This is default featured post 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Tuesday, 22 September 2015

Walinzi wa rais Burkina Faso ‘kupigana’

Burkina Demos
Wanajeshi wamelakiwa kwa shangwe na waandamanaji ambao wamekuwa wakipinga mapinduzi
Viongozi wa mapinduzi Burkina Faso wamekataa kutii makataa ya kusalimu amri na kutishia kupigana vita wakishambuliwa.

Walinzi wa rais walioongoza mapinduzi walikuwa wamepewa hadi saa nne saa za huko kuweka chini silaha na wanajeshi ambao walifika katika mji mkuu Ouagadougou usiku.

 

Hayo yamejiri huku marais wa mataifa ya Afrika Magharibi chini ya muungano wa Ecowas wakikusanyika Abuja, Nigeria kufahamishwa na Rais wa Senegal Macky Sall kuhusu hatua zilizopigwa katika kutatua mzozo huo.

Duru zinasema mashaurino ya kupatanisha wanajeshi hao na walinzi waliopindua serikali yaligonga mwamba usiku, suala tata likiwa hatima ya walinzi hao wa rais.

Rais Sall amekuwa akiongoza mashauriano akishirikiana na mwenzake wa Benin Yayi Boni.
Barabara za kuelekea ikulu ya rais hazina watu wala magari huku hali ya wasiwasi ikiendelea kutanda Ouagadougou.

Kiongozi wa mapinduzi Jenerali Gilbert Diendere alikuwa awali ameambia BBC kwamba yuko tayari kurejesha mamlaka kwa uongozi wa kiraia, lakini baada tu ya mpango wake wa kumaliza mzozo wa sasa kuungwa mkono na viongozi wa mataifa ya eneo hilo.

Akiongea kutoka mafichoni, Jenerali Diendere aliambia BBC: “Kuwa tayari kusalimu amri? Hatujafika huko bado …Tungependa kuendelea na mazungumzo na tunawaambia wote kwamba tuko tayari kutekeleza maamuzi ya Ecowas (kundi la mataifa ya Afrika Magharibi).”

Aidha, aliomba radhi kwa raia, akisema hilo tu ndilo wawezalo kufanya kwa sasa.

Walinzi wa rais waliopindua serikali ni watiifu kwa kiongozi aliyetimuliwa mamlakani mwaka jana Blaise Compaore.

Walimzuilia Kaimu Rais Michel Kafando Jumatano iliyopita, na kumtangaza Jenerali Diendere kuwa kiongozi mpya.

Tangu wakati huo, watu 10 wameuawa kwenye makabiliano kati ya waandamanaji wanaopinga mapinduzi hayo na maafisa wa usalama. Watu zaidi ya 100 wamejeruhiwa.

Balozi wa Ufaransa nchini Burkina Faso, Gilles Thibault, aliandika kwenye Twitter kwamba Bw Kafando ameachiliwa huru na sasa yumo kwenye makao ya balozi huyo.

Monday, 21 September 2015

MWALIMU ALIYETOWEKA MABAKI YA MWILI WAKE YAPATIKANA SHAMBANI KWA MWALIMU MWENZAKE....

 

 Mabaki ya Mwili wa Aliyekuwa Mwalimi mkuu shule ya msingi Muholo kata ya Luana wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe aliyepotea ktk mazingira ya kutatanisha tareh 29 mei 2015 Majuto Haule mwili wake umekutwa umefukiwa katika shamba la mwalimu Vincent Haule Nje kidogo ya kijiji cha Muholo leo

Wednesday, 16 September 2015

wazazi wa luke shaw wamshuhudia mtoto wao akiumia uwanjani>> na kusema hivi

 2C5A626400000578-0-image-a-17_1442391403899

Kumbe jana usiku wakati Luke Shaw anapata jeraha kubwa ambalo litamfanya akae nje ya uwanja angalau kwa miezi 6, wazazi wake walikuwepo uwanjani kumuangalia mtoto wao akicheza mechi ile.

