This is default featured post 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Wednesday, 8 October 2014

kenyatta ana kwa ana na ICC


Rais Uhuru Kenyatta ICC
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amefika mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC huko Hague, ambako anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu.
Yeye ni kiongozi wa kwanza wa taifa kuwasili mbele ya mahakama hiyo.
Kenyatta amefika mbele ya mahakama hiyo baada ya waendesha mashtaka kuishutumu serikali ya Kenya kukata kuwasilisha ushahidi muhimu.
Kenyatta amekanusha madai ya kupanga na kufadhili ghasia za kikabila nchini Kenya baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata mwaka 2007/2008.
Kikao cha leo kitatathmini ombi la upande wa mashitaka la kutaka kuahirishwa kwa kesi hiyo hadi pale serikali ya Kenya itakapoikabidhi mahakama hiyo ushahidi unaohitajika kuhusiana na mali ya Rais Kenyatta.
Upande wa utetezi nao unataka kesi hiyo ifutiliwe mbali ukisema kuwa upande wa mashitaka hauna ushahidi wa kutosha kwa kesi hiyo kuendelea.
Kiongozi wa mashitaka Fatou Bensouda, amewasili mahakamani akisema kesi hiyo iko katika awamu muhimu sana.
Kenyatta ameamua kukaa kimya akimtaka wakili wake kuongea kwa niaba yake.

Sunday, 5 October 2014

Ngome nyengine ya Al-Shabaab yaanguka

Mwanajeshi wa AU akiweka doria 


 Mji wa bandari wa Barawe nchini Somalia ambao ulikuwa umetajwa kuwa ngome ya mwisho ya kundi la Al shabaab umethibitiwa na vikosi vya serikali vikisaidiwa na wanajeshi wa muungano wa Afrika.
Mji wa Barawe ulio umbali wa kilomita 200 Kusini Mashariki mwa mji mkuu wa Mogadishu umekuwa chini ya udhibiti wa wanagambo wa Al Shabaab kwa miaka sita.
Muungano wa Afrika unasema kuwa wanamgambo wamekuwa wakiutumia mji huo kama kituo cha kupanga mashambulizi dhidi ya mji mkuu Mogadishu.
Wapiganaji wa Al-Shabaab walianza kuondoka katika mji huo siku chache zilizopita.

Wenger:Costa ni moto wa kuotea mbali


















 Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa Diego Costa ni mshambuliaji hatari na kwamba mshambuliaji huyo wa Chelsea ni tishio kubwa kwa kikosi chake katika mechi ya Leo itakayochezwa katika uga wa stamford Bridge.
Kilabu zote mbili hazijafungwa tangu msimu huu wa ligi uanze,lakini Chelsea iko juu ya Arsenal kwa pointi sita.
Costa aliyenunuliwa kwa kitita cha pauni millioni 32 kutoka kilabu ya Uhispania ya Atletico Madrid,amefunga mabao 8 katika mechi 6 za ligi ya Uingereza alizoshiriki.


 


 ''Costa ana kila kitu cha mshambuliaji,anajitolea na yuko tayari kufunga bao'',alisema Wenger.
Wenger anahisi matumaini kwamba huenda Arsenal ikaishangaza Chelsea ilio katika kilele cha jedwali la ligi ya Uingereza ikiwa na pointi 16 kati ya 18.
Msimu uliopita Arsenal ilipata kichapo cha mabao 6 kwa 0 katika mechi iliochezwa katika uga wa Stanford Bridge huku Wenger akiweka rekodi ya kuisimamia kilabu hiyo kwa mechi yake ya1000.
Kwa upande wake Mourinho anatarajia ushindani mkali kutoka kwa Arsenal na amejitayarisha vilivyo.


