Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema kimelituhumu Jeshi la polisi nchini kikidai kuwa jeshi hilo linafanya kazi ya siasa kukisaidia chama tawala na kukandamiza vyama vya upinzani hali inayodaiwa kudidimiza Demokrasia na kuondoa ushindani halali wa kisiasa.
Malalamiko hayo yametolewa na viongozi mbalimbali wa chama cha Chadema akiwemo mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho na mbunge wa iringa mjini mchungaji peter msigwa na makamu wa mwenyekiti wa baraza la vijana la chama hicho (bavicha) Patrick Sosopi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya kihesa.
Malamiko hayo yametokana na jeshi la polisi mkoani iringa kuzuia maandamano ya wafuasi wa chama hicho waliotaka kumpokea makamu mwenyekiti huyo wa Baraza la vijana Bavicha.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chadema wilaya ya iringa Frank Nyalusi amewataka wananchi wakazi wa iringa mjini kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la makazi litakalotumika na mamlaka ya vitambulisho vya taifa nida kwaajili ya uhakiki wa wakazi hao wakati watakapojiandikisha kwaajili ya vitambulisho vya utaifa zoezi alilodai kuwa limeanza kuhujumiwa na baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi.



0 comments:
Post a Comment