This is default featured post 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Monday, 29 September 2014

ALONSO AWANYAZISHA WATU BUNDESLIGA, APIGA PASI 175 MECHI MOJA



Wakati Xabi Alonso alipotua Bayern Munich, wengi walilalamika kwamba hakukuwa na haja ya timu hiyo kumchukua mkongwe huyo kuziba pendo la Toni Kroos aliyekwenda Real Madrid.

Badala yake wakasisitiza wangeweza kuwapa nafasi vijana.
Lakini kadiri siku zinavyosonga mbele, Xabi Alonso amezidi kutoa somo kwa kufanikiwa kuwa mchezaji bora wa mechi mara mbili katika mechi tano.
Kama hiyo haitoshi, Alonso amefanikiwa kugusa mpira mara 679, huku akipiga pasi 558 zilizofika ukiwa ni wastani wa  89% ambao ni wa juu kabisa.

Katika mechi wakati Bayern ilipoivaa Cologne jana, Alonso alipiga pasi 175, si mchezo.

LIGI YA ENGLAND YATEKWA NA WAGENI



IKIWA ndiyo asilimia 15 ya msimu wa Ligi Kuu England imechezwa, tayari kuna mambo mengi sana yamejitokeza ambayo yanaonyesha utakuwa ni msimu wenye kila aina ya mapya yatakayojitokeza.


Tayari mechi 58 zimechezwa kati ya 380 ambazo zinatakiwa kuchezwa kwa msimu mzima wa Premier League kwa 2014-15.
Msimu unaonyesha mabao yaliyofungwa ni mengi, wafungaji waliofunga mabao mengi hadi sasa ni wapya na wachache sana waliofanya vizuri msimu uliopita.
Lakini idadi ya mabao yaliyofungwa na mchezaji mmojammoja pia iko juu, hali inayoashiria ushindani na utamu zaidi wa mabao kupachikwa kwa wingi kwenye msimu.
Mshambuliaji Diego Costa wa Chelsea ndiye anaonekana kuwa matata zaidi katika upachikaji mabao baada ya kufunga nane katika mechi sita za Premier League ambayo ilionekana ni ngumu kwake kwa kuwa anatokea La Liga.
Maana yake kwa asilimia, Costa amepanda juu ya 100% kiufungaji na suala hapa linaloangaliwa ni kama ataweza kuendelea na kasi hiyo au baadaye mabeki watamtuliza.
Wageni:
Baada ya mechi sita, chati ya wanaoongoza kwa kupachika mabao inashikiliwa na wageni zaidi ambao wanaongozwa na Costa mwenye mabao hayo nane.
Unaweza kusema wageni wameiteka ‘nchi’. Hadi sasa inaonekana wengi wao si wale waliofanya vizuri msimu uliopita au hawakuwepo England.
Jose Ulloa wa Leicester ana matano, Graziano Pelle wa Southampton ana manne sawa na Nacer Chadli wa Tottenham na Sergio Aguero (Man City).
Hii inaonyesha hadi sasa wageni ndiyo wanashika chati ya juu zaidi ya wafungaji bora huku wale wakali kama Wayne Rooney na Robin van Persie wakiwa wanachechemea lakini hawako mbali kwa kuwa mmoja ana mabao mawili na mwingine matatu.          
Wastani:
Tayari mabao 164 yalikuwa yamefungwa kabla ya mechi za jana Jumapili na leo. Hadi sasa wastani wa idadi ya mabao uko juu sana, kwani unaonyesha kuna asilimia 2.83. Kimahesabu ni hivi, katika kila mechi iliyochezwa, tayari wastani wake ni mabao matatu.
Kama ni mabao matatu kwa kila mechi na mechi kawaida hupigwa ni 380, kuna uwezekano wa kufungwa mabao 1,140, lakini kwa kawaida lazima yatapungua, kwa hali inavyokwenda, inaonekana hayatashuka chini ya 1000.
Penalti:
Inaonekana hadi mechi sita kwa kila timu zimechezwa na idadi ya penalti si nyingi sana kwani ni asilimia 4.3, idadi ambayo ni ya chini.
Idadi ndogo ya mabao ya penalti na idadi kubwa ya mabao ya kufunga inaonyesha kiasi gani uwezo wa kufunga mabao bila aina hiyo ya adhabu uko juu.
Mwisho:
Ukitaka kujua ligi bado ni ngumu, angalia namna mabao yanayofungwa katika dakika za mwisho. Kwamba kila upande unakuwa haukubali hadi hatua za mwisho.
Tangu kuanzishwa kwa ligi hiyo inaonekana kuna wastani mkubwa wa mabao yaliyofungwa baada ya dakika 80. Hadi sasa katika mechi hizo chache, inaonyesha kuna wastani wa mabao asilimia 16 yamefungwa dakika 10 za mwisho.
Nyumbani & ugenini:
Idadi ya mabao kuwa juu pia imeongeza ugumu katika mechi za nyumbani na ugenini. Inaonekana ushindi wa mechi za nyumbani wastani wake ni 31%, ushindi wa ugenini ni 33% na sare ni 36%.
Hii inakuonyesha ligi hiyo haina mwenyewe kwa kuwa ushindi wa ugenini unaonekana uko juu kuliko nyumbani. Maana yake timu zimepoteza mfululizo nyumbani na hii inathibitisha ugumu wa ligi hiyo.
Hata hivyo, unaweza kusema ni mapema kwa kuwa ligi inaweza kuwa na mabadiliko kutokana na makocha, makipa, mabeki, viungo na washambuliaji wanavyobadilika na kutokana na makosa wanayoyafanya.
Inawezekana washambuliaji wakafunga mabao mengi zaidi au mabeki wakawa imara na kupunguza idadi ya mabao yanayofungwa wakishirikiana na makipa na viungo wakabaji.
Raha ya ligi hiyo ni kuendelea kuangalia, lakini wiki hizo sita, tayari zimeonyesha kuwa kuna harufu ya ushindani wa juu zaidi kuliko misimu mingine iliyopita.

