This is default featured post 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Thursday, 2 July 2015

Ugiriki yaonywa kuhusu kura ya 'La'


Raia wa Ugiriki
Raia wamegawanyika huku wengi wakianza kuhamia kambi ya 'Ndio'

Ugiriki imeonywa dhidi ya kupiga kura ya 'La' wakati wa kura ya maoni hapo Jumapili kwa sababu haitasaidia kutatua matatizo ya kiuchumi yanayokumba taifa hilo.

Hofu ya Ebola DRC



Mgonjwa wa Ebola DRC 
Watu wanne wamefariki dunia wakiwa na dalili za ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Boko Haram yashambulia zaidi

Boko haram wazidisha mashambulizi
Watu 150 wameuawa baada ya Boko Haram kuvamia kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Walioshuhudia mashambulizi hayo wanasema watu tisini na saba wameuawa siku ya Jumatano katika kijiji cha Kukawa kilichopo karibu na Ziwa Chad.

Habari zinasema pia wanaume 48 wamepigwa risasi na wapiganaji katika mashambulizi tofauti siku ya Jumanne.

Mashuhuda wanaokimbia eneo lililopo karibu na Ziwa Chad wanasema idadi kubwa ya wapiganaji wamevamia vijiji vitatu ambapo wameuwa wanaume, wanawake na watoto.

Baadhi ya ripoti zinasema walipigwa risasi huku wengine wakielezea jinsi wapiganaji hao walivyowachinja watu na kuchoma majengo.

Upande wa Kusini, nje kidogo na mji wa Monguno, kundi la wapiganaji wa Boko Haram wamefika usiku wakati watu walipokuwa wanaswali. Waliwasubiri mpaka walipomaliza kuswali na kuwatenganisha wanaume na wanawake na baadae kuanza kuwamiminia risasi wanaume.

Mwanasiasa anayewakilisha eneo hilo, Mohammed Tahir amesema awali alitoa tahadhari kwa jeshi la Nigeria kwamba vijiji hivyo viko hatarini kwa sababu Boko Haram wameweka makazi katika maeneo hayo baada ya kutimuliwa katika himaya yao ya msitu wa Sambisa. 

Haya ni mashambulizi mabaya zaidi kufanywa na Boko Haram katika kipindi cha wiki kadhaa.
Kundi hilo limekuwa likilipuwa mabomu kadhaa baada ya kudhoofishwa na majeshi ya Nigeria.

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari amesema kipaumbele chake ni kuimarisha mapambano dhidi ya Boko Haram.

Msumbiji yakubali mapenzi ya jinsia moja

Wapenzi wa Jinsia moja
Nchi chache Afrika zimekubali mapenzi ya jinsia moja
Msumbiji imehalalisha mapenzi ya jinsia moja,na kuwa moja wapo wa nchi chache Afrika zinazohalalisha mapenzi ya jinsia moja.

Sheria hiyo iliyowekwa na wakoloni wa nchi hiyo Ureno iliondolewa na bunge la nchi.Watetezi wa haki za wapenzi wa jinsia moja,wametaja hatua hiyo kama ushindi mkubwa.

Hata hivyo nchi nyingi za Afrika zimeweka sheria kali dhidi ya mapenzi ya jinsia moja.Nigeria ilipiga marufuku na kuweka adhabu ya kifungo cha miaka 14 jela kwa wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.Uganda nayo imeapa kurejesha sheria kali kuharamisha mapenzi ya jinsia moja.

Sheria ya awali ilitupiliwa nje na mahakama ya kikatiba.

Msumbiji sasa anajiunga na mataifa mengine ikiwa ni pamoja na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ivory Coast na Afrika Kusini ambapo siyo hatia kuwa mpenzi wa jinsia moja.