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































Mwigulu afunguka urais 2015


Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba









 Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema ameanza kuchangiwa fedha na Watanzania wanaoishi ughaibuni ili zimsaidie iwapo ataamua kuwania urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani.
Akizungumza katika mahojiano maalumu bungeni jana, Mwigulu alisema amesikia makundi mbalimbali, wakulima, wafugaji na wanafunzi wa elimu ya juu, walitoa tamko lao juu ya kumtaka kugombea nafasi ya urais.
“Wakulima na wafugaji walisema kuwa nikigombea watachangishana fedha za kampeni kwa kutambua mimi ni mtoto wa maskini na mimi ni maskini,”alisema na kuongeza;
“Wanafunzi wa elimu ya juu walisema kuwa wao watatembea kwa miguu kuhakikisha kuwa kura zinatosha. Kuzungusha fomu niende tu siko pekee yangu.”
Alisema na walimu pia baada ya kupata mishahara kwa wakati sasa wamemwomba kugombea nafasi hiyo ya juu kitaifa.
“Watanzania walioko nje ya nchi walisema wanachangishana na kimsingi wameshaanza kuchangishana ili kuhakikisha kwamba nagombea,” alisema na kuongeza,
“Mimi naendelea kusema ni vizuri watu kukutathmini kwa sababu jambo la urais si kujaza nafasi ni kazi watu wanakutuma uwafanyie na wewe uwajibike kwao na wala si jambo la kutaka tu.”
Alisema wanakutuma kuifanya kazi hiyo baada ya kupima changamoto walizonazo na kuona nani anaweza kufaa katika kuzitatua changamoto hizo.
“Sauti ikiwa kubwa hivyo ni jambo jema ambalo wanaona kuwa unaweza kufanya kazi hiyo vizuri. Naheshimu sana mawazo yao, lakini kwa sasa nataka niweke nguvu katika usimamiaji wa bajeti ya serikali, sera na miradi ya serikali,”alisema na kuongeza:
“Na naweka mkazo kwenye majukumu haya niliyopewa ya sasa. Na mimi huwa ni kawaida yangu jukumu lolote ninalopewa najitahidi kufanya kwa nguvu zote, kwa moyo wote ili Watanzania waweze kunufaika.”
Mwigulu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, alisema muda ukifika ataongea kuhusu kama anagombea urais ama la.
“Mimi niko pia katika chama kwa hiyo naheshimu miiko ya chama, taratibu za chama kwa hiyo chama kitakaporuhusu watu waanze harakati hizo ndiyo tutasema,”alisema

Jeshi la Polisi limetumia maji ya kuwasha kuwatawanya wanawake wafuasi wa Chadema waliokuwa wakijiandaa kuandamana hadi ikulu jijin Dar es Salaam.

Jeshi la polisi limetumia maji ya washawasha kutawanya maandamano ya wanawake wa chadema waliokuwa wakiandamana kutokea kinondoni kuelekea ikulu jijini Dar es salaam kwa lengo la kumshinikiza Rais jakaya kikwete kutosaini Rasimu ya tatu ya katiba iliyopendekezwa Bungeni mjini Dodoma hivi karibuni.

ITV ilitia timu katika mtaa wa togo Kinondoni jijini Dar es salaam na kushuhudia baadhi ya wafuasi wa Chadema kutoka Baraza la wanawake wakiwa katika ofisi tayari kujiandaa na maandamano hayo ambapo Mwenyekiti wa Bawacha taifa halima mdee akizungumza na vyombo vya habari akasema maandamano ni haki,na katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania inaruhusu watu kuandamana.
 
Licha ya askari kuonekana kujipanga katika maeneo hayo ya kinondoni kudhibiti maandamano hayo lakini wanawake hao wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wa Bawacha halima mdee walianza Maandamano.

Katika kudhibiti maandamano hayo jeshi la polisi walitumia maji ya washawasha kutawanya wafuasi hao wa Chadema na kujikuta wakikimbilia katika Baadhi ya vibanda vya eneo hilo.
 
Ghafla ITV ilishuhudia mwenyekiti wa Bawacha taifa Halima Mdee akishikiliwa ndani ya moja ya kibanda alichokimbilia huku katibu wake wa jimbo la kawe naye akitiwa mbaroni.
 