Saturday, 20 September 2014

YANGA SC ‘ WAFALME WASIO NA MWISHO’



yanga-team
 Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Kitu kizuri huleta furaha ya siku zote katika dunia,  uzuri wake huwa wa kuendelea hata kama kitu cha zamani. Thamani ya kitu kizuri ni ‘ shida’ kukishusha chini kutokana na ubora wake. Kitu kikiwa kizuri ni ‘ pambo’ katika dunia hii. Yanga wameendeleza ‘ utawala’ katika Ngao ya Jamii baada ya ushindi wa kuvutia wa mabao 3-0 dhidi ya mabingwa wa Bara, Azam FC katika mchezo uluipigwa uwanja wa Taifa, Jumapili hii. Yanga ndiyo Wafalme tena wa Ngao ya Jamii, hawana mwisho kushinda.

Geilsons Santos ‘ Jaja’ alifunga mara mbili mara baada ya kuanza kwa kipindi cha pili na kuzima ‘ wasiwasi’ wote ambao ulitanda juu yake kama kweli ni mshambulizi-mfungaji. Amedhihirisha kuwa yeye ni Mbrazil mchezaji ambaye nilimuamini tangu Maximo alipoamua kumfanya ‘ kiongozi wa safu ya mashambulizi’ katika mfumo wa 4-5-1.
Timu ambayo ilionekana bora na ngumu kupitika katika kipindi cha kwanza ilikuwa ‘ nyanya’ nusu ya pili ya mchezo.  Azam waliibana Yanga licha ya kushambuliwa mara nne katika kipindi cha kwanza, ilionekana kama vile Marcio Maximo amechemsha  katika mfumo wake baada ya kushuhudia  timu yake ikishindwa kutengeneza nafasi. Jaja alionekana kutengwa huku mshambulizi namba mbili ambaye alitakiwa kucheza nyuma kidogo ya Jaja akishindwa kutimiza majukumu yake ipasavyo.
Maximo ameshinda taji lake la kwanza akiwa kocha, na hilo limekuja baada ya kutua Yanga. Alimuanzisha kiungo wa timu ya Taifa ya Tanzania, Said Juma baada ya kukosa huduma ya kiungo wake Mbrazil, Andrey Coutinho. Yanga walimiliki mpira na kiungo mchezesha timu Haruna Niyonzima alikuwa na kasi, nguvu na ufundi ambao uliifanya safu ya kiungo ya Yanga kucheza mchezo wa kasi. Nizar Khalfan alianza katika kikosi cha kwanza, Azam ilionekana kutawala mchezo licha ya kutotengeneza nafasi za kufunga.
Maximo alimtoa Juma na kumuingiza Hassan Dilunga katika dakika ya 38. Mabadiliko hayo yalilenga kuimarisha eneo la katikati ya uwanja ambalo lilionekana kuzidiwa baada ya Nizar kuanza kuchoka. Mrisho Ngassa alikuwa katika kiwango cha juu licha ya upinzani mkali kutoka kwa Erasto Nyoni. Ngassa alikaribia kufunga bao la ufundi kwa mpira wa umbali mrefu kutoka winga ya kulia, lakini golikipa Mwadini Ally aliuona ujanja wa winga huyo wa Taifa Stars.