Bahati mbaya wamemshuhudia mtoto wao akipata maumivu makali badala ya kumuona akiisaidia club yake. Taarifa zinasema kwamba wazazi hao walishindwa kumalizia kuangalia mechi walielekea hospitali ambapo Luke alipelekwa. Siku ya leo Luke Shaw anategemea kufanyiwa matibabu kamili ili kuendelea kuuguza mguu wake.

Luke amelazwa kwenye hospitali ya St Anna Ziekenhuis ambapo Ed Woodward amemtembelea leo asubuhi.

Moreno ambae alihusikka kwenye rafu hiyo alisema, “Najiskia vibaya sana kwake najiskia vibaya snaa kwasababu najua jinsi anavyojiskia. Kitu kama kile kimewai kunitokea mimi kwenye kombe la dunia. Namtakia heri apone haraka na halikua lengo langu”

RATIBA YA MECH ZA LEO UEFA Champions League

UEFA Champions League




Bayer Levkn v BATE Bor 21:45 at BayArena
Roma v Barcelona 21:45 at Olimpico
Dinamo Zagreb v Arsenal 21:45 at Maksimir

Olympiakos v Bayern Mun 21:45 at Georgios Karaiskakis Stadium

Chelsea v Maccabi Tel Aviv 21:45 at Stamford Bridge

Dynamo Kiev v FC Porto 21:45 at Kiev Olympic Stadium

KAA Gent v Lyon 21:45 at Ghelamco Arena

Valencia v Zenit St P 21:45 at Mestalla

Wagombea wa michezo ya Olimpiki 2024 watangazwa

 

Wanaogombea kuandaa mashindano ya michezo ya Olimpiki mnamo mwaka 2024 wametangazwa.
Miji hiyo ni pamoja na Paris- Ufaransa, Roma- Italia, Los Angeles nchini Marekani, Budapest pamoja na Hamburg.

Maamuzi ya mwisho yatatangazwa nchini Peru katika mkutano wa kamati kuu ya Olimpiki katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Mwaandishi wa habari za michezo wa BBC , anasema kuwa miji miwili ambayo inapigiwa upatu wa kuteuliwa ni Paris na Los Angeles.

Bondia afariki baada ya kupigwa 'knock out'

David Browne
Mwana masumbwi mmoja wa Australia amefariki siku nne baada ya kupoteza fahamu alipopigwa 'knock out' katika pigano la kijimbo mjini Sidney.

Davey Browne mwenye umri wa miaka 28 aliangushwa na Carlo Magali wa taifa la Ufilipino mwisho wa raundi ya 12 katika taji la uzani wa Feather siku ya Ijumaa.

Brown ambaye ni baba ya watoto wawili alipelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kabla ya mitambo inayomsadia kuzimwa alipokosa kuimarika kiafya.

Muungano wa wahudumu wa matibabu nchini Australia umetaka mchezo wa ndondi kupigwa marufuku nchini humo kufuatia kifo hicho.

Kifo cha Browne kinajiri wiki sita baada ya mwanamasumbwi wa Queensland Braydon Smith kuzirai na kufariki kufuatia pigano la uzani wa Feather nyumbani kwake huko Toowoomba.

Hapatoshi >>>Lissu amjibu JK, Kuhusiana na SAKATA LA Richmond

Pg 1 lowassa

MWANASHERIA mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amemkingia kifua mgombea urais wa chama hicho, Edward Lowassa akisema hahusiki na sakata la Richmond.

Lissu ametoa kauli hiyo siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kunukuliwa na gazeti moja akisema kuwa muhusika wa Richmond ni yule anayetembea na Lissu katika kampeni huku akimtaka amtaje kabla Rais Kikwete hajafanya hivyo.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Viwanja  vya Shule  ya Msingi  ya Kiwanja  cha  Ndege Manispaa  ya Morogoro jana, Lissu alimtaja kwa jina kigogo wa serikali akisema ndiye muhusika mkuu wa  wa Richmond na si Lowassa.

