Sunday, 5 October 2014

Wananchi arumeru walalamikia Hujuma kwenye Miundombinu ya Maji.

Baadhi ya watumishi wa mamlaka ya maji ya Mji mdogo wa Usariver wilayani Arumeru wamelalamikiwa kushirikiana na Baadhi ya watu kuhujumu  miundombinu ya maji ili  waweze kujipatia  fedha  wakati  wanapohitajika  kutengeneza Miundombinu  hiyo.  

  Malalamiko  ya  hujuma hizo  ikiwemo  ya  kukata mabomba yametolewa na wananchi wa mji huo ambao wamesema hatua hiyo pamoja  na  kuwaongezea makali ya tatizo la maji inawasabibishia Hasara.
 
Akizungumzia  malalamiko hayo Meneja wa mamlaka hiyo  Bw, Daniel Ndeku amekiri kupokea malalamiko hayo na tayari ameshaanza  kuyafanyia  kazi  na ameongeza kuwa pia lipo tatizo la wakandarasi wanaopewa kazi ya ujenzi wa barabara kutojali   Miundombunu ya maji.
 
Baadhi ya watendaji  wa sekta ya barabara wamesema tatizo la ukataji wa mabomba ya maji wakati wa kukarabari Barabara  linatokana na utaratibu wa baadhi  ya wananchi wa kutofuata taratibu wakati wa kuunganishiwa huduma ya maji.

0 comments:

Post a Comment