Jaribio la kwanza la Jaja ilikuwa ni kupiga ‘ kishuti mtoto’ ambacho kiliokotwa na Mwadini mwishoni mwa kipindi cha kwanza, lakini ilikuwa ni onyo ambalo halikufanyiwa kazi na walinzi wa Azam kwani ‘ walitorokwa’ pasipo kukijua. Kama angepiga mpira ule kwa nguvu angefunga, si rahisi kumuona akipiga mpira nje. Yanga walikuwa makini kila idara, safu ya ulinzi chini ya golikipa, Deogratius Munishi ilijiamini huku umakini ukiwa mkubwa katika uchezaji wao. Juma Abdul alimbana, Lieonel Saint kila alipojaribu kuisaidia timu yake, Oscar Joshua alikuwa mgumu kwa Kipre Tchecthe, wakati Nadir Haroub na Kelvin Yondan walihakikisha hakuna nafasi ya wazi ambayo Kavumbagu anaipata.
Mara moja Kavumbagu alioneka kuwa tishio wakati alipotaka kuwahi pasi ya kupenyeza ya Salum Abubakary lakini alibanwa kifundi na Nadir ambaye alicheza ‘ tackling’ nzuri ndani ya eneo la hatari akiwa mchezaji wa mwisho. Kipre alitolewa baadae kipindi cha pili, na hivyo pia ilikuwa kwa Saint.
Kuingia kwa Saimon Msuva mara baada ya kuanza kwa kipindi cha pili kuliimaliza kabisa Azam katika eneo la kiungo. Dilunga alikuwa akikimbia na mipira upande wa kulia na kumpa wakati mgumu Shomari Kapombe ambaye hakupanda hata mara moja. Akiwa amechukua nafasi ya Nizar, Msuva alicheza kama kiungo wa kushoto, majukumu mapya ambayo aliyatimiza vizuri . Alikimbia na mpira katika winga ya kushoto na kupiga pasi ya kupenyeza kwa ‘ mchezaji bora wa mechi kwa upande wangu’ Niyonzima ambaye alipiga krosi kwa mguu wa kushoto iliyomaliziwa na Jaja katika dakika ya 53.
Ngassa ambaye alicheza kama msaidizi wa karibu wa Jaja katika kipindi cha pili alimpatia pasi muruha Jaja ambaye alipiga mpira wa juu kiufundi akimuacha kipa Mwadini akiutazama bila kujua cha kufanya. Bao hilo la pili katika dakika ya 65 liliimaliza kabisa Azam. Kocha, Joseph Omog akaamua kufanya mabadiliko yake ya kwanza kwa kuwaingiza uwanja Hamis Mcha na Kelvin Friday lakini tayari alikuwa amechelewa. Kikosi chake kilisambaratishwa na bao hilo na Niyonzima akawa anapiga pasi zinazofika huku akiichezesha timu yake.
Hussein Javu ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Jaja, alipiga pasi ndefu kwa Msuva ambaye alifunga moja ya mabao mazuri zikiwa zimesalia dakika tatu mchezo kumalizika. Yanga wameendeleza ‘ utamaduni wa kuishinda Azam kila katika mchezo wa vikombe’ waliifungwa mabao 2-0 katika fainali ya Kagame Cup, 2012 na waliichapa bao 1-0 katika mchezo wa Ngao ya Jamii mwaka uliopita. Azam ilizidiwa kutokana na kasi ya Yanga katikati ya uwanja. Jaja ataendelea kuwafunga , apewe heshima yake. Watu hitoa sifa nyingi nzuri kwa kilicho bora, kitu kizuri hakitoki nje kujitembeza.

