Saturday, 4 October 2014

Wadau sekta ya anga wapitisha azimio kuboresha huduma


Wadau wa sekta ya safari za anga kutoka umoja wa vyuo vya usafiri wa anga barani Afrika wamepitisha azimio la kuboreshwa kwa viwango vya huduma katika sekta ya safari za anga barani Afrika. 
Wakizungumza katika mkutano wa kwanza wa vyuo vya usafiri wa anga barani Afrika uliomalizika leo mjini Unguja, wadau hao wamesema huduma hizo zinapaswa kuboreshwa ili kukidhi mahitaji ya soko la safari za anga kimataifa. 
Aidha wamependekeza kuundwa kwa umoja utakaoweza kusaidia kufuatilia mitaala ya utoaji wa taalum ya usafiri wa anga ambayo italiwezesha bara la Afrika kuhimili ushindani katika soko la kimataifa la safari za an
ga.

0 comments:

Post a Comment