Wednesday, 10 September 2014

KOCHA OMOG WA AZAM WALA HAUMIZWI KICHWA NA YANGA


Kocha wa kikosi cha mabingwa msimu uliopita, Azam, Mcameroon, Joseph Omog, ameibuka na jipya baada ya kuitupia kijembe mechi yao ya Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga kwa kuilinganisha na mechi ya bonanza huku akisema kuwa hawezi kuumiza kichwa kuiwaza kwani wana mambo mengi ya msingi ya kufikiria na si mechi hiyo.

Azam walitwa ubingwa huo kwa Yanga ambayo ilikuwa ikiwanyatia kwa karibu,lakini tayari Yanga wameweka mikakati kabambe kwa ajili ya mchezo huo

Lakini Omog amesema kwake ni bonanza badala yake anatoa programu kwa ajili ya ligi kuu na mechi za kimataifa tu.
“Siwezi kulala niwaze mchezo wetu na Yanga, nauona kama mchezo wa bonanza, siwezi kuumiza akili katu. Sawa, unatoa changamoto katika kujiandaa na ligi kuu, lakini siyo suala la kujipa presha kwa mchezo wa namna hiyo.

“Naandaa kikosi kwa ajili ya kutetea ubingwa pamoja na mipango ya kukifikisha mbali kikosi chetu katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika mwakani,” alisema Omog.

0 comments:

Post a Comment