Wednesday, 17 September 2014

MASHUJAA YAJIPANGA KULISHIKA JIJI LA DAR BAADA YA KUPAGAWISHA ZIARA YA MIKOANI UTAMBULISHO WA USHAMBA MZIGO



RAIS wa bendi ya Mashuja ‘Wana Kibega’, Charles Gabriel 'Chalz Baba' amesema amewataka wapenzi wa bendi hiyo wajitokeze kwa wingi katika maonesho yao matatu ya utambulisho wa albamu yao ya Ushamba mzigo.
Akizungumza na Waandashi wa Habari Dar es Salaam leo,  Chalz Baba alisema, baada ya kwenda mikoa mbalimbali, sasa wanamalizia Dar es Salaam kwa shoo tatu ili kuhitimisha maonyesho 30 ambayo walipanga kufanya.
Charles Baba kushoto akizungumza na Waandishi wa Habari 

Alisema shoo ya kwanza Dar es Salaam itakuwa Ijumaa hii katika ukumbi wa Ten Roung zamani Millennium Business Park, Jumamosi katika ukumbi wa Bwalo la Magereza na Jumapili kumalizia katika ukumbi wa Peace of Mine uliopo Tabata.
“Tumezunguka sana, mikoa mbalimbali hapa nchini, na tumefarijika kuwaona mashabiki na wadau wetu wanaotufanya Mashujaa tuzidi kuwepo mpaka sasa, hivyo basi katika hizi shoo zitaenda sambamba na uzinduzi wa albam yetu ya Ushamba Mzigo ambayo tunaiingiza rasmi sokoni ikiwa ya muziki na video,”alisema.
Naye Meneja wa bendi hiyo, Martine Sospeter alisema, ziara yao ilienda sawa, ambapo yeye alikuwa mkuu wa msafara, kwani kikubwa zaidi wanamshukuru Mungu walikwenda na kurejea salama.
Meneja wa mauzo wa Bavaria, Jestas Kyolike, akiwataka wadau na mashabiki wa bendi hiyo, kuendelea kutumia kinywaji hicho kwani wao wataendelea kuwaunga mkono Mashujaa bendi katika safari yao ya mafanikio zaidi.

SIMBA SC KUJIFUA LEO ZENJI, KUIVAA COASTAL UNION YA TANGA SIKU YA JUMAPILI


Wachezaji wa Simba SC wakifanya mazoezi Uwanja wa Chuo Kikuu cha Chukwani, Zanzibar asubuhi ya leo kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayoanza mwishoni mwa wiki. Simba SC iliyoweka kambi visiwani Zanzibar, itafungua dimba na Coastal Union ya Tanga Jumapili Uwanja wa Taifa

MAJANGA WILSHERE NJE MIAKA MIWILI BAADA YA KUTONESHA ENKA KATIKA MECHI YA DORTMUND


KOCHA Arsene Wenger amewalaumu wachezaji wake wa Arsenal kwa kushindwa kucheza vizuri wakichapwa mabao 2-0 na Dortmund jana, huku akirejea na kiungo Jack Wilshere akiwa majeruhi baada ya kuumia kwenye mchezo huo.
Wilshere alitonesha enka yake ya mguu wa kulia kikosi cha Wenger kikilala 2-0 katika mchezo wa kwanza wa makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Wlishere ameumia sehemu lie lie ambayo ilimfanya akawa nje ya Uwanja kwa miezi 17. "Ni vigumu kusema ni mbaya kiasi gani,"amesema kocha wa Arsenal. "Kwa kawaida haitakuwa mbaya sana, lakini nina wasiwasi mno kulingana na historia yake,".

Majanga; Kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere akiwa chini baada ya kuumia jana
Wilshere has injured his right ankle, which has been problematic for him over the past two years

ARSENE WENGER ANENA KUHUSIANA NA WELBECK KUPOTEZA NAFASI ZA MAGOLI DHIDA YA BORUSSIA



Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amefunguka kuhusiana na suala la mshambuliaji wake mpya Danny Welbeck kupoteza nafasi katika mechi dhidi ya Borussia Dortmund.


