![]() |
| Rais JAKAYA KIKWETE |
Rais JAKAYA KIKWETE amewahakikishia wakazi wa mikoa ya kanda ya kati na mikoa ya jirani kuwa hivi karibuni watapata huduma ya uhakika ya uchunguzi wa afya zao bila kwenda hospitali za rufaa au nchi za nje.
Akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa kituo cha uchunguzi wa magonjwa ya binadamu kinachojengwa katika chuo kikuu cha Dodoma Dkt. KIKWETE amesema kituo hicho kitakuwa na vifaa vya kisasa na madaktari bingwa wa magonjwa ya binadamu.
Naye makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dodoma-UDOM profesa IDRISS KIKULA amesema baadhi ya changamoto zimekuwa ni kikwazo kikubwa katika kukamilisha ujenzi wa kituo cha uchunguzi wa magonjwa ya binadamu.
Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi DKT SHUKURU KAWAMBWA amesema serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kuvutia kwa wanafunzi wa masomo ya sayansi.




0 comments:
Post a Comment