Kauli hiyo ya Lissu haitofautiani na ile ya Lowassa aliyoitoa alipokuwa akijiunga na Chadema ambapo alisema katika moja ya vikao vya serikali vya kujadili sakata hilo, kiongozi mmoja alisema amepata amri kutoka ngazi za juu kwamba asaini mkataba wa kampuni hiyo.

Lissu alisema ni vema Watanzania kutambua kuwa mmiliki halali wa Richmond ambayo imebadilishwa majina kutoka Dowans hadi Symbion kwa sasa yupo ngazi za juu serikalini.
‘’Huyu mzee wa watu wameshampaka matope vya kutosha na wala hajatoka mbele za watu kulalamika, anatumia busara zaidi.

‘’Tunaishangaa serikali kuendelea kuwadanganya wananchi bila ya huruma kwa kudai kampuni hizo zote zinamilikiwa na Lowassa, kama  kungekuwa na ukweli wowote, kwanini wanaendelea  kulipa hayo madeni  ya mabilioni ya fedha?

“Ni lazima Watanzania watambue kuwa Richmond ilijadiliwa bungeni ikiwa chini ya mwenyekiti wake Dk. Harisson Mwakyembe  ambaye alikuwa kwenye kamati ya Bunge iliyochunguza mkataba wa Kampuni ya Richmond na mwishowe kuja kuibuka kashfa ya mafisadi  ambao walikuwa 11,” alisema na kuongeza.

“Katika mlolongo wa mafisadi waliotajwa namba tisa alitajwa Lowassa wakati akiwa waziri mkuu, lakini hakuhusika moja moja na suala hilo,” alisema.

Lissu alisema katika orodha hiyo namba 10 alitajwa kiongozi mmoja mstaafu na baadae akataja tena jina la kigogo mwingine ambaye alisema huyo ndiye mmiliki wa kampuni hiyo.
Alisema Lowassa ambaye anatembea naye katika kampeni zake hahusiki hata kidogo na suala hilo ila aliwajibika kisiasa ili kuiokoa serikali, kwa kuwa alikuwa msimamizi wa serikali hiyo.
Lissu alisema ili kuondoa mfumo mbovu ni lazima wahakikishe wanaing’oa serikali iliyopo madarakani kwa kipindi cha muda mrefu, kwani hiyo ndio chanzo kikuu cha umaskini.

Lowassa: na wakulima
Kwa upande wake Lowassa, alisema serikali yake itakuwa rafiki kwa wakulima na wafugaji na kuwa atatoa elimu bora bila malipo yoyote.

“Hakutakuwa na mambo ya michango ya ajabu ajabu, tutatoa elimu ya bure lakini iliyo bora,” alisema.
Kuhusu suala la viwanda vya miwa, alisema atahakikisha viwanda vinavyowezekana vitarudishwa mikononi mwa serikali.
Alisema pia kuwa, wafanyabiashara ndogo ndogo wakiwamo mama lishe na bodaboda, atawahakikisha wanaendelea kuwa rafiki zake.

Sumaye: CCM inahukumiwa kwa uongo wake
 Waziri  mkuu  mstaafu, Fredrick Sumaye,  alisema   kwa sasa CCM   inahukumiwa  kwa  kusema  uongo  kwa  kipindi cha  miaka 50 tangu  taifa lipate  uhuru 

Alisema katika kipindi hicho, chama hicho kimeshindwa kukidhi mahitaji muhimu ya Watanzania, hivyo wananchi wamechoka  kudanganywa .

Aidha Sumaye  alidai  Watanzania  bado  wamekuwa  wakiishi  katika mazingira  magumu  na  yenye  shida  pamoja  na CCM  kuja  na  sera  yake  ya  uongo  ya maisha  bora  kwa kila Mtanzania .
“Ni wazi  hakuna  ubishi  kama  Watanzania  sasa  wamechoshwa  na uongo wa CCM, ndio  maana   wametuunga  mkono  kwa  asilimia 100  katika mikutano  yote  ya  Ukawa  pasipo  kuletwa  na magari  kama  ilivyo  katika mikutano  yao”alisema  Sumaye .