Wenger amemkingia kifua Welbeck ambaye alipoteza nafasi zaidi ya mbili katika yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Arsenal.
Welbeck alinunuliwa na Arsenal kwa pauni milioni 16 akitokea Manchester United.
Tokea jana usiku, amekuwa gumzo kwenye mitandao wadau wakionyesha kuchukizwa naye kupoteza nafasi huku Arsenal ikiambulia kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Wajerumani hao.

IKIFIKA JANUARI NI WENGER NA CASILAS, NG’ADU KWA NG’ADU


Kocha Arsene Wenger ameeleza wazi kuwa ataendelea kumfukuzia kwa kasi kipa Iker Casillas wa Real Madrid wakati wa dirisha dogo la usajili Januari, mwakani.

Tayari Wenger alionyesha nia yake ya kumpata Casillas ambaye amekaa Madrid kwa zaidi ya miaka 14 sasa.
Casillas anaonekana kutokuwa na furaha Madrid na hivi karibuni mashabiki walimzomea.
Lakini Wenger pia anaonekana hafurahii kwa asilimia mia kazi ya kipa wake namba moja Wojciech Szczesny ambaye alikuwa langoni walipochapwa 2-0 na Borussia Dortmund, usiku wa kuamia leo.

Bado haijajulikana kama Madrid itakuwa tayari kumuachia Casillas, lakini Wenger anaonyesha ataendelea kuweka wazi nia yake.

MAN UNITED KULA BATA, TIM NYINGINE ZA ENGLAND ZAWA BIZE LIGI YA MABINGWA ULAYA


Wakati timu nyingine za England zikiwa bize na Ligi ya Mabingwa Ulaya wachezaji wa Man United watafanyaje sasa.

Wameamua kula bata tu kama ambavyo imeonekana picha ambayo aliitupia kipa David de Gea akiwa an wenzake wanapata mlo wa usiku jana.
Kipa huyo alikuwa na wachezaji wengine kama Marcos Rojo, Rafael, Antonio Valencia, Andreas Pereira, Anderson, Angel di Maria, Ander Herrera and Juan Mata.

CHEKI, EVRA&TEVEZ WALIVYOSHANGILIA MABAO WAKIWA JUVENTUS


Kwa mara nyingine wachezaji wa zamani wa Man United, Carlos Tevez na Patrice Evra walishangilia pamoja wakiwa Juventus.

Juve iliitwanga Malmo ya Sweden kwa mabao 2-0 katika mechi iliyochezwa Turin na Tevez ndiye alikuwa shujaa aliyefunga yote mawili.
Wawili hao walikuwa Man United wakati wa kipindi cha Kocha Alex Ferguson.

BENZEMA AINGIA KWENYE REKODI MADRID BAADA YA KUFUNGA BAO LA1000


BENZEMA AKIPACHIKA BAO LA 1000...
Klabu ya Real Madrid imekuwa ya kwanza kufunga mabao 1000 katika michuano ya Ulaya.

Mshambuliaji wake Karim Benzema raia wa Ufaransa ndiye aliyefunga bao hio la 1000 wakati Madrid ikishinda mabao 5-1 dhidi ya Basle ya Uswiss katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi.
Benzema ameingia kwenye rekodi za klabu hiyo kwani wa mwisho alikuwa ni Cristiano Ronaldo ambaye alifunga bao la 900 mwaka 2011 wakati Madrid ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lyon.
Mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Roberto Soldado ndiye alifunga bao la 800 akiunganisha krosi ya David Beckham.
Lakini kabla ya Soldado, mshambuliaji nyota zaidi wa klabu hizo enzi hizo, Raul Gonzalez ndiye alipata rekodi ya kufunga bao la 700.

Alifunga bao hilo siku ambayo alikuwa ameweka rekodi ya kufikisha mabao 71 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Tuesday, 16 September 2014