Baada ya baadhi ya waandamaji hao kushikiliwa,ITV ilizunguka katika maeneo mbalimbali ikiwemo Fire,Mnazi mmoja,Pam Beach,upanga na kukuta maeneo yote hayo yakiwa hayana waandamaji,ambapo katika kituo cha polisi ostebay hali ilikuwa tofauti baada ya watu wakiwemo waandishi wa habari kuzuiliwa kuingia katika kituo hicho huku Magari yanayofika kituoni hapo nayo yakizuiliwa na askari polisi ambapo baada ya kufika baadhi ya wafuasi wa Chadema mzozo ukatokea.
 
Licha ya ITV kuweka kambi katika kituo hicho kwa zaidi ya saa 7 lakini mpaka inatoka katika eneo hilo bado viongozi wa chadema ngazi ya juu walikuwa hawajaonekana katika kituo hicho licha ya katibu mkuu wa chadema Mh Wilbrod Silaa kuzungumza na ITV kwa njia ya simu na kusema kuwa tayari wanasheria wa chama chao watakuja kushughulikia sakata hilo.

Wazee waiomba Serikali kuwachukulia hatua watu wanao wanyanyasa katika kupata huduma za kijamii,Mkoani kagera.

Wazee mkoani kagera wameiomba Serikali kuwachukulia hatua watu wote wanao wanyanyasa katika huduma mbalimbali za kijamii na wale wanao jihusisha na  ukatili wakuwauwa vikongwe. 

Wakiongea katika Maadhimisho ya siku ya wazee Duniani wazee hao wamesema wamekuwa wakinyanyasika katika mambo mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya nakwamba Serikali inatakiwa kuchukua hatua Madhubuti za kuwawajibisha watu wote wanaojihusha na vitendo vya ukatili kwa  wazee ambao  wameshiriki katika kulinda amani na utulivu ulioko hapa Nchini ambapo wameongeza kuwa wazee wanatakiwa kulindwa na kuheshimiwa.
 
Katika taarifa yake kwa Mgeni Rasimi mzee Yolonimo Ijugo amesema wazee wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali ikiwemo kukubwa na magonjwa na kwamba Serikali inatakiwa kuangali upya suala la afya kwa wazee, nahivyo kuongeza kuongeza kuwa serikali inatakiwa kuimarisha ulinzi kwa wazee kwakua wamekuwa wakituhumiwa katika kesi mbalimbali ambazo maranyingi zimekuwa zikisababisha vifo visivyokuwa vya lazima kwa wazee.
 
Kwa upande wake Mgeni Rasimi katika hafla hiyo Nashoni Kabaye  amesema serikali  imejipanga vyema katika kuhakikisha kuwa inawasaidia wazee kuwasaidia katika kutoa huduma mbalimbali muhimu ambazo zinaweza kuwasaidia wazee wote hapa Nchini huku mratibu wa maadhimisho hiyo Lydia Lugazia amesema katika shirika lao wamekuwa na Changamoto mbalimbali katika kuwahudumia wazee nakwamba Shirikala lao linahudumia zazidi ya wazee elfu moja wanao hitaji kupata pesheni.

Jamii ya Wafugaji yaiomba serikali kuwajengea Uwezo wa kuhimili Mifugo yao Ili kukabiliana na Hali ya Hewa.