Vikwazo kwa makamanda wa S Sudan


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limewawekea vikwazo ikiwemo marufuku ya usafiri na kupiga tanji mali za majenerali sita wa Sudan Kusini.
Watatu ni kutoka upande wa serikali na wengine watatu ni kutoka upande wa waasi.
Wapiganaji Sudan Kusini
Watoto wengi wamelazimishwa kuwa wapiganaji Sudan Kusini

BREAKING NEWS-Bunge Laharishwa gafla baada ya Wabunge wa UKAWA kugomea Miswada Petroli na Gesi

 
wanachokiita wanaburuzwa, Wabunge wa UKAWA kwa pamoja wamegoma kuendelea na bunge na wote kuamua kusimama baada ya kupinga uwasilishaji wa dharula wa Miswada mitatu muhimu ya Gesi, Petroli na Uziduaji "Extractive Industries". 

Ni baada ya John Mnyika kuomba Muongozo juu ya uvunjaji wa kanuni za bunge. shuguli za leo zimekiuka kanuni kwani miswada imewekwa ikiwa sambamba. anasema hoja ikishatolewa ni lazima ijadiliwe iamuliwe ndo itolewe hoja nyingine, lakini leo zipo hoja tatu kwa pamoja.



Mnyika kasema na huu Muongozo sitaki useme utautolea ufafanuzi siku nyingine kwa maana hatuwezi kuendelea kufanya kazi ambazo zimevunja kanuni.

Wanapinga kuwasilishwa kwa dharula na kwa pamoja Miswada yenye manufaa makubwa kwa nchi.

Miswada wanayo pinga na iliyo wasilishwa kwa pamoja ni;

1.Muswada juu ya Petroli, 2015 (The Petroleum Act, 2015):

2.Muswada juu ya Usimamizi wa Mafuta na Gesi, 2015 (The Oil and Gas Revenues Management Act, 2015):

3.Muswada juu ya tasnia ya Uziduaji Tanzania (The Tanzania Extractive Industries Act, 2015): The Tanzania Extractive Industries Act, 2015.

Hata baada ya Spika kuwataka watoke nje kama hawataki kuendelea, Wamegoma na kusimama na kuanza kupiga kelele hadi Spika akaahirisha bunge. UKAWA wamesema mwanaharamu hapiti leo
.

Chadema yaibwaga CCM mahakamani

Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara imezidi kupata pigo baada ya Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi wa wenyeviti wa vitongoji 16 vya mji mdogo wa Mirerani, kwa maelezo kuwa ulikiuka sheria na utaratibu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Hii ni mara ya pili katika kipindi cha mwezi mmoja kwa Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi huo ambao uliwaweka madarakani makada wa CCM.

Awali, Mei 30 Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kiteto ilitengua matokeo ya uchaguzi wa mwenyekiti wa Kijiji cha Lobosireti kwa kukiuka sheria na utaratibu.

Chadema ilifungua kesi kadhaa mahakamani hapo kupinga kitendo cha wagombea wa CCM kupewa ushindi bila kufanya uchaguzi Desemba 14, mwaka jana.

Hukumu hiyo ya jana, inatokana na kesi zilizofunguliwa na Chadema wilayani Simanjiro kwenye kata za Endiamtu na Mirerani, wakipinga wagombea wa CCM kupewa ushindi bila kupigiwa kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Desemba 14 mwaka jana.

Hakimu Mkazi Mfawidhi mahakama hiyo, Elimo Massawe aliagiza kurudiwa kwa uchaguzi wa viongozi wa vitongoji vya Zaire, Kisimani, Tenki la Maji, Endiamtu, Kairo na Kazamoyo vilivyoko Kata ya Ediamtu.

Hakimu Massawe alitaja vitongoji vingine kuwa ni Sekondari, Kilimahewa, Tanesco, Kazamoyo Juu, Mji mpya, Tupendane na vitongoji vya Kata ya Mirerani ambavyo ni Kangaroo, Songambele A, Getini na Songambele B.

Katika kesi hiyo, Chadema iliwakilishwa na mawakili James Millya, Shadrack Kimomogoro na Daudi Haraka na Mahakama iliamuru walipwe Sh160 milioni za gharama za kesi hiyo ambayo ilichukua takribani miezi sita hadi kutolewa hukumu.

Katibu Mwenezi wa Chadema mkoani Manyara, Ambrose Ndege alisema Mahakama imetenda haki kwa kutoa hukumu sahihi na wanajipanga ipasavyo kuhakikisha watashinda vitongoji vyote pindi uchaguzi huo utakaporudiwa.