PAUL SCHOLES AWATABIRIA MAKUBWA LIVEROOL MICHUANO YA UEFA



1410822292405_wps_24_LIVERPOOL_ENGLAND_SEPTEMB
Brendan Rodgers akiwapa mbinu wachezaji wake kuelekea katika mchezo wa kundi B wa ligi ya mabingwa.
MSHINDI wa ligi ya mabingwa ulaya,Paul Scholes anaamini kuwa Liverpool wanaweza kutoa upinzani mkali katika mashindano ya mwaka huu.
Liverpool, mabingwa mara tano wa ulaya wamerudi tena katika michuano hiyo msimu huu baada ya kukosekana kwa miaka mitatu.
Majogoo hao wa jiji wanaanza kampeni yao leo jumanne kwa kuwakaribisha mabingwa wa Bulgaria, Ludogorets.
Pia watachuana na mabingwa watetezi Real Madrid na wakali wa Uswizi , Basle katika michezo ya kundi B.
Scholes aliyekuwepo katika kikosi cha Manchester United kilichotwaa ubingwa mwaka 2008, anatarajia kuona Anfield inakuwa sehemu ngumu kwa timu zitakazotua hapo.
Mkongwe huyo aliyasema hayo wakati akichambua ligi ya mabingwa katika kituo cha ITV.
Scholes alisema: “Liverpool ni farasi weusi katika michuano ya mwaka huu.
“Brendan Rodgers amefanya kazi kubwa. Staili ya uchezaji aliyochagua inavutia kuitazama na wachezaji wameonekana kumuelewa. Nahisi watafanya vizuri tena kwa aina ya wachezaji walionao”.
“Faida kubwa kwao ni mashabiki wa nyumbani. Anfield ni sehemu inayotisha kwenda wakati wote, kitu ambacho Manchester City wamekosa”Liverpool boss Brendan Rodgers will be looking to use the Anfield crowd to his advantage
Kocha Brendan Rodgers
Liverpool walifanikiwa kufuzu UEFA baada ya kuonesha kiwango kikubwa msimu wa 2013/2014 wa ligi kuu England, lakini wakaishia kushika nafasi ya pili dhidi ya Manchester City.
Wamempoteza nyota wao Luis Suarez aliyejiunga na FC Barcelona, lakini Scholes anaamini Mario Balotelli anaweza kurithi nafasi hiyo.
Akimzungumzia Suarez, Scholes alisema: “Ni mchezaji mkubwa, lakini usisahau kuwa wamemsajili Balotelli,

JAMIE CARRNAGHER ADAI ARSENAL HAWAWEZI KUNYANYUA KOMBE LA LIGI KUU


1410818546684_wps_6_Jamie_Carragher
Jamie Carragher usiku wa jana alidai kuwa Arsenal haiwezi kushinda taji la ligi kuu.
JAMIE Carragher anaamini Arsenal hawatashinda ubingwa msimu huu baada ya kushindwa kulinda bao la kuongoza dhidi ya Manchester City jumamosi iliyopita.
Bao la dakika ya 83 la Martin Demichelis lilifanya mechi imalizike kwa sare ya 2-2 katika uwanja wa Emirates.
Kwa matokeo hayo, maana yake tayari Arsenal wameshatoa sare katika mechi zao tatu za ligi kuu na kuachwa nyuma kwa painti sita na vinara Chelsea. 
Beki wa zamani wa Liverpool, Carragher amesema Arsenal imekuwa nyuma sana dhidi ya Chelsea msimu huu kama ilivyokuwa mwaka jana.
Akizungumza na Sky Sports, Carragher alisema: “Nilizungumza mwanzoni mwa msimu, sidhani kama Arsenal watashinda ubingwa. Ninavyoiona Arsenal ni sawa na Chelsea ambapo moja ilimaliza nafasi ya tatu na nyingine ya nne. Yawezekana walitumia kiasi cha fedha kinachoelekea majira ya kiangazi.
“Kwanini Arsenal haikumpata [Diego] Costa. Danny Welbeck anaweza kuwa usajili mzuri. Wanahitaji beki wa kushoto, Chelsea walienda Atletico Madrid na kumpata Felipe Luis. Wanafanya kila wanachotaka kufanya”.
Arsenal walipata changamoto ya kuingia nne bora msimu uliopita na Carragher anaamini washika bunduki hao wa London hawawezi kutwaa taji msimu huu.
Martin Demichelis equalised for Manchester City late on to rescue a 2-2 draw at Arsenal on Saturday
Jack WIlshere's fabulous strike had put the Gunners 2-1 up at the Emirates Stadium

