![]() |
| David Browne |
Mwana masumbwi mmoja wa Australia
amefariki siku nne baada ya kupoteza fahamu alipopigwa 'knock out'
katika pigano la kijimbo mjini Sidney.
Brown ambaye ni baba ya watoto wawili alipelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kabla ya mitambo inayomsadia kuzimwa alipokosa kuimarika kiafya.
Muungano wa wahudumu wa matibabu nchini Australia umetaka mchezo wa ndondi kupigwa marufuku nchini humo kufuatia kifo hicho.
Kifo cha Browne kinajiri wiki sita baada ya mwanamasumbwi wa Queensland Braydon Smith kuzirai na kufariki kufuatia pigano la uzani wa Feather nyumbani kwake huko Toowoomba.




0 comments:
Post a Comment