KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, TAIFA STARS, MART NOOIJ, ametangaza kikosi cha wachezaji 26 kwa ajili mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Benin itakayochezwa Oktoba 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kocha Nooij ambaye yuko Cairo, Misri kwenye kongamano la makocha la Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), amesema kikosi cha STARS kitaingia kambini Oktoba 6 jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo huo.
Iwapo STARS itaifunga BENIN katika mchezo huo itapanda katika viwango vya FIFA vitakavyo tangazwa mwezi OCTOBA mwaka huu.



0 comments:
Post a Comment