KOCHA Arsene Wenger amewalaumu wachezaji wake wa Arsenal kwa
kushindwa kucheza vizuri wakichapwa mabao 2-0 na Dortmund jana, huku
akirejea na kiungo Jack Wilshere akiwa majeruhi baada ya kuumia kwenye
mchezo huo.
Wilshere
alitonesha enka yake ya mguu wa kulia kikosi cha Wenger kikilala 2-0
katika mchezo wa kwanza wa makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Wlishere
ameumia sehemu lie lie ambayo ilimfanya akawa nje ya Uwanja kwa miezi
17. "Ni vigumu kusema ni mbaya kiasi gani,"amesema kocha wa Arsenal.
"Kwa kawaida haitakuwa mbaya sana, lakini nina wasiwasi mno kulingana na
historia yake,".





0 comments:
Post a Comment