This is default featured post 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Tuesday, 27 October 2015

MBATIA AMLAZA CHALI MZEE ELYIATONGA MREMA JIMBO LA VUNJO


Mbunge mteule wa jimbo la vinjo Mh. JAMES MBATIA
Tume ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza James Mbatia wa NCCR Mageuzi kuwa mbunge mteule wa jimbo la Vunjo huku kada wa Chadema, Anthony Komu naye akiibuka mshindi katika jimbo la Moshi Vijijini lililokuwa linaongozwa na Waziri wa zamani wa Biashara na Viwanda, Dk. Cyril Chami kupitia CCM.

Akitangaza matokeo ya majimbo hayo mawili mkoani Kilimanjaro kuamkia leo, msimamizi Fulgence Mponji, amesema Mbatia amepata kura 60,187 akiwashinda wapinzani wake; Innocent Shirima wa CCM aliyepata kura 16,617 na Augustine Mrema wa TLP aliyepata kura 6,416.

Kutokana na matokeo hayo,  Mrema ameshindwa kutetea kiti chake cha ubunge katika jimbo la Vunjo huku wananchi wa eneo hilo wakiendeleza historia ya kutomchagua mbunge wa chama kimoja kwa vipindi viwili tangu kurudi kwa mfumo wa siasa za vyama vingi.

Kwa upande mwingine, CCM imepoteza jimbo la Moshi Vijijini kupitia kwa mgombea Cyril Chami na kurudi tena upinzani baada ya kada wa Chadema, Anthony Komu kutangazwa mshindi. Hata hivyo, waziri huyo wa zamani wa Viwanda na Biashara hakuwepo wakati NEC wa kusaini kuonyesha kuwa amekubali matokeo.

Kwa mujibu wa Mponji, mbunge mteule wa Moshi Vijijini, Komu amepata kura 55,813 huku Dk Cyril Chami akijikusanyia kura kura 24,415.

MAWAZIRI WA JK WLIOANGUKA KWENYE NAFASI YA UBUNGE MWAKA HUU 2015



Mawaziri watano wa Serikali inayomaliza muda wake wameanguka kwenye uchaguzi majimboni mwao, sambamba na wagombea wengine maarufu wa Bunge lililopita baada ya matokeo ya kura zilizopigwa Jumapili kuanza kutangazwa jana.

Mawaziri hao wanaungana na wabunge wengine maarufu wa Bunge la Kumi walioshindwa kutetea majimbo yao, wakiwamo wa kambi ya upinzani ambao wameangushwa na wagombea wa CCM.

Pia wamo mawaziri wa zamani wawili, Cyril Chami na Omary Nundu walioanguka kwenye uchaguzi, kwa mujibu wa matokeo ambayo yanaendelea kutangazwa.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema jana kuwa itakamilisha kazi ya kutangaza matokeo yote keshokutwa.

Mawaziri walioanguka kwenye uchaguzi huo ni Steven Wasira, Christopher Chiza, Aggrey Mwanri, Dk Steven Kebwe na Anne Kilango.

Katika matokeo yaliyotangazwa jana, Wasira, kada maarufu na mwanasiasa mkongwe aliyekuwa akitetea Jimbo la Bunda, alijikuta akiangushwa na mwanasiasa kijana, Ester Bulaya, ambaye alihamia Chadema baada ya Bunge la Kumi kumaliza muda wake.

Wasira, ambaye alikuwa Waziri wa Kilimo na Chakula, alianza mchakato wa uchaguzi mwaka huu kwa kuomba ridhaa ya CCM agombea urais, lakini hakupitishwa. Bulaya, ambaye alikuwa mbunge wa viti maalum (CCM), alipata kura 28, 508 na kumuacha mbali waziri huyo mkongwe aliyepata kura 19, 126.

Mwingine aliyeanguka ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwezeshaji na Uwekezaji, Christopher Chiza ambaye ameangushwa na Bilago Samson wa Chadema katika Jimbo la Buyungu. Waziri huyo alizidiwa kwa kura 104 baada ya Samson kupata kura 23,041 dhidi ya 22,934 za Chiza.

Lakini hali haikuwa hivyo kwa Naibu Waziri wa Tamisemi, Aggrey Mwanri kwenye Jimbo la Siha. Waziri huyo alizidiwa kwa zaidi ya kura 4,100 na mpinzani wake kutoka Chadema, Dk Godwin Mollel aliyepata kura 22,746.

Katika Jimbo la Serengeti, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe pia alijikuta akipoteza nafasi ya kurudi bungeni kwa kura alipoangushwa na Marwa Ryoba wa Chadema. Dk Kebwe alipata kura 39,232, akiwa amezidiwa na mpinzani wake kwa zaidi ya kura 820.

