![]() |
| Mwenyekiti wa chama cha wabunge wanawake ANNA ABDALLAH |
Wajumbe wa chama cha wabunge wanawake wameazimia kufikisha fursa zote zilizotolewa na katiba iliyopendekezwa kwa wananchi ili kuhakikisha wanaielewa katiba hiyo na kuipigia kura za ndio.
Akizungumza katika semina ya wanawake walioshiriki bunge maalum la katiba mjini DODOMA, Mwenyekiti wa chama cha wabunge wanawake ANNA ABDALLAH amewataka wanawake kugombea nafasi za uongozi huku akiwahamasisha wajumbe hao kuwaelimisha wanawake na jamii juu ya katiba iliyopendekezwa.
Watoa mada katika semina hiyo wamesema haki za wanawake zimeainishwa katika katiba iliyopendekezwa na kwamba hatua kubwa imefikiwa katika haki za binadamu.




0 comments:
Post a Comment