Tuesday, 16 September 2014

ADEBAYOR KUWA NAHODHA MSAIDIZI HOTSPUR

NYOTA wa Togo, Emmanuel Adebayor ameteuliwa kuwa Nahodha Msaidizi wa Tottenham Hotspur, chini ya Mfaransa Younes Kaboul.
Mfaransa huyo ameiongoza Spurs mara kadhaa msimu huu kama nahodha wa mechi na sasa kocha Mauricio Pochettino amempa moja kwa moja beji hiyo akirithi mikoba ya beki Michael Dawson, aliyehamia Hull City mwezi uliopita.
Adebayor atakuwa Nahodha Msaidizi pamoja na kipa Hugo Lloris.

Saluti kwa Nahodha; Emmanuel Adebayor amereuliwa kuwa Nahodha Msaidizi Spurs chini ya  Younes Kaboul 

0 comments:

Post a Comment