Sunday, 1 March 2015

Wananchi wa LESOTHO wapiga kura

Wananchi wa LESOTHO wapiga kura
Wananchi wa LESOTHO wamepiga kura kuchagua viongozi wapya wa nchi hiyo ya kifalme. Watu milioni MOJA na LAKI MBILI wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi huo uliohusishavyama 24 vilivyosimamisha wagombea. 

Uchaguzi mkuu ulikuwa umepangwa kufanyika mwaka 2017, lakini tarehe ilibadilishwa baada ya kutokea jaribio la kuipindua serikali miezi sita iliyopita. 

Mwaka jana waziri mkuu wa nchi hiyo THOMAS THABANE alikimbilia nchi jirani ya AFRIKA KUSINI baada askari kuteke makao makuu ya polisi na kuizingira Ikulu ya nchi hiyo. 

THABANE anamshutumu naibu wake MOTHETJOA METSING kwa kupanga njama za kumwondoa madarakani madai ambayo Metsing ameyakanusha. 

Matokeo ya awali ya uchaguzi yanatarajiwa kesho na matokeo kamili yatatolewa Alhamisi ijayo.

0 comments:

Post a Comment