This is default featured post 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Thursday, 22 January 2015

NEC: Hakuna mabadiliko ya ratiba Daftari la Wapigakura

Mkurungenzi wa Uchaguzi Julius Malaba
 

Wakati Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ikisisitiza kuwa ratiba ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura itakuwa kama ilivyopangwa, Chadema imesema itachukua uamuzi mgumu endapo shughuli hiyo itachelewa na kuharibu mchakato wa Kura ya Maoni.

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Julius Malaba alisema jana kuwa uboreshaji huo utaanza Februari 16 na utamalizika kwa wakati ili kupisha ratiba ya Kura ya Maoni.
“Ratiba inazingatiwa, vifaa vitafika kwa wakati na kuanza kazi,” alisema Malaba.
Hata hivyo, Chadema imeeleza kwamba Kamati Kuu yake itakayokaa leo itajadili hatima ya mchakato huo kabla ya kupiga Kura ya Maoni Aprili 30.
Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene alisema watachukua hatua zaidi iwapo mashine za Biometric Voters Registration (BVR) zitabainika kuwa na kasoro katika uboreshaji huo.
Uandikishaji wa Watanzania milioni 26 wenye sifa ya kupiga kura ulitakiwa kuanza mwezi huu lakini NEC ilibadilisha ikisema inasubiri mashine 7,750 kwa ajili ya kazi hiyo.
Makene alisema muda uliobaki kwa ajili ya kazi hiyo hautoshi ndiyo maana wameamua kuitisha kikao cha dharura ili wafanye uamuzi.
Hivi karibuni, Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba alisema hana uhakika iwapo NEC itamaliza kazi hiyo kwa wakati na elimu ya Kura ya Maoni kutolewa kabla ya upigaji kura.
Sheria Namba Tatu ya mwaka 2014 kuhusu Kura ya Maoni inaweka utaratibu wa kutoa miezi miwili ya elimu na mmoja wa kampeni kabla ya kupiga kura ya maoni itakayofanyika nchini kote Aprili 30 mwaka huu.

Mwigulu atii agizo la Kinana, asitisha ziara zake mikoani

Naibu Katibu Mkuu wa CCM bara

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesitisha ziara zake za mikoani ili kutii agizo alilopewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana.

Nchemba ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, alisema jana kuwa anawajibika kutekeleza amri hiyo kutoka ndani ya chama.

Alisema agizo hilo halina lengo baya zaidi ya kukijenga chama ili kufikia malengo ikiwa ni pamoja na kuimarisha nidhamu miongoni mwa wanachama.

“Huwa ananituma, anaweza akaniambia nifanye au nisifanye jambo ambalo halina masilahi ya chama,” alisema Nchemba.

Utekelezaji huo umekuja baada ya Nchemba kuandikiwa barua na Kinana ambayo pia imezagaa katika mitandao ya kijamii ikimtaka kusitisha ziara anazozifanya maeneo mbalimbali kwa kuwa hazina baraka za chama hicho.

Katika barua hiyo iliyoandikwa Januari 18, ilieleza Nchemba amekuwa akifanya ziara nyingi katika mikoa na wilaya bila ya ushirikishwaji wa makao makuu, mikoa na wilaya na hasa kamati za siasa.

Kituo kingine cha Polisi kuvamiwa na Majambazi Tanzania

Polisi Ikwiriri
Msemaji wa Jeshi la Polisi Bi Advera Bulimba
Askari wawili wa kituo cha Ikwiriri wilayani Rufiji mkoani Pwani wameuawa na majambazi ambao idadi yao haijafahamika ambao baada ya kufanya mauaji walipora bunduki tano, risasi 60 na mabomu mawili ya machozi ndani ya kituo cha Polisi.

Walikuwa ni majambazi wengi, walivamia na kuanza kuwashambulia askari wetu, walifanikiwa kuwaua askari wetu wawili na kuchukua silaha… Polisi imelaani tukio hilo, msako mkali umeanza na milioni 20 itatolewa kwa atakaefanikisha Majambazi hawa kukamatwa“– Advera Bulimba, msemaji wa Jeshi la Polisi akiongea on ITV

Majambazi hawa walivamia wakiwa na silaha za moto, mabomu ya kurusha kwa mkono na mapanga ambapo hili linakuwa tukio jingine kulisikia baada ya lile la Majambazi kufanya vivyo hivyo kwa kituo cha Polisi Geita.

Mazungumzo ya kutafuta amani Sudan kusini yafanyika mkoani Arusha


Rais Jakaya Kikwete  wa pili kutoka kulia akiwa kwenye mazungumzo ya kutafuta Aman
Mazungumzo ya kutafuta amani SUDAN KUSINI yanaendelea mkoani ARUSHA.
 Habari za hivi karibuni kutoka Arusha zinasema mazungumzo hayo ambayo yanafanyika kwa faragha  
yanahudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Rais JAKAYA KIKWETE, Rais UHURU KENYATTA wa KENYA, YOWERI MUSEVENI wa UGANDA na SALVA KIIR wa SUDAN KUSINI.
Hatua inayosubiriwa katika mazungumzo hayo ni kutiwa saini kwa makubalino ya amani kumaliza mgogoro baina ya vikundi vinavyopingana ndani ya chama tawala nchini SUDAN KUSINI cha SPLM.

Mazungumzo ya upatanishi kati ya vikundi hivyo yamekuwa yakifanyika chini ya uratibu wa Chama Cha Mapinduzi - CCM yakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM mstaafu JOHN MALECELA tangu mwezi Oktoba mwaka jana.