“Tuliwaeleza tangu awali kuwa uchaguzi ukifanyika tutawashinda saa nne asubuhi hivyo tunawasubiri uwanjani na tutaongoza Mamlaka ya Mji wa Mirerani kwani wananchi wanatukubali,” alisema Ndege.

Hata hivyo, Katibu Mwenezi wa CCM wa Kata ya Endiamtu, Mashaka Jeroro alisema wanatarajia kukata rufaa kupinga hukumu hiyo akisema wagombea wa Chadema walikosea kujaza fomu ndiyo sababu wakawekewa pingamizi.

Upinzani wambana Dk Migiro, AG bungeni


Waziri Kivuli wa Sheria (Chadema), Tundu Lissu akichangia  muswada wa Kuwalinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi wa mwaka 2015 bungeni mjini Dodoma jana. 
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha Rose Migiro, jana alibanwa bungeni baada ya wabunge wa upinzani kuhoji juu ya Muswada wa Sheria ya Kulinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi wa mwaka 2015 wakieleza umewahishwa bila sababu yoyote.

Dk Migiro alikutana na kimbuga cha upinzani ikiwa ni siku moja baada ya Bunge la 10 kuigomea Serikali ilipotaka kuingiza bungeni miswada mitatu iliyohusu Wizara ya Nishati na Madini wakisema inahitaji muda mzuri.

Mapema jana, Dk Migiro aliwasilisha ndani ya Bunge muswada huo akilitaka lijadili na kuupitisha ili kutoa nafasi ya kuwalinda watu wa aina hiyo.

Akiwasilisha maoni ya upinzani bungeni, msemaji wa kambi hiyo katika Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu alisema muswada huo hauna tija kwa muda huo kwani unatoa nafasi finyu kwa wabunge kujadili jambo ambalo ni muhimu zaidi kwa wananchi.

Lissu ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), alisema uharaka wa muswada huo ni kiashiria tosha kwamba Serikali inataka kuminya uhuru wa wabunge kupitia kwa kina sheria hiyo.

“Kanuni zinasema kuwa, sheria inaweza kupitishwa kwa hati ya dharura ikiwa tu kuna mambo ambayo yanataka kutokea ambayo ni pamoja na majanga au vita. Je, kuna uharaka kiasi gani wa kupitisha muswada huu?” alihoji Lissu.

Mbunge huyo mbali na kutoa ufafanuzi katika vifungu vingi katika muswada huo, lakini alisisitiza kuwa ukipitishwa utakuwa umewanyima haki watu wa kada ya chini na kuwapa mwanya viongozi wao.

Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika alipinga vikali muswada huo pamoja na namna ulivyowasilishwa na akazua mgogoro mkubwa baina yake na Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG), George Masaju.

Malumbano ya wawili hao yalianzia pale Mnyika aliposema kuwa Serikali ni dhaifu katika suala zima la utungaji wa sheria jambo ambalo pia liliamsha hasira za Spika. 
Katika hoja zake, Mnyika alipinga jinsi muswada ulivyokuwa ukitoa upenyo kwa watu kutoa taarifa kwa wakubwa wao badala ya kuzipeleka kwa vyombo vingine.

“Mfano, muswada unaelekeza mtu kutoa taarifa kwa kiongozi wake yaani akiwa mfanyakazi wa benki kuu anawezaje kutoa taarifa za ufisadi wa gavana kwa gavana mwenyewe?” alihoji Mnyika.

AG Masaju alipinga kauli za kuwa Serikali inafanya vitu dhaifu akisema siyo nia yao, bali wanafanya kazi ya kupeleka miswada ili wabunge wenyewe ndiyo wafanye uamuzi.

Ukawa: NEC inatuvurugia mipango majimboni

Mwenyekiti mwenza UKAWA, Mh. Freeman Mbowe
Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ameishukia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kushindwa kutangaza mgawanyo wa majimbo, akisema kuchelewa huko kunavuruga mipango yao.

Ukawa, inayoundwa na vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, imekubaliana kusimamisha mgombea mmoja kuanzia ngazi ya urais hadi diwani na viongozi wa vyama hivyo wameshakutana mara kadhaa kuzungumzia kugawana majimbo kulingana na nguvu ya chama kwenye eneo husika.