Wafugaji  wa  wilaya  za  Longido  na  Monduli  Mkoani  Arusha  wameiomba  Serikali  na wadau  wengine kuwajengea uwezo  wa  Kufuga aina  za mifugo  wenye tija na wanaohimili ukame ikiwemo   Mbuzi, Kondoo na kuku  kama  hatua  ya kukabiliana  na Mabadiliko  ya  Hali ya  Hewa  ambayo  yanaendelea  kuwaathiri siku  hadi siku.
Wakizungumza  na  watendaji  wa  Mtandao  wa  vikundi  vya  wakulima  na  wafugaji  nchini  (mviwata) waliotembelea  Baadhi  ya  Vikundi  wananchi  hao wamesema pamoja  na misaada  wanayopata  wanaendelea  kukabiliwa  na umaskini  kutokana na athari za ukame  hivyo  wameshauri  kuwezeshwa kufuga mifugo inayohimili  hali  iliyopo.
Baadhi ya  wanawake walianza kufuga mbuzi ,na  kuku   wamesema  aina  hiyo  ya  Mifugo   inaweza  kuwapunguzia  makali  ya  maisha  kama  watasaidiwa  kuepukana  na  Magonjwa na hivyo kuwezeshwa  kufuga  kibiashara. 
Afisa  ugani   kutoka  Mtandao  wa  wakulima  (mviwata )  mkoa  wa  arusha Bi,Eunoti  Aberenego   Amesema  Baada  ya  kufanikiwa  kuwahamasisha  wafugaji   na  wakulima  kuunda  vikundi  sasa  wanaendelea   kuwaelimisha juu ya umuhimu wa  kulima  na  kufuga  kwa tija japo bado  kuna  changamoto  kubwa  ya   aina  za mbegu za  Mifugo na mazao ya chakula.
Baadhi ya  viongozi  akiwemo  Diwani  wa  kata  ya   namanga  Bw John Kimli   amesema   asilimia  kubwa  ya  Ng”ombe  wameshaanza  kuathirika  na ukame licha ya   kuwashukuru wadau wanaendelea  kuwasaidia  kwa  kuwapa  Mbegu  za Ng”ombe  wa  kisasa  zikiwemo zilizotolewa  na Mh.Rais ,ukame  umeziathri  kwa   kwa  Kiasi  kikubwa.

Chadema Chalituhumu Jeshi La polisi Nchini Chadai Jeshi hilo linafanya Kazi ya Siasa.

Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema kimelituhumu Jeshi la polisi nchini kikidai kuwa jeshi hilo linafanya kazi ya siasa kukisaidia chama tawala na kukandamiza vyama vya upinzani hali inayodaiwa kudidimiza Demokrasia na kuondoa ushindani halali wa kisiasa.

Malalamiko hayo yametolewa na viongozi mbalimbali wa chama cha Chadema akiwemo mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho na mbunge wa iringa mjini mchungaji peter msigwa na makamu wa mwenyekiti wa baraza la vijana la chama hicho (bavicha) Patrick Sosopi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya kihesa.
 
Malamiko hayo yametokana na jeshi la polisi mkoani iringa kuzuia maandamano ya wafuasi wa chama hicho waliotaka kumpokea makamu mwenyekiti huyo wa Baraza la vijana Bavicha.
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chadema wilaya ya iringa Frank Nyalusi amewataka wananchi wakazi wa iringa mjini kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la makazi litakalotumika na mamlaka ya vitambulisho vya taifa nida kwaajili ya uhakiki wa wakazi hao wakati watakapojiandikisha kwaajili ya vitambulisho vya utaifa zoezi alilodai kuwa limeanza kuhujumiwa na baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi.

Wananchi arumeru walalamikia Hujuma kwenye Miundombinu ya Maji.

Baadhi ya watumishi wa mamlaka ya maji ya Mji mdogo wa Usariver wilayani Arumeru wamelalamikiwa kushirikiana na Baadhi ya watu kuhujumu  miundombinu ya maji ili  waweze kujipatia  fedha  wakati  wanapohitajika  kutengeneza Miundombinu  hiyo.  

  Malalamiko  ya  hujuma hizo  ikiwemo  ya  kukata mabomba yametolewa na wananchi wa mji huo ambao wamesema hatua hiyo pamoja  na  kuwaongezea makali ya tatizo la maji inawasabibishia Hasara.
 
Akizungumzia  malalamiko hayo Meneja wa mamlaka hiyo  Bw, Daniel Ndeku amekiri kupokea malalamiko hayo na tayari ameshaanza  kuyafanyia  kazi  na ameongeza kuwa pia lipo tatizo la wakandarasi wanaopewa kazi ya ujenzi wa barabara kutojali   Miundombunu ya maji.
 
Baadhi ya watendaji  wa sekta ya barabara wamesema tatizo la ukataji wa mabomba ya maji wakati wa kukarabari Barabara  linatokana na utaratibu wa baadhi  ya wananchi wa kutofuata taratibu wakati wa kuunganishiwa huduma ya maji.

Mwanaume mkazi wa Nane nane Morogoro mwenye Umri wa Miaka 53 ambaka Mtoto wa Miaka 7 nakumsababishia Maumivu.

