![]() |
| Kamishana wa Madini na Petroli kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi HOSEA MBISE |
Kamishana wa Madini na Petroli kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi HOSEA MBISE amesema serikali itatoa zaidi ya shilingi Bilioni NNE kwa Kampuni 20 za kufua umeme zitakazokidhi viwango vya kutoa huduma ya umeme kwa wananchi waishio maeneo ya vijijini.
Kamishana huyo akizungumza Jijini ARUSHA mara baada ya kutembelea maonesho ya Kampuni 52 za kufua umeme ambayo yanashindanishwa ili kupata Kampuni 20 zitakazotoa huduma ya kufunga umeme katika maeneo muhimu ya kijamii ikiwemo zahanati, shule pamoja na mitambo ya kuvuta maji yaliyoandaliwa na Wakala wa Umeme Vijijini -REA.
Mmoja wa mawakala wanaotoa huduma ya umeme vijijini ALSI MBISE amesema wanatarajia kufunga umeme katika Kijiji cha KIBINDU kilichopo Wilaya ya BAGAMOYO Mkoani PWANI ambapo jumla ya Kaya 680 zinatarajia kunufaika na huduma hiyo.
Asilimia 50 ya wananchi watakuwa wamepata huduma yakufungiwa umeme katika maeneo ya vijijini ifikapo mwaka 2025.




0 comments:
Post a Comment