Hata hivyo, vimeshindwa kumalizia kazi hiyo kutokana na kutokamilika kwa mgawanyo wa majimbo kama NEC ilivyoahidi Mei 12 kuwa majimbo mapya kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 yangetangazwa Juni 30.

Akizungumza jana, Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema aliitupia lawama NEC akisema wakati huu ilitakiwa kuwa imeshamaliza suala la majimbo na kushughulikia mambo mengine.

“Tunataka kutengeneza ratiba ya mpango kazi, lakini tunashindwa. Tunataka tujue majimbo mapya ili twende huko, lakini sasa tunashindwa na muda unakwenda,” alisema Mbowe.

Akizungumzia ukimya wa kutangaza majimbo hayo licha ya kusema ingefanya hivyo Juni mwishoni, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alisema hadi sasa Tume hiyo haijakamilisha ugawaji wa majimbo lakini bado wanaendelea na mchakato huo.

Alisema Tume yake imeamua kugawa majimbo hayo kwa kuzingatia vigezo mbalimbali, ikiwamo idadi ya watu, upatikanaji  wa mawasiliano, hali ya kijiografia na kanuni za uchaguzi wa Rais na wabunge za mwaka 2010.

Jaji Lubuva pia alisema Tume itayagawa majimbo hayo kwa kuzingatia uwepo wa miundombinu bora, hali ya kiuchumi kwa kuweka uwiano kati ya eneo moja na jingine, mawasiliano ya simu na vyombo vya habari kwa ajili ya kupata mwakilishi atakayeharakisha maendeleo katika eneo husika.

Wakati ikisuasua kutangaza majimbo mapya ya uchaguzi, NEC pia inakabiliwa na kibarua kingine cha kumalizia uandikishaji wapigakura kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura.

Kazi hiyo imekumbwa na matatizo kadhaa na inatakiwa ikamilishwe katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, lakini imeahirishwa kutokana na kuchelewa kwa mashine zinazotumika za teknolojia ya mfumo wa kuchukua alama na taswira za mpigakura (Biometric Voters Registration).

Jaji Lubuva alisema kuwa kuna baadhi ya majimbo ambayo ni makubwa, jambo ambalo alisema linatokana na ongezeko la watu nchini.
Ugawaji wa majimbo unatakiwa kufanyika mara kwa mara au angalau mara moja baada ya miaka 10

Uingereza yataka kukabili kitisho cha IS

Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Michael Fallon
                                    
Wabunge nchini Uingereza wametakiwa kufikiria kuiruhusu Uingereza kushambulia maeneo ya wapiganaji wa Kiislam wa Islamic State nchini Syria, anasema waziri wa ulinzi wa Uingereza, Michael Fallon.

Jeshi la Uingereza,RAF limekuwa likifanya mashambulio nchini Iraq tangu mwezi Septemba lakini Bwana Michael Fallon anatarajiwa kuliambia bunge kuangalia uwezekano wa kupeleka pia majeshi yake nchini Syria.

Bwana Fallon anasema hakuna kikwazo kisheria lakini amewahakikishia wabunge kwamba hakuna uamuzi utakaochukuliwa bila ruhusa yao.

Katika hotuba yake Bwana Fallon atazungumzia mashambulio ya kigaidi, kama mauaji ya Tunisia, huenda yalipangwa na wapiganaji wa IS nchini Syria.

Watalii 29 kati ya 38 waliouawa katika pwani ya Sousse nchini Tunisia tarehe 26 Juni wamethibitika kuwa raia wa Uingereza.Mwanafunzi Seifeddine Rezgui, mwenye umri wa miaka 23, aliuawa kwa kupigwa risasi baada kufanya shambulio hilo.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema IS bado ni kitisho kwa nchi za magharibi na washirika wake katika nchi za Iraq na Syria walikuwa wanapanga mashambulio ya kutisha katika ardhi ya Uingereza.

