GEORGE KAVISHE
WATANI wa Jadi SIMBA na YANGA zitakutana DESEMBA 13 nje ya mchezo wa ligi kuu soka TANZANIA BARA kucheza katika shindano la kuhitimisha ujumbe wa mdhamini wao kupitia shindano la NANI MTANI JEMBE linalowashirikisha mashabiki wa vilabu hivyo.
Meneja wa bia ya KILIMANJARO ambao ni wadhamini wa vilabu vya SIMBA na YANGA, GEORGE KAVISHE amesema shindano hilo limetenga kiasi cha shilingi milioni MIA MOJA ambapo wakati wa mchezo huo timu itakayoibuka mshindi itapata MILIONI 15 na aliyefungwa atapata milioni TANO
mashabiki wa vilabu hivyo wamekuwa wakipambana kwa kutuma ujumbe wa simu ambapo kiasi cha shilingi milioni THEMANINI zimetengwa , huku kila timu ikianza na shilingi MILIONI 40 kila moja.
Kutokana na kiasi hicho, fedha itakatwa katika kwa klabu husika na kwenda kwa klabu pinzan




0 comments:
Post a Comment