ambaye ni ndugu wa Baba yake mzazi ambapo amesema mtuhumiwa alitumia mbinu ya kumtuma Dawa chumbani ndipo akambaka ambapo wazazi wa mtoto huyo wamesema walibaini mtoto kufanyiwa ukatili baada ya kumuona anashindwa kutembea na wakamhoji na kumpeleka polisi.
Dawati la jinsia jeshi la polisi wamelazimika kumpeleka mtoto huyo katika hospitali ya mkoa wamorogoro kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ambapo Daktari wa zamu Hilda lyimo baada ya kufanya uchunguzi amesema Mtoto huyo amefanyiwa ukatili wa kubakwa mara nyingi na kuandika tararifa itakayosaidia kutoa ushahidi Mahakamani.
Kwaupande wake kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro leonard Paul amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na vielelezo vimekamilika mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi na atafikishwa mahakamani huku akiwataka wazazi kuwakagua watoto mara kwa mara.



0 comments:
Post a Comment