Mtoto mwenye umri wa miaka (7) Mkazi wa nane nane mjini Morogoro amebakwa   na mtu mzima mwenye umri wa miaka (53) na kumsababishia maumivu makali na kulazimika kupelekwa hospitali ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu 
 .
Akizungumza kwa uchungu  mtoto huyo  akiwa katika kituo cha polisi mkoani Morogoro   amemtaja aliembaka kuwa ni Joseph Paula(53)  ambaye ni ndugu wa Baba yake mzazi  ambapo amesema mtuhumiwa alitumia mbinu ya kumtuma Dawa  chumbani ndipo akambaka ambapo wazazi wa mtoto huyo wamesema walibaini mtoto kufanyiwa ukatili baada ya kumuona anashindwa kutembea na wakamhoji na kumpeleka polisi.
 
Dawati la jinsia jeshi la polisi wamelazimika  kumpeleka mtoto huyo katika hospitali ya mkoa wamorogoro kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ambapo Daktari wa zamu Hilda lyimo baada ya kufanya uchunguzi amesema Mtoto huyo amefanyiwa ukatili wa kubakwa  mara nyingi na kuandika tararifa itakayosaidia kutoa ushahidi Mahakamani.
 
Kwaupande wake kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro leonard Paul amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na vielelezo vimekamilika mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi na atafikishwa mahakamani huku akiwataka wazazi kuwakagua watoto mara kwa mara.

Man City yaichapa Aston Villa nyumbani kwao bao 2-0


Aston Villa: Guzan 8, Hutton 5, Senderos 6.5, Baker 7, Cissokho 6.5, Cleverley 5.5, Westwood 5, Delph 7, Richardson 7 (Grealish 71), Weimann 6 (Benteke 61, 6.5), N'Zogbia 6.5 (Bacuna 71)

Subs (not used): Clark, Bent, Sanchez, Given
Bookings: NONE
Goals: NONE

Man City: Hart 6, Zabaleta 6.5, Kompany 6.5, Mangala 7, Kolarov 7, Milner 6.5, Fernandinho 5.5 (Lampard 56, 6.5), Toure 7, Silva 7 (Navas 84), Dzeko 6 (Fernando 64, 6), Aguero 7.5

Subs (not used): Sagna, Caballero, Demichelis, Jovetic
Bookings: Kolarov
Goals: Toure (82), Aguero (88)
Referee: Chris Foy (Merseyside)

Ratings by Jack GaughaN

-

Saturday, 4 October 2014

SIMBA YABANWA MBAVU TAIFA

FULL TIME: Dk 90+4
Dk 90, Simba inapata kona tatu mfululizo, lakini hakuna lolote.

Dk83, Maguli tena anashindwa kufunga baada ya kupiga kichwa, mpira unapaa puuu.


Dk 77 Saidi Mohamed anapigwa shuti, linaokolewa na kuwa kona.

Dk 72, Maguli anapiga shuti kali lakini linadakwa kiufundi.
Dk 65, Okwi anapiga mpira unagonga mwamba na kutoka nje.


Dk 62, Mobi anapiga shuti lakini linatoka juu kidogo juu ya lango la Simba.


Dk 61, Ndemla anapiga shuti kali lakini linaguswa na kupaa nje( anagusa mchezaji mwenzake)


Dk 59, Okwi tena anashindwa kufunga baada ya mpira mzuri wa kona kumkuta akiwa pekee...Stand wanaonekana kujilinda zaidi.


Dk 58, Tambwe anapiga kichwa safi kabisa lakini kipa wa Stand anaugusa na unagonga mwamba na kurudi uwanjani.

Dk 56, Simba ndiyo wanashambulia zaidi, nafasi nyingine anapoteza Okwi.
Dk 54, Ndemla anashindwa kufunga yeye akiwa na kipa tu, lakini akashindwa kufunga.

Dk 52 Miraji anafanya kazi ya ziada kuutoa mpira nje na kuwa kona, shambulizi halina madhara.
Dk 46, Simba wafanya sahambulizi na shuti alilopiga Okwi linaokolewa na kuwa kona isiyo na msaada.