MAMBO 5 MUHIMU DANNY WELBECK KU ‘SHAINI’ ARSENAL



455290_gallery
Moja kati ya habari kubwa sana za usajili wa kiangazi msimu huu nchini Uingereza ni uhamisho wa mshambuliaji mwenye nguvu na mbio Danny Welbeck kutoka Manchester United kwenda Arsenal kwa ada ya paundi 16m. kijana huyu mwenye miaka 23 pamoja na kubezwa na mashabiki wengi lakini ana kitu ambacho kwa macho ya kawaida hakikuonekana pale Old Trafford. Ndio maana sivishangai vilio vya wakongwe wa Manchester United kama Paul Scholes, David Becham na Rio Ferdinand wakionesha kusikitishwa kwao kwa kuondoka kwa kijana huyo aliyekulia mjini Manchester tangu akiwa mdogo. Zifuatazo ni sababu zinazoweza kumng’arisha Dany Welbeck Arsenal;
1.Kutaka kuthibitisha uwezo wake
Welbeck kama ambavyo mchezaji yeyote angeweza fanya, atajituma uwanjani ili kuonesha Manchester United walimuuza kimakosa huku pia akitaka kuwaondoa shaka mashabiki wa Arsenal kwamba mzee Wenger hakukosea kumsajili.
2. Uhakika wa kucheza kikosi cha kwanza
Kuumia kwa Olivier Giroud kunamfanya Dany awe na upinzani mdogo na mshambuliaji aliye fiti Yaya Sanogo. Tofauti na ilivyokua Manchester United, Wayne Rooney na Robin Van Persie walimpa wakati mgumu Welbeck kupata nafasi kikosi cha kwanza huku usajili wa Radamel Falcao ungemfanya asipate nafasi kabisa.
3. Viungo wa Arsenal
Tofauti na Manchester United ambapo hakukua na viungo wenye uwezo wa kucheza na kutengeneza nafasi kwa washambuliaji wao kufunga magoli, lakini uwezo wa viungo wazuri kama Jack Wilshere, Mesut Ozil, Aaron Ramsey, Carzola na wengine, sina shaka Dany atafunga magoli mengi tofauti na alivyokua Old Trafford.
4. Matarajio hafifu ya mashabiki wa Arsenal kwa kijana huyo
Presha sio kubwa kwa Welbeck kufanya vizuri kwa washika mitutu hao wa London kutokana na ukweli kwamba mashabiki wengi wa gunners hawana uhakika na uwezo wa mshambuliaji huyo raia wa Uingereza na hivyo Dany anaweza kucheza vizuri kwani mashabiki hawamtarajii makubwa.
5.Uwezo wa mwalimu Arsene Wenger
Wengi mtakubaliana na mimi jinsi Arsene Wenger alivyo wabadilisha wachezaji wake wengi kutoka kua wachezaji wa kawaida hadi kuwa wachezaji wa kiwango cha dunia kama Aaron Ramsey na wenzake huku akiwa na uwezo mkubwa wa kuwa saikoloji wachezaji wake.
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=6454#sthash.tE5MnX1O.dpuf