Alisema uongo  wa CCM unajionesha  wazi wazi  kwenye  sekta  ya  kilimo, afya , miundombinu, elimu  na  kudai   kuwa  hayo  ni maeneo ambayo  yanawatesa  kwa  kiasi  kikubwa na kuyaona maisha  kuwa  magumu.

Alisema  kuwa  dalili  za  Watanzania  kuunga mkono  ukawa  ni  dalili  tosha  kuonesha  wanahitaji mabadiliko  ndani  ya   taifa , pasipo  kushawishika  na pesa .

“Hapa  mmekuja  kwa  upendo  wenu na taifa lenu hamjaletwa  kwa  magari  kama  ilivyo  katika  mikutano  yao (CCM),” aliongeza  Sumaye .

Naye Mjumbe  wa Kamati  ya Utendaji  Kanda  ya  Kati wa Chadema, Mathew Likwina  akizungumza na  wanachama  wa  chama  hicho alisema  kuwa  lengo  la UKAWA   ni  kufanya  mabadiliko   ya  kimfumo.

Alisema  kuwa  kuondoa  mfumo sio  kubadilisha  kiongozi  mmoja  wa ccm  , bali  ni kuondoa  uongozi  wote  wa  CCM usio  na mfumo mzuri  katika  kuleta maendeleo  ya  taifa  na watu  wake .
Aidha   alidai  kuwa  kama  Watanzania  wataiondoa CCM  taifa  linauhakika  mkubwa   wa  kuwa na mfumo mzuri Wenye  kujali   maslahi  ya wananchi badala  ya  sasa  CCM imekuwa na mifumo  ya  kujali  watu wachache  na  familia  zao .

NEC: Lushoto hawatapiga kura ya ubunge

JAJILUBUVA

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema wananchi wa Jimbo la Lushoto mkoani Tanga, hawatapiga kura ya kuchagua mbunge katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25.

Hatua hiyo, inatokana na kufariki dunia kwa aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Mohamed Mtoi (39).

Mtoi, alifariki dunia Jumamosi iliyopita baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kuacha njia na kupinduka kisha kudumbukia kwenye korongo wilayani Lushoto.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva, alisema sheria inaruhusu kama mgombea atafariki dunia wakati huu wa uchaguzi uahirishwe.

“Wananchi wa Lushoto hawatapiga kura ya mbunge Oktoba 25, tumeahirisha hadi hapo baadaye tutakapowatangazia na chama husika kitapokuwa kimepata mgombea,” alisema Jaji Lubuva.

Kulingana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Zubery Mwombeji, Mtoi alipata ajali katika eneo la Magamba Coast, Kata ya Magamba wilayani Lushoto.

Alisema gari hilo lilikuwa likiendeshwa na Miraj Nuru (43), likitokea Tarafa ya Mlola kwenda Mkuzi baada ya kumaliza shughuli za kampeni.

Facebook, Kuja na mabadiliko haya wakati wowote !!



 

Facebook ndio mtandao wa Kijamii ambao unatumiwa na watu wengi zaidi, Takwimu zinaonesha Duniani kuna jumla ya watu kama Bilioni 7 hivi, alafu Ripoti ya The Statistics Portal 2015 inaonesha watumiaji wa Mitandao ya Kijamii wako Bilioni 1.96, na kati yao zaidi ya 70% ni watumiaji wa mtandao wa Facebook !!

3d illustration of a facebook logo standing in front of an upright map of the world on a blue reflective surface

Mark Zuckerberg katupasha kuhusu mipango mingine ya Facebook, sasahivi kama ukiandika post yoyote au ukiingia kwenye ukurasa wa mtu yoyote wa Facebook unakutana na alama tatu, alama ya ‘LIKE’, ‘COMMENT’ na alama ya ‘SHARE’… lakini  CEO Zackerberg anasema ni maombi ya muda mrefu watumiaji wa Facebook wanataka iwepo na alama ya DISLIKE, yani kama kitu hujakipenda unabonyeza tu hapo. 

