![]() |
| Kikosi maalum kimetumwa kuchunguza tukio la mauaji |
Misri imesema jeshi lake la ulinzi
limeua raia 12 kwa bahati mbaya,wakiwemo watalii kutoka Mexico wakati
wa operesheni ya kupambana na ugaidi.
kwa upande wa Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto amekemea tukio hilo na kusema kuwa ameitaka serikali ya Misri kufanya uchunguzi wa kina, Wizara ya mambo ya nje ya Mexico imethibitisha kuwa takriban raia wake wawili wameuawa na kuongeza kuwa inafanya jitihada kuwatambua waathirika wengine.
tamko la wizara limesema , Balozi wa Mexico nchini Misri, Jorge Alvarez Fuentes alitembelea hospitali na kuzungumza na raia watano wa Mexico ambao hali zao zilikuwa njema.




0 comments:
Post a Comment