Miili ya baadhi ya Waingereza waliouawa kwa kupigwa risasi katika shambulio la fukwe za Tunisia imewasili nchini Uingereza. Waziri mkuu alishindwa katika bunge miaka miwili iliyopita, wkati wabunge wa chama cha Labour walipoungana kupinga mashambulio ya anga katika maeneo yaliyokuwa yakishambuliwa na serikali ya Syria ili kuzuia matumizi ya silaha za kemikali ambazo zilihofiwa kutumiwa na serikali hiyo.

Lowasa awakemea wanaomuhusisha na ufisadi

Wafuasi wa mbunge wa Monduli, Edward Lowassa wakimsindikiza nje ya ofisi za CCM Makao Dodoma jana wakati wa kurejesha  fomu za kugombea urais.
 Dodoma. Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa jana aliwataka wanaomhusisha na ufisadi kuacha mara moja kwa sababu hakuna hata chembe ya ukweli katika tuhuma hizo.

Lowassa, aliyeonekana kuzungumza kwa hisia, alisema hayo jana mara baada ya kurejesha fomu ya kuwania kuteuliwa na CCM kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.

Mbunge huyo wa Monduli alikuwa mmoja kati ya makada tisa waliorudisha fomu jana, ikiwa ni siku moja kabla ya kuisha kwa muda uliowekwa na chama hicho. Wengine waliorejesha fomu jana ni Elidephonce Bilohe, Mwigulu Nchemba, Luhaga Mpina, Dk Hamisi Kigwangalla, Hassy Kitine, Mariki Marupu, Dk Asha Rose Migiro na Lazaro Nyalandu.

Hadi sasa, tayari wanachama 32 kati ya 42 wa CCM walioomba kuteuliwa na chama hicho kugombea urais wamerudisha fomu na kazi hiyo itahitimishwa leo.

Hakuna mtu ambaye amejitokeza hadharani kumtuhumu Lowassa kwa ufisadi, lakini tuhuma hizo zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii, hasa kutokana na mbunge huyo wa Monduli kujiuzulu nafasi ya Waziri Mkuu mwaka 2008 baada ya kuibuka sakata la mkataba wa ufuaji umeme wa dharura baina ya Serikali na Kampuni ya Richmond RDC ya Marekani ambayo ilionekana haina uwezo.

Wakati huo, Lowassa alisema kwenye hotuba yake ya kujiuzulu kuwa amefanya uamuzi huo “ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji, lakini kutokubaliana na utaratibu uliotumika wa kusema uongo ndani ya Bunge kwa kumsingizia mtu.”

Akizungumza jana kwenye ofisi za makao makuu ya CCM, Lowassa alirudia wito wake wa kutaka wenye ushahidi wa tuhuma hizo wajitokeze hadharani.

“Nataka nitumie fursa hii kuwataka wale wote ambao wamekuwa wakinituhumu kwa miaka kadhaa sasa na kunihusisha na suala zima la rushwa, nawaambia waache mara moja, kwani hakuna chembe hata ya ukweli wa maneno hayo,” alisema.

“Natoa changamoto kwa yeyote mwenye ushahidi wa tuhuma hizo za kipuuzi, autoe na aeleze kwa ushahidi rushwa yoyote inayonihusu, aseme nimechukua lini, kwa nani, kwa lipi na kiasi gani?”

Alisema yeye ni mwadilifu na anaposema atasimamia vita dhidi ya rushwa atafanya hivyo kwa vitendo bila kumuonea mtu na bila kumuonea haya yeyote.

“Ndugu wanachama wenzangu na wananchi kwa jumla, ni lazima sasa tufike mahali tuseme imetosha. Majungu yametosha, upotoshwaji umetosha, rushwa imetosha na kwa pamoja tunaweza kukomesha haya. Tutayakomesha kwa kusimamia ukweli, uadilifu, uaminifu na kutenda kwa haki,” alisema.

Ukumbi wa Whitehouse, jana ulijaa wana-CCM ambao walifika kushuhudia Lowassa akirudisha fomu tofauti na idadi iliyowahi kutokea kwa wagombea wengine kadhaa waliomtangulia. Hali hiyo ilisababisha foleni kwenye Barabara ya Mtaa wa Kuu unaopita mbele ya ofisi za CCM, na kusababisha usumbufu kwa wapita njia.