![]() |
Serena katika mkutano na vyombo vya habari baada ya mechi hiyo. |
Bingwa wa mchezo wa tenisi upande wa
wanawake Serena Williams amepata pigo kubwa katika mashindano ya US
Open baada ya kushindwa kwa seti 2-6 6-4 6-4 na Muitaliano Roberta Vinci
katika nusu fainali.
''Hili ni pigo kubwa katika historia ya mchezo huu kutokana na kile kilichofanyika''.
![]() |
Serena akisalimiana na Vinci baada ya mechi hiyo |
William alianza mechi hiyo akiwa hajashindwa katika mechi 33 katika Grand Slum tangu machindano ya Wimbledon ya mwaka 2014.
Alikuwa amejitahidi kufikia rekodi iliowekwa na Steffi Graf ya mwaka 1988 ambapo mwana dada huyo alizoa mataji yote mwaka huo na alikuwa akikabiliana na mchezaji ambaye alimshinda mara nne bila kushindwa seti moja.





0 comments:
Post a Comment