Wednesday, 1 October 2014

Mradi wa umeme wazinduliwa mkoani RUVUMA

Add captionNaibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi JENISTA MHAGAMA

















Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi JENISTA MHAGAMA amezindua mradi wa umeme katika eneo la LILONDO mkoani RUVUMA. 

Mradi huo wa umeme utakaonufaisha maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na WINO, MADABA na LILONDO umegharimu takribani Shilingi Milioni Mia Moja na Themanini . 

Naibu waziri MHAGAMA amechangia shilingi milioni 100 katika mradi huo ambapo baada ya kuzindua mradi huu wa umeme, amekagua maendeleo ya kufyatua matofali kwa nguvu za wananchi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya muuguzi ya zahanati ya LILONDO, bwalo la chakula na nyumba za walimu katika shule ya msingi LILONDO na kuchangia mabati 440 na mifuko 60 ya saruji kusaidia nguvu katika ujenzi huo 

JENISTA pia ameshiriki katika mahafali ya sita ya kidato cha nne katika shule ya sekondari WINO na kueleza kuwa serikali imejipanga kuinua elimu kwa kuboresha miundo mbinu ya sekta ya elimu. 

0 comments:

Post a Comment