MAPUMZIKO:

KIPINDI CHA KWANZA KIMEMALIZIKA KWA SARE YA BAO 1-1 HUKU SIMBA IKITANGULIA KUFUNGA BAO KUPITIA SHABANI KISIGA NA BAADAYE STAND KUSAWAZISHA MWISHONI.

Sikukuu ya EID EL HAJI: Bei ya mbuzi na kondoo jijini DSM imepanda maradufu

Bei ya mbuzi na kondoo jijini DSM imepanda maradufu kutokana na mahitaji makubwa ya wanyama hao kwa ajili ya sikukuu ya EID EL-HAJI itakayofanyika siku ya jumapili 05/10/2014 ambapo muumini wa dini ya kiislamu anatakiwa kuchinja mnyama 
Katika soko la mbuzi la Vingunguti , bei imepanda kutoka shilingi elfu sitini kwa mbuzi au kondoo mmoja hadi shilingi laki moja na ishirini ambapo baadhi ya wachuuzi wa soko hilo wamesema mauzo yameongezeka kutokana na mahitaji makubwa ya wanyama hao. 
Hata hivyo wateja wa soko hilo wamesema bei hiyo ni kubwa kupita kiasi jambo ambalo linaweza kusababisha baadhi ya waislamu kushindwa kutimiza ibada muhimu ya kuchinja 

SERENA WILLIAMS ajitoa katika mashindano ya wazi ya CHINA kutoka na kuumia goti la kushoto

SERENA WILLIAMS


Mchezaji namba moja kwa ubora DUNIANI katika mchezo wa tenesi SERENA WILLIAMS amejitoa katika mashindano ya wazi ya CHINA kutoka na kuumia goti la kushoto katika mguu wake. 

Hii ni mara ya pili kwa mchezaji huyo kujitoa katika mashindano nchini CHINA baada kujitoa katika mashindano ya WUHAN kutoka na kuumwa wiki iliyopita. 
Mpinzani wake katika hatua ya mtoani Sam Stosur, ambaye ni bingwa wa mashindano ya wazi ya US mwaka 2011 anatinga moja kwa moja hatua ya robo fainali. 
Pia dada yake mchezaji VENUS amejitoa katika mashindano hayo kutokana na kuugua

TFF YAANZA KUSHUHULIKIA MALALAMIKO YATIKETI ZA KIELEKTRONIKI




Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwesigwa Celestine , amesema kuwa malalamiko juu ya changamoto za mfumo mpya wa matumizi ya tiketi za kielektroniki yamefika mezani kwake na akasisitiza kuwa tayari wameanza kulifanyia kazi suala hilo.


Kumekuwa na malalamiko ya mfumo huo wa tiketi ikiwemo kulanguliwa, pia kuwepo na mashine chache za kutolea huduma hiyo uwanjani jambo linalofanya baadhi ya mashabiki kutoingia uwanjani kwa muda muafaka kuzisapoti timu zao.

Mwesigwa amesema malalamiko juu ya mfumo huo wameyapata na wameyafikisha sehemu husika ambapo ni CRDB ili kuweza kuyatafutia ufumbuzi na kusisitiza kuwa tatizo hilo litamalizika katika michezo michache ya hivi karibuni.

“Hili tatizo nikiri tu lipo maana malalamiko yapo mengi na yametufikia walengwa, tulichokifanya ni kuwasiliana na watoa huduma (CRDB) na kuwafikishia ambapo wametuhakikishia watalipatia ufumbuzi ndani ya muda mchache tu, hivyo tunaomba tu mashabiki wawe na subira maana teknolojia hii ni mpya hapa kwetu.


“Jambo jema ni kwamba CRDB wameonyesha ushirikiano mkubwa katika hilo na kuahidi ‘kuimprove’ huduma yao ili wadau wa soka waendelee kuona burudani na kuzisapoti timu zao bila tatizo,” alifafanua Mwesigwa.

