Na, Seif Baruti.
Mkurugenzi wa chuo cha uandishi habari na utangazaji Arusha
Bw. Joseph Mayagila amefungua semina ya ujasiriamali hii leo itakayomalizika siku ya ijumaa chuoni hapo.
Bw. Joseph Mayagila aliesema kuwa semina hiyo ni muhimu sana
kwa wanafunzi wote kwa sababu dunia ya sasa imejengeka katika misingi ya
ujasiriamali na ili mtu yeyote afanikiwe kibiashara ni lazima ajue kupanda
mbegu, thamani ya muda pamoja na mavuno ambayo ni matokeo ya kupanda mbegu.
![]() |
| Mkurugenzi wa mafunzo katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji akifungua semina ya ujasiamali mapema leo: picha BENSON MREMI |
Semina hiyo iliyowahusisha wanafunzi wa kozi zote chuoni
hapo ikiwemo kozi ya Uandishi wa habari
na Utangazaji, Ualimu,Sekretari pamoja na kozi ya Kompyuta.
Katika semina hiyo ziliawasilishwa mada kuu tatu na
Wakufunzi wa Chuo hicho, ambapo mwalimu Onesmo Elia Mbise aliwasilisha mada ya
mikakati ya kibiashara, na mada ya huduma
kwa wateja iliwasilishwa na Bw, Christian Ndege nae Mratibu wa semina hiyo Bw.
Adrea Ngobole aliweza kuwasilisha mada ya misingi au mikakati ya mjasiriamali.
Mbise alisema mjasiriamali anatakiwa kuwa na mikakati
mahususi kuhusu biashara anayofanya kwa kuweza kujiuliza maswali ya msingi na
kujijibu katika biashara yake ili kuweza kutatua changamoto zitakazo mkabiri mfabiashara huyo.
Mfanyabiashara anatakiwa kuwa na wazo la kibiashara ambalo
familia yake imekubaliana nalo ili iweze kumsaidia pindi anapohitaji kutumia
baadhi ya rasilimali za familia kuwa
rahisi kwake kuzipata, pia anatakiwa kuwa ni mtu mzuri wa matuminzi ya muda na awe
tayari kufanya kazi kwa bidii zaidi ya yule aliyemwajiri, alisema Mbise
| Mkufunzi katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw. Onesmo Mbise akiwasilisha mada leo: picha BENSON MREMI |
Bw, Christiani Ndege
katika uwasilishaji wake wa mada ya pili alisema, mjasiriamali anatakiwa kuijua
vizuri biashara yake ili aweze kumbakiza mteja wake kwa kumtafutia mbadara ya bidhaa
aliyokuwa anaihitaji pindi anapoikosa katika biashara yake.
“Wafanyabiashara wengi huwapoteza wateja wao bila ya wao
kujijua, kwani mteja ni rahisi kumpata ila ni vigumu sana kumfanya adumu kuwa
mteja wako kama hautojua ninamna gani ya kuweza kumfanya awe wako”alisema Ndege
Mfanyabiashara anatakiwa kuwa na lugha nzuri kwa mteja wake
ili kumfanya ajisikie kuwa yeye ni wa dhamani kwake, pia wafanye wateja wako wafahamu mfumo unaotumia na kumsaidia mteja
kufaniksha huduma anayoitaka na uumpe mteja wako kitu cha ziada na alichokuwa
akikihitaji.
Nae, Bw. Adrea Ngobole alisema mjasiriamali anatakiwa kuwa
na wazo tajirishi na awe na jicho la kuona fursa ambazo zinapatikana mbele ya
jamii kwa kuweza kutoa majibu ya changamoto yanayopatikana katika jamii hiyo.
Pia Mjasiriamali anatakiwa
kuweka mipango endelevu ya kibiashara ili kuweza kumfikisha kuwa tajiri na kuwa
mvumilivu kwa matatizo yatakayo mkumba katika biashara yake, pia anatakiwa
kuwaepuka marafiki wanaoweza kumkatisha tamaa pindi anapohitaji ushauri,
alisema Ngobole.
| Mratibu wa semina ya ujasiriamali katika chuo cha uanndishi wa habari na utangazaji Arusha Bw. Andrea Ngobole akitoa mada mapemaa leo: picha BENSON MREMI |
Mmoja wa wanafunzi chuoni hapo,aliyejitambulisha kwa jina la
Ziara Nyatu alisema wamefurahi kupata mafunzo hayo kwani yatawawezesha
kujiajiri wenyewe pindi wamalizapo mafunzo ya uandishi na hata wakiwa chuoni
hapo, licha ya kusubiria kujiajiri ili kujikwamua katika dibwi la kukosa ajira
na ana tegemea makubwa katika siku mbili zilizo baki.
![]() |
| Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria semina ya ujasiriamali katika ukumbi wa chuo cha uandshi wa habari utangazaji Arusha leo: picha BENSON MREMI |





0 comments:
Post a Comment