Anne Kilango, ambaye aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Elimu mwaka 2013 baada ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyosababishwa na kashfa ya Operesheni Tokomeza, ameangushwa na mgombea wa Chadema, Naghenjwa Kaboyoko wa Chadema kwa tofauti ya kura 3,297.

Kilango alipata kura 15,539 wakati mgombea huyo wa Chadema alipata kura 18,836. Pia wabunge maarufu kama Vincent Nyerere (Musoma Mjini), James Lembeli (Kahama Mjini) na Kyisieri Chambiri (Babati Mjini) wameangushwa.

Nyerere, aliyekuwa akitetea kiti cha Musoma Mjini kwa tiketi ya Chadema, aliachwa mbali na mgombea wa CCM, Vedastus Mathayo aliyepata kura 32, 836 dhidi ya 25,549.43 za Nyerere.

Lembeli, ambaye alihamia Chadema muda mfupi baada ya Bunge la Kumi kumaliza muda wake, aliachwa mbali na mfanyabiashara maarufu, Jumanne Kishimba aliyepata kura 47,553 dhidi ya kura 30,122 za Lembeli.

Wednesday, 21 October 2015

mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini Jenerali davis mwamunyange aonekana


Jenerali Davis Mwamunyange
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange, (pichani) aonekana katika Kamandi ya Anga Kizuka iliyopo Ngerengere, mkoani Morogoro wakati Rais Jakaya Kikwete, akizindua uwanja wa Ndege wa Kamandi hiyo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Rais Kikwete alisema kuwa katika miaka 10 ya uongozi wake, amefanya mambo mengi kwa Watanzania pamoja na kuliacha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) likiwa katika hali nzuri ya kiutendaji.

Alisema hakuna nchi inayoweza kupata maendeleo mbalimbali kama haina jeshi imara kutokana na kuwapo vitendea kazi vya kutosha na madhubuti vinavyoimarisha jeshi hilo.


Jenerali Mwamunyange alisema katika kipindi chote cha uongozi wa Rais Kikwete, ameimarisha JWTZ na kutimiza mahitaji ya jeshi hilo.


Alisema pamoja na changamoto ndogo zilizobaki, lakini anaamini serikali ijayo itazifanyia kazi na kuendeleza pale alipoishia ili kuwa na jeshi imara.

Tuesday, 20 October 2015

zikiwa zimebaki siku 5 kuelekea uchaguzi mkuu, huyu hapa kigogo mwingine wa ccm kutimkia ukawa

Dkt. Eve Sinare akihojiwa na Waandishi wa Habari

Wimbi la kujivua uanachama lazidi kuitafuna CCM, mwanachama mwingine muhimu aliyefanikisha mipango ya Ushindi wa Rais Jakaya Kikwete kuingia madarakani amehama CCM na kujiunga UKAWA.

Zikiwa zimebaki siku 5 kabla ya Oktoba 25, siku ambayo watanzania wataandika historia ya kuiweka madarakani serikali mpya ya awamu ya Tano, kada mwingine Mkongwe wa Chama hicho, ametangaza rasmi kujiweka kando.

Dkt. Eve Sinare, ambaye ni wakili wa kujitegemea aliyekuwa sehemu ya harakati za CCM,  alitangaza jana kukihama chama hicho akidai kuwa kimepoteza sifa za utawala bora na kimeshindwa kuwahudumiwa wananchi kwa kuwapa elimu bora iliyotarajiwa.

Dkt. Eve Sinare aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA). Pia, ni Mwenyekiti Mtendaji wa Rex Attoneys na aliwahi kuteuliwa kuwa mmoja kati ya wajumbe wa Bodi ya Huduma ya Dunia iliyoko Texas inayofahamika kwa jina la World Services Group (WSG).

Hata hivyo, kama alivyosema Balozi Juma Mwapachu wakati anahama chama hicho, Dkt. Eve Sinare ameeleza kuwa hatajiunga na chama chochote cha siasa.

JK akumbushwa kutangaza mali alizochuma kabla ya kung'atuka.


Rais wa Tanzania
Mkurugenzi wa Idara ya Utetezi na Maboresho kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia, amemkumbusha Rais Jakaya Kikwete, asiondoke kimyakimya bila kutangaza au kuorodhesha mali alizochuma wakati akiwa madarakani.

“Rais Kikwete alijaza fomu ya mali alizokuwa nazo Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, lakini hakutangaza. Tunasubiri kuona sasa baada ya kumaliza atatangaza mali aliyopata akiwa madarakani,” alisema.