 1014_mark-zuckerberg-e1413303739290-1940x1091
Watu wengi wameulizia kuhusu kuwepo alama hiyo, leo ni siku maalum kwa sababu natangaza rasmi kwamba tunashughulikia hicho kitu na muda sio mrefu tutakiweka kwenye majaribio‘ >>> Mark Zuckerberg.

UEFA: Man United, Man City zachapwa


Timu za Uingereza za Man United na Man City zimeanza vibaya michuano ya kombe la kilabu bingwa barani Ulaya baada ya kuchapwa.

Man United wakiwa ugenini nchini Uholanzi wamelala kwa kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya PSV. Memphis Depay alianza kuifungia timu yake bao la kwanza kabla ya Héctor Moreno wa PSV kusawazisha kisha Luciano Narsingh akafunga bao la ushindi.

Man City nao wakiwa katika dimba lao la Etihad walikubali kipigo cha mabao 2-1 toka kwa vibibi vizee vya Turin Juventus mabao ya Juve yakifungwa na Álvaro Morata na Mario Mandzukic huku bao la kujifunga la beki Giorgio Chiellini, likiwapa Man City bao moja.

Real Madrid wakiwa nyumbani Santiago Bernabeu wameshinda kwa kishindo kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Shakhtar Donetsk, Cristiano Ronaldo akifunga hat trick na Karim Benzema akifunga bao moja.

Matokeo mengine ya michuano hii ni:
PSG 2 – 0 Malmö FF
VfL Wolfsburg 1 – 0 CSKA
Benfica 2 – 0 FC Astana
Galatasaray 0 – 2 Atletico Madrid
Sevilla 3 – 0 Borussia Mönchengladbach

Monday, 14 September 2015

Jeshi la Misri ladai kuua watu 12 kimakosa

Kikosi maalum kimetumwa kuchunguza tukio la mauaji

Misri imesema jeshi lake la ulinzi limeua raia 12 kwa bahati mbaya,wakiwemo watalii kutoka Mexico wakati wa operesheni ya kupambana na ugaidi.

Wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo imetuma kikosi kwa ajili ya kufanya uchunguzi kuhusu tukio hilo

kwa upande wa Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto amekemea tukio hilo na kusema kuwa ameitaka serikali ya Misri kufanya uchunguzi wa kina, Wizara ya mambo ya nje ya Mexico imethibitisha kuwa takriban raia wake wawili wameuawa na kuongeza kuwa inafanya jitihada kuwatambua waathirika wengine.

tamko la wizara limesema , Balozi wa Mexico nchini Misri, Jorge Alvarez Fuentes alitembelea hospitali na kuzungumza na raia watano wa Mexico ambao hali zao zilikuwa njema.

Saturday, 12 September 2015

Serena William apata pigo kwenye mchezo wake wa Nusu fainali



Serena katika mkutano na vyombo vya habari baada ya mechi hiyo.


Bingwa wa mchezo wa tenisi upande wa wanawake Serena Williams amepata pigo kubwa katika mashindano ya US Open baada ya kushindwa kwa seti 2-6 6-4 6-4 na Muitaliano Roberta Vinci katika nusu fainali.

''Ni pigo kubwa'', alisema aliyekuwa bingwa mara mbili katika mchezo huo Tracy Austin.
''Hili ni pigo kubwa katika historia ya mchezo huu kutokana na kile kilichofanyika''.


Serena akisalimiana na Vinci baada ya mechi hiyo



William alianza mechi hiyo akiwa hajashindwa katika mechi 33 katika Grand Slum tangu machindano ya Wimbledon ya mwaka 2014.

Alikuwa amejitahidi kufikia rekodi iliowekwa na Steffi Graf ya mwaka 1988 ambapo mwana dada huyo alizoa mataji yote mwaka huo na alikuwa akikabiliana na mchezaji ambaye alimshinda mara nne bila kushindwa seti moja.