SUDAN KUSINI ilipata uhuru wake kutoka SUDAN mwaka 2011 ambapo hata hivyo mwishoni mwa mwaka 2013 iliingia katika mgogoro kufuatia jaribio la kuipindua serikali ya Rais SALVA KIIR.

Mwezi Novemba mwaka jana kundi la usuluhishi linaloundwa na nchi za KENYA, UGANDA, SUDANI pamoja na ETHIOPIA walisaini makubaliano ya suluhu lakini bado mapigano yaliendelea katika nchi ya SUDAN KUSINI.

Viongozi wengine wanaohudhuria mazungumzo hayo ni pamoja na Makamu wa Rais Dkt MOHAMED GHARIB BILAL, Makamu wa Rais wa AFRIKA KUSINI CYRIL RAMAPHOSA na Dk RIEK MACHAR aliyekuwa Makamu wa Rais wa SUDAN KUSINI.

GRACA MACHEL azitaka NGO nchini kuandaa programu za kuelimisha jamii

GRACA MACHEL
Mke wa Rais wa zamani wa AFRIKA KUSINI Hayati NELSON MANDELA, GRACA MACHEL amewataka wataalam wa masuala ya jinsia na Taasisi za taaluma za maendeleo nchini kutafiti na kuandaa program za kuelimisha jamii kuhusu unyanyasaji wa kijinsia.

GRACA MACHEL ameyasema hayo jijini DSM katika majadiliano maalum ya kuhusu masuala ya jinsia ikiwa ni sehemu ya ziara yake hapa nchini ambapo amesisitiza kuwa jamii inawajibika kupambana na unyanyasaji katika jamii.

Mke huyo wa Raisi wa zamani wa afrika ya kusini Hayati NELSON MANDELA, GRACA MACHEL anafanya ziara katika Chuo Kikuu cha DSM na kuhamasisha yafanyike mapambano ya kisomi dhidi unyanyasaji wa kijinsia.

Kwa upande wao wadau mbalimbali walioudhuria kwenye majadiliano hayo wameeleza kuwa ili kupambana na matukio ya unyanyasaji wa kijinsia ni muhimu kuwashirikisha wanaume na kuepukana na tamaduni zilizopitwa na wakati.

Vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vimekuwa vikipigwa vita duniani kutokana na mila na desturi zilizopitwa na wakati kuendelea licha ya juhudi za taasisi mbali mbali za kupambana na vitendo hivyo

Mkoa wa KIGOMA watakiwa kumaliza mgogoro wa Ranchi ya UVINZA

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt TITUS KAMANI

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt TITUS KAMANI ameuagiza uongozi wa mkoa wa KIGOMA kuhakikisha mgogoro wa mpaka kati ya Ranchi ya Uvinza na pori la Akiba la Moyowosi unakwisha mara moja na ametaka pia uonevu unaofanywa dhidi ya wawekezaji wa mifugo katika ranchi ya Uvinza ukome mara moja.

Waziri KAMANI ametoa agizo hilo kufuatia malalamiko ya wawekezaji wa mifugo waliopewa vitalu katika RANCHI ya Uvinza kuwa wamekuwa wakichomewa mazizi ya mifugo yao, nyumba za watumishi , kuporwa mifugo yao kupigwa na kulazimishwa kutoa fedha na baadhi ya watumishi wa kampuni iliyopewa kitalu cha kuwinda katika pori la Akiba la MOYOWOSI wilayani KASULU

Bangi halali kwa matibabu Jamaica

Mswada wa kuhalalisha uvutaji wa Bangi utaidhinshwa na baraza la Senate wiki ijayo

Baraza la mawaziri la Jamaica, limeidhinisha mswada ambao unahalalisha watu kumiliki kiwango kidogo cha Marijuana.

Ina maana kwamba hii ni mara ya kwanza kwa jamii ya 'Warastafarian' wanaotumia Bangi kwa sababu za kidini kuweza kuivuta hadharani bila ya kupatikana na hatia. 

Mswada huo,pia unatawezesha kuwepo halmashauri itakayokua ikitoa leseni za kupandwa , kuuzwa na kusambazwa kwa Marijuana kwa sababu za kimatibabu.

Lakini uvutaji wa Bangi katika maeneo ya umma haitaruhusiwa. Mswada huo huenda ukaidhinishwa na baraza la Senate wiki ijayo.

Serikali yakana kuwaua waandamanaji DRC

Serikali inasema kwamba walinzi wa maduka binafsi ndio waliowaua waandamanaji

Serikali ya jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekanusha madai ya kuwauwa waandamanaji waliokuwa wakiandamana kupinga mapendekezo ya kubadilisha sheria za uchaguzi mkuu.

Makundi ya kutetea haki za binadamu, yanasema kuwa zaidi ya watu arubaini wameuawa katika siku tatu za ghasia.

Waziri wa mawasiliano Lambert Mende, aliambia BBC kwamba polisi hawakutumia silaha zozote dhidi ya waandamanaji hao.

Alisema waandamanaji ambao aoliwataja kama waporaji, waliuawa na walinzi waliokuwa wanalinda majengo ya biashara yaliyoporwa
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema kwamba zaidi ya watu 40 wameuawa katika siku tatu za vurugu mjini Kinshasa.

Mabadiliko yaliyopendekezwa huenda yakachelewesha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao, wakati Kabila anatarajiwa kung'atuka baada ya kuitawala nchini huo kwa miaka 14.

Wednesday, 21 January 2015

Muasi Dominic Ongwen afikishwa Hague