Alisema mwaka 1995, Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, alipoingia madarakani alitangaza mali zake, lakini alipong’atuka, ‘alisahau’ kutangaza, pengine ni kutokana na majukumu aliyokuwa nayo kitaifa sasa tunasubiri kuona kwa Rais Kikwete,” alisema.  


Kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13, 1995 na kanuni zake, mwananchi anaweza kupata taarifa za mali za viongozi kwa kufuata utaratibu uliopo, lakini baada ya kupata taarifa hizo, haruhusiwi kuzitangaza au kuzichapisha kwenye vyombo vya habari. 

Chanzo TUBONGE TZ

Chadema yamshtaki Kikwete UN.



Rais wa Tanzania
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema tayari kimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki Moon, kumshtaki Rais Jakaya Kikwete.

Mwanasheria wa Chadema, John Mallya, aliwaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwa barua hiyo waliituma UN jana.


Mallya alisema lengo la barua ni kumshtaki Rais Kikwete kwa mataifa mengine kutokana na kauli yake ya kuwatisha Watanzania  aliyodai aliitoa Oktoba 14, mwaka huu ya kuwataka wapigakura kuondoka kituoni baada ya kupiga kura na endapo watakiuka watashughulikiwa.


Mallya alisema kauli ya Rais Kikwete ni kinyume cha Sheria ya Uchaguzi inayomtaka mpigakura kukaa mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura.


“Kwa sababu Rais Kikwete hatuwezi kumshtaki kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, ziko mamlaka ambazo tunatumia kumshtaki kama tulivyofanya kuiandikia barua UN na kupeleka nakala Jumuiya ya Madola, Umoja wa Afrika, Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai na kusainiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari,” alisema Mallya.


Chanzo... TUBONGE TZ

Daktari bandia awaambukiza Ukimwi watu 100


Mwanaume mmoja aliyejidai kuwa daktari na kuwaambukiza watu zaidi ya mia moja virusi amefikishwa mahakamani nchini Cambodia. Yamkini daktari huyo bandia alikuwa akiwadunga wagonjwa wake kwa sindano aliyokuwa ameitumia kwa mgonjwa aliyekuwa na virusi vya Ukimwi.

Yem Chhrin anakabiliwa na kosa la kuua na kuambukiza watu ugonjwa huo kwa kukusudia. Aidha Bw Yem anashtakiwa kwa kuwalaghai watu kuwa ni daktari ilhali hana vyeti halali vya kuhudumia umma. Iwapo atapatikana na hatia mahakama ya nchi hiyo huenda ikamhukumu kifungo cha maisha jela.

Waathiriwa walioambukizwa maradhi ya Ukimwi wanatokea katika kijiji cha Roka kilichoko Kaskazini Magharibi. Mmoja wao ni kiongozi wa kidini wa madhehebu ya Buddha na mtoto wa miaka mitatu.

Takriban 10 kati ya waathiriwa hao wanakisiwa kuwa wameshakata roho. Kwa mujibu wa ripoti za mahakama daktari huyo bandia amekiri kuhudumu bila vyeti maalum ila anakana kukusudia kuwaambukiza watu hao 100 virusi vinavyosababisha maradhi ya Ukimwi.

Monday, 19 October 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MRADI WA VITUO VYA MAPUMZIKO NA VYOO VYA WASAFIRI KATIKA BARABARA KUU NCHINI, KATIKA KIJIJI CHA IDETERO, MUFINDI-IRINGA.

 

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi wa Kijiji cha Idetero Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa, wakati wa hafla ya uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mradi wa Vituo vya Mapumziko na Vyoo vya Wasafiri katika Barabara Kuu nchini, juzi Okt 17, 2015.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mgimwa, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais Dkt. Bilal, kuhutubia wananchi wa Kijiji cha Idetero Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa, wakati wa hafla ya uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mradi wa Vituo vya Mapumziko na Vyoo vya Wasafiri katika Barabara Kuu nchini, juzi Okt 17, 2015.
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuweka Jiwe la Msingi la wa Mradi wa Vituo vya Mapumziko na Vyoo vya Wasafiri katika Barabara Kuu nchini, wakati wa hafla ya kuweka jiwe la Msingi iliyofanyika katika Kijiji cha Idetero Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa juzi Okt. 17, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo ya ujenzi huo kutoka kwa msimamizi wa Ujenzi, Stanley Ndosite Nzowa, wakati wa hafla ya uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mradi wa Vituo vya Mapumziko na Vyoo vya Wasafiri katika Barabara Kuu nchini, juzi Okt 17, 2015.