
Kumbe jana usiku wakati Luke Shaw anapata jeraha kubwa ambalo
litamfanya akae nje ya uwanja angalau kwa miezi 6, wazazi wake
walikuwepo uwanjani kumuangalia mtoto wao akicheza mechi ile.
Bahati mbaya wamemshuhudia mtoto wao akipata maumivu makali badala ya
kumuona akiisaidia club yake. Taarifa zinasema kwamba wazazi hao
walishindwa kumalizia kuangalia mechi walielekea hospitali ambapo Luke
alipelekwa. Siku ya leo Luke Shaw anategemea kufanyiwa matibabu kamili
ili kuendelea kuuguza mguu wake.
Luke amelazwa kwenye hospitali ya St
Anna Ziekenhuis ambapo Ed Woodward amemtembelea leo asubuhi.
Moreno ambae alihusikka kwenye rafu hiyo alisema, “Najiskia vibaya
sana kwake najiskia vibaya snaa kwasababu najua jinsi anavyojiskia. Kitu
kama kile kimewai kunitokea mimi kwenye kombe la dunia. Namtakia heri
apone haraka na halikua lengo langu”



0 comments:
Post a Comment