MAN UNITED YATOA PICHA YA KIKOSI KIPYA, SURA 10 MPYA


9/16/2014 08:58:00 PM


Kikosi kipya cha Manchesterpamoja na kocha Louis van Gaal na benchi lake lima la ufundi mstari wa nyuma kutoka kushoto ni Jonny Evans, Marouane Fellaini, Chris Smalling, Tyler Blackett, Marcos Rojo* na Phil Jones, mstari wa tatu ni Antonio Valencia, Anderson, Daley Blind*, Robin van Persie, Michael Carrick, James Wilson, Andreas Pereira na Ashley Young, mstari wa pili ni Gary Walker*, Marcel Bout*, Dr Steve McNally, Luke Shaw*, Ben Amos, Dave De Gea, Anders Lindegaard, Angel di Maria*, Frans Hoek*, Alec Wylie na Neil Hough na wa mbele ni Rafael, Ander Herrera*, Radamel Falcao*, Albert Stuivenberg*, Wayne Rooney, Louis van Gaal*, Darren Fletcher, Ryan Giggs, Juan Mata, Adnan Januzaj na Jesse Lingard. Wote waliowekewa nyota ni wapya 
A total of 17 players or staff have left the club since the beginning of the 2013-14 season under David Moyes - United finished seventh in the Premier League
Jumla ya wachezaji 17 na viongozi wameihama klabu hiyo tangu mwisho wa msimu wa 2013-14 chini ya kocha David Moyes - United ikimaliza nafasi ya saba katika Ligi Kuu England. Mstari wa nyuma ni Danny Welbeck, Phil Jones, Chris Smalling, Jonny Evans, Marouane Fellaini, Rio Ferdinand, Michael Carrick na Robin van Persie, mstari wa tatu Masseur Garry Armer, mtathmini viwango vya wachezaji  Paul Brand, mkuu wa idara ya fiziki Tony Strudwick, Antonio Valencia, Darren Fletcher, Wilfried Zaha, Adnan Januzaj, Fabio da Silva, mchua misuli Rod Thornley, mtunza vifaa Alec Wylie, na daktari wa viungo, Neil Hough, mstari wa pili mtunza vifaa msaidizi Ian Buckingham, daktari wa viungo Rob Swire, Dk Steve McNally, Alexander Buttner, Sam Johnstone, Anders Lindegaard, David de Gea, Ben Amos, Ashley Young, kocha Phil Neville, mchua misuli Andy Caveney na kocha wa makipa Chris Woods. Mstari wa mbele ni Shinji Kagawa, Rafael da Silva, Anderson, Nani, kocha Msaidizi Steve Round, Ryan Giggs, Kocha Mkuu David Moyes, Nemanja Vidic, kocha Jimmy Lumsden, Patrice Evra, Javier "Chicharito" Hernandez, Tom Cleverley na Wayne Rooney. Wote ambao picha zao si za rangi wameondoka.

'BABU' ANELKA ASAINI TIMU YA INDIA, MWENYEWE AMEFURAHI KINOMA


MSHAMBULIAJI wa zamani wa Real Madrid na Chelsea, Nicolas Anelka ametangaza kujiunga na Mumbai City ya Ligi Kuu ya India.
Imeripotiwa kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35, ambaye amekuwa hana timu tangu aondoke West Brom Machi mwaka huu, amekubali mkataba wa muda mfupi na timu ya ISL inayofundishwa na Peter Reid.
"Ninayo furaha kujiunga na Mumbai City FC na nimevutiwa sana kujiunga na Ligi Kuu ya India," ameandika Anelka kwenye akaunti yake ya Twitter.

Nicolas Anelka amekuwa hana timu tangu ameondoka West Brom Machi mwaka huu

KOCHA AZAM ABWAGA MANYANGA SIKU MOJA BAADA YA MECHI NA YANGA SC


KOCHA wa Azam Academy, Vivik Nagul raia wa India, ameacha kazi baada ya kuitumikia klabu kwa miaka mitatu ya mafanikio.
Nagul aliaga rasmi Azam FC baada ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga SC Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Azam FC ilifungwa 3-0.
Nagul aliyeanza kazi Azam FC mwaka 2011, ameondoka baada ya kupata Mkataba mzuri zaidi kwao India.
Nagul alikwenda India kumpeleka mchezaji Ismail Gambo ‘Kussi’ kwa matibabu mwezi uliopita na baada ya kurejea mwezi huu, akatoa taarifa ya kuacha kazi.
Ameondoka; Vivik Nagul ameacha kazi Azam Acadrmy na kurejea kwao India

Nagul aliiongoza Azam FC kwa mara ya mwisho katika mchezo wa utangulizi wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam, Academy ikiwafunga watoto wa Yanga mabao 2-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Nagul atakumbukwa Azam FC kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kuinua vipaji vya wachezaji waliopandishwa timu ya kwanza kama Joseph Kimwaga, Aishi Manula, Kevin Friday, Farid Mussa, Gariel Michael na wengineo.
Aliiwezesha Azam Academy kutwaa mataji kadhaa kama Kombe la Uhai na Rollingtosn pamoja na pia kuwa tegemeo la timu za taifa za vijana nchini kwa wachezaji wengi wanaozalishwa hapo kuchukuliwa timu za kuanzia U17 hadi U20.
Kwa ujumla, Nagul ameifanya Azam Academy kuwa msingi imara wa vipaji si tu kwa klabu hiyo inayomilikiwa na Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake, bali pia na taifa kwa ujumla.       
Nagul pia kuna wakati alikuwa anakaimu ukocha wa timu ya wakubwa na kuiongoza vizuri, inapotokea dharula za makocha wa timu hiyo kuachishwa kazi
.