Shughuli za binadamu lazima zizingatie kuendeleza uhai

Uharibifu wa mazingira 

                                                                                                               
Taasisi ya Raslimali za Afrika ya Chuo Kikuu cha Umoja wa Mataifa (UNU-INRA) yenye makao makuu nchini Ghana, wiki iliyopita, iliendesha mafunzo maalumu mjini Lusaka, Zambia, yaliyolenga kuelezea hatari kwa viumbe hai duniani.
Lengo la mafunzo lilikuwa ni kuwajengea uwezo watafiti, wafanyabiashara, wanamazingira na wachumi ili watambue mambo ya hatari kwa uhai yanayoweza kujitokeza katika shughuli zao za kila siku na jinsi ya kuyakabili.
Waliendesha mafunzo hayo chini ya kaulimbiu Weka Mazingira Mazuri ya Shughuli za Makundi ya Kijamii ili Kuimarisha na Kuendeleza Mahitaji kwa Uhai.”
Hii ni kaulimbiu ambayo inahamasisha shughuli mbalimbali ili ziendane na mipango ya mapinduzi ya kijani barani Afrika.
Haya ni mapinduzi yanayolenga kuimarisha kilimo kupambana na njaa na wakati huohuo kuhifadhi mazingira kwa lengo la kukabili matatizo yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi.
Mchumi na mtafiti wa UNU-INRA, Dk Calvin Atewamba anasema binadamu ana kila sababu ya kujutia kwa kuharibu mazingira wakati akiendesha shughuli mbalimbali ili kupata chakula na kufanya biashara.
Alisisitiza kuwa “shughuli zote za kijamii hapa duniani zina matokeo chanya au hasi kwa mazingira. Kinachotakiwa kifanyike ni jamii kuelimishwa ili kutekeleza malengo ya Afrika katika kufikia mapinduzi ya kijani katika uchumi”.
Alitoa mfano wa shughuli zinazochangia athari za mazingira kama vile uvunaji kupita kiasi wa raslimali za bahari, uchafuzi wa mazingira na kuongeza athari za mabadiliko ya tabianchi.
Dk Atewamba anasema jamii kwa sasa inahitaji kuwekewa mfumo ambao utasimamia na kutathmini shughuli mbalimbali ili kuelekeza nini kifanyike kwa lengo la kupunguza athari za mazingira zinazosababishwa na shughuli za binadamu.
Kufanya hivyo, Dk Atewamba anaamini, kutainua hadhi ya binadamu kwa kuboresha mazingira yanayoendeleza uhai.
Mkurugenzi wa UNU-INRA, Dk Elias Ayuk anaamini kuwa ipo haja ya kuweka kiunganishi kati watafiti wa mazingira na jamii kwa kuwa shughuli za kila siku za binadamu ndizo zinachangia athari za mazingira.
Nchi zilizokuwa na uwakilishi kwenye mafunzo haya ni Ghana, Cameroon, Nigeria, Kenya, Zimbabwe, Misri, Uganda, Malawi, Benin, Swaziland, Tunisia na Zambia

Pato la taifa laongezeka

 Mkurugenzi wa takwimu za uchumi wa ofisi ya taifa ya Takwimu Morrice Oyuke

Pato la taifa limeongezeka kutokana na ukuaji wa shughuli mbalimbali za kiuchumi nchini. 

Kwa mujibu wa ofisi ya Taifa ya Takwimu, thamani ya pato la taifa kwa robo ya pili ya mwaka huu wa 2014 imeongezeka na kufikia shilingi tirioni 5.40 kutoka shilingi tirioni 5.05 katika kipindi kama hicho mwaka jana wa 2013. 

Akielezea ukuaji wa pato la Taifa jijini DSM Mkurugenzi wa takwimu za uchumi wa ofisi ya taifa ya Takwimu Morrice Oyuke amesema katika kipindi hicho kasi ya ukuaji wa pato la taifa iliongezeka kwa asilimia 6.9 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 7.6 katika kipindi kama hicho mwaka jana. 

Amesema shughuli za mawasiliano, biashara za rejareja na jumla ziliongoza kwa kuwa na kasi kubwa ya ukuaji na shughuli za misitu na uwindaji ziliongoza kwa kuwa na kasi ndogo ya ukuaji katika kipindi hicho