Sunday, 5 October 2014

Jamii ya Wafugaji yaiomba serikali kuwajengea Uwezo wa kuhimili Mifugo yao Ili kukabiliana na Hali ya Hewa.



Wafugaji  wa  wilaya  za  Longido  na  Monduli  Mkoani  Arusha  wameiomba  Serikali  na wadau  wengine kuwajengea uwezo  wa  Kufuga aina  za mifugo  wenye tija na wanaohimili ukame ikiwemo   Mbuzi, Kondoo na kuku  kama  hatua  ya kukabiliana  na Mabadiliko  ya  Hali ya  Hewa  ambayo  yanaendelea  kuwaathiri siku  hadi siku.
Wakizungumza  na  watendaji  wa  Mtandao  wa  vikundi  vya  wakulima  na  wafugaji  nchini  (mviwata) waliotembelea  Baadhi  ya  Vikundi  wananchi  hao wamesema pamoja  na misaada  wanayopata  wanaendelea  kukabiliwa  na umaskini  kutokana na athari za ukame  hivyo  wameshauri  kuwezeshwa kufuga mifugo inayohimili  hali  iliyopo.
Baadhi ya  wanawake walianza kufuga mbuzi ,na  kuku   wamesema  aina  hiyo  ya  Mifugo   inaweza  kuwapunguzia  makali  ya  maisha  kama  watasaidiwa  kuepukana  na  Magonjwa na hivyo kuwezeshwa  kufuga  kibiashara. 
Afisa  ugani   kutoka  Mtandao  wa  wakulima  (mviwata )  mkoa  wa  arusha Bi,Eunoti  Aberenego   Amesema  Baada  ya  kufanikiwa  kuwahamasisha  wafugaji   na  wakulima  kuunda  vikundi  sasa  wanaendelea   kuwaelimisha juu ya umuhimu wa  kulima  na  kufuga  kwa tija japo bado  kuna  changamoto  kubwa  ya   aina  za mbegu za  Mifugo na mazao ya chakula.
Baadhi ya  viongozi  akiwemo  Diwani  wa  kata  ya   namanga  Bw John Kimli   amesema   asilimia  kubwa  ya  Ng”ombe  wameshaanza  kuathirika  na ukame licha ya   kuwashukuru wadau wanaendelea  kuwasaidia  kwa  kuwapa  Mbegu  za Ng”ombe  wa  kisasa  zikiwemo zilizotolewa  na Mh.Rais ,ukame  umeziathri  kwa   kwa  Kiasi  kikubwa.

